Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwahiyo gentleman,Think tank na Mbobevu wa Genge la wahuni ngazi ya Taifa.
Kwanini unafikiri wengine waligoma kuendelea na mdahalo wao?Angekuja kwenye mdahalo ili tuone kama hakuna wa kufanya nae mdaharo!
Mbona Nchimbi mwenyewe aliukimbia mdahalo?Kwanini unafikiri wengine waligoma kuendelea na mdahalo wao?
Hivi Akina mwashambwa niwatu wa wapi?Ndugu zangu Watanzania,
Sasa mnaweza kuelewa ni kwanini Edwin Odemba alilia na kububujikwa machozi hadharani kama mtoto mdogo pale alipoona Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi ameshindwa kufika na kuhudhuria kwenye mdahalo kutokana na kutingwa na majukumu ya chama ,ambapo alikuwa anaendesha vikao vya Secretarieti katika maandalizi ya vikao vya kamati Kuu.
Mnaweza sasa kuelewa ni kwanini na wengine waliokuwepo wa CHADEMA na Act Wazalendo waligoma kuendelea na mdahalo bila uwepo wa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi.mnaweza kuelewa kiu na shauku kubwa ya washiriki kutamani uwepo wa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi.
Siyo kwamba washiriki na waandaaji walitaka kwenda kufanya mdahalo na Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi. Bali waandaaji walitaka kwenda kujifunza na kupata ufafanuzi wa Masuala mbalimbali,walitaka kwenda kuuliza mambo mbalimbali yanayowasumbua akili zao,walikuwa na maswali ya kuuliza na siyo hoja za kwenda kujadili na kujadiliana na Katibu mkuu wa CCM.
Ndio maana baada ya kukosekana kwake Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi waliamua na kuona hakuna sababu ya kuendelea na mdahalo,maana wao wanajuwa uwezo mkubwa wa kiakili,uzoefu wa kiuongozi,umakini ,utulivu na maarifa makubwa aliyonayo Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi ,na ndio sababu waliona ni nafasi ya kipekee kwa wao kwenda kujifunza na kuongeza maarifa . na hivyo kukosekana kwake kukawa hakuna sababu ya wao kuendelea na mazungumzo kwa sababu mwenye majibu na Mkata kiu yao na wakuwasaidia hayupo.
Kwa hiyo siku nyingine waandaaji wasiseme na kuita mdahalo bali waseme maswali mbalimbali kwenda kwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi juu ya masuala mbalimbali.kwa sababu simuoni mwenye uwezo wa kufanya mdahalo na Katibu mkuu wetu kwa makatibu wakuu wa vyama vya upinzani vilivyopo hapa Nchini.
Kinachopaswa kufanywa na makatibu wakuu wa vyama vya upinzani ni kuendelea kujifunza kutoka kwa katibu mkuu wa CCM. Kwa hakika Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi ni hazina kwa CCM na Taifa letu kwa ujumla wake.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Basi wangeupa jina lingine na siyo kusema mdahalo.Mi nadhani makatibu wengine walihairisha mdaharo siku ile kwa sababu wengi walienda pale wakiwa na maswali yao muhimu na mtu pekee alietakiwa kuulizwa hakufika.
Unadhani kwamba Mnyika anaweza kumuuliza kativu wa ACT juu ya utekaji na mfumuko wa bei!
Washington na NewYork Marekani na wengine Paris Ufaransa,huku wengine wakiwa wa Amsterdam uholaanzi.Hivi Akina mwashambwa niwatu wa wapi?
Alikuwa kwenye vikao.Mbona Nchimbi mwenyewe aliukimbia mdahalo?
Unazingua Kaka badilika basiWashington na NewYork Marekani na wengine Paris Ufaransa,huku wengine wakiwa wa Amsterdam uholaanzi.
Hahaha, siasa za wapi izo!Watawaletea majibu waulize maswali.au kama wewe una maswali nipe hata mimi nipande gari nipeleke ofisini.
Nazingua nini.Unazingua Kaka badilika basi
Hata CHADEMA wanamkubali sana Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi.
Dr. Nchimbi amekulia mjini Dar es Salaam kama Freeman Mbowe na John John Mnyika, hivyo anajua jinsi ya kuongea na watoto wa mjini wenzie kuhusu masuala ya siasa
View: https://m.youtube.com/watch?v=RPqhXYKDPA4
Siyo suala la kukulia Mjini bali ni suala la uelewa wa mtu na akili. Mbona wapo wengi wamezaliwa mjini lakini ni vichwa maji tu.
Nimeshatoa ufafanuzi kuwa alikuwa kwenye vikao vizito sana vya sekretarieti ambapo yeye anakuwa ni Mwenyekiti wa vikao hivyo. Kwa hiyo ulitaka aache vikao hivi vizito vinavyotoa Dira na muelekeo wa nchi ,halafu aende huko kwenye kuulizwa maswali ambayo hata mimi naweza kuwajibu hapa jukwaani?Dakta Nchimbi aliingia Mitini na Nchi nzima iliona na kusikia sasa wanakutuma wewe uje ujaze serva za JF kwa kububujikwa na Uharo.
Kwanini aahidi kuwa atahudhuria?!Nimeshatoa ufafanuzi kuwa alikuwa kwenye vikao vizito sana vya sekretarieti ambapo yeye anakuwa ni Mwenyekiti wa vikao hivyo. Kwa hiyo ulitaka aache vikao hivi vizito vinavyotoa Dira na muelekeo wa nchi ,halafu aende huko kwenye kuulizwa maswali ambayo hata mimi naweza kuwajibu hapa jukwaani?
Onyesha barua aliyoahidi kuwa atahudhuria.Kwanini aahidi kuwa atahudhuria?!