Imejitokeza sintofahamu ya watoto kupotea na kukutwa wakiwa wamefariki huku miili yao ikiwa haina baadhi ya viungo, mamlaka ichuke hatua stahiki

Imejitokeza sintofahamu ya watoto kupotea na kukutwa wakiwa wamefariki huku miili yao ikiwa haina baadhi ya viungo, mamlaka ichuke hatua stahiki

Hizo ni takwimu za kwenye makaratasi lakini uhalisia sivyo.

Tunajitangaza sana huko nje kwamba Tz ni nchi ya Amani lakini uhalisia wa ndani ya nchi sivyo.
Sasa mbona mwanzo ulisema Tanzania haipo hata Top 100. Ulitumia Source gani?

Halafu kuwa na amani ndio kumaanisha hakuna mauaji kabisa? Hata nchi zilizoizidi amani Tanzania kuna wakati hutokea mauaji.
 
Wakuu amani ya Mungu iwe nanyi.

Kumekua na taharuki kwa wakazi wa Temeke, Tandika, Mbagala na Vikindu kwa ujumla wake.

Imejitokeza sintofahamu ya watoto kupotea na kukutwa wakiwa wamefariki huku miili yao ikiwa haina baadhi ya viungo.

Majuma kadhaa yaliyopita maeneo ya Mbagala Mgeni nani miili ya watoto imekutwa huku baadhi ya viungo vikiwa havipo.

Pia soma: Ukatili: Mtoto auawa na kukatwa sehemu za siri

Wiki iliyoisha maeneo ya Tandika mtoto wa jirani yangu alikoswa kuchukuliwa na watekaji mara baada ya kufanya jaribio la kumteka mtoto, bahati nzuri mtoto alikimbia na kuja kusimulia kwa wazazi wake.

Juzi maeneo ya Kisemvule inaripotiwa mama mjamzito amekutwa amefariki huku sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa.

Jana maeneo ya vikindu(kazole) nimepewa taarifa ya kukutwa kwa miili ya watoto wawili wanaodaiwa kuwa na miaka kati ya 11 mpaka 14 ikiwa haina baadhi ya viungo.

Vyombo vya habari mpaka sasa sijasikia ikiripoti tokio lolote kati ya hayo juu au yanayo shaabiana na hayo.

Rai yangu kwa mamlaka husika tunaomba wanaotenda haya matukio muwashughulikie haraka sana watatumalizia watoto wetu na jamaazetu.

====

Pia soma: Kagera: Mwanafunzi auawa, mwili watupwa kichakani
Tuombe MUNGU uchaguzi mkuu upite kwani haya yote yataisha!!!
 
Jana imetokea huku Dodoma Nyumba 300 mtoto amekutwa amekufa baada ya kupotea..ametupwa karibu na nyumba za hapo....nimeona kwny group moja...
Jamani ni kina nani hawa wanafanya hivi kwa watoto wasio na hatia jamani...tena wa umri kuanzia miaka 4....
 
Back
Top Bottom