Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Kwanza nitangulie kusema kuwa sina chuki waka hila na mh. Waziri Mkuu Majaliwa. Waziri mkuu ndiye msimamizi wa shughuli ZOTE za kiserikali nchini.
Hata hivyo hili nililolisikia kwenye vyombo vya habari ndiyo vinaelezea ukakasi wa siasa tunazojiwekea zisivyoendana na kanuni na utaratibu wa hususan suala la ujenzi nchini.
Mh Waziri Mkuu anaonekana akimkaripia Daktari wa binadamu kwa ujenzi hafifu hasa milango katika hospitali ya Namtumbo huko Ruvuma.
Huyo Daktari anaonekana wala hajui kitasa na bawaba vinapatikana wapi!
Lakini inakuwaje madudu haya hayakuonekana mapema, ilhali wasimamizi wa mradi wapo, Mtendaji wa Halmashauri yupo, Mkuu wa Wilaya Yupo, Mkuu wa Mkoa yupo.
Waziri Mkuu atakagua yeye mwenyewe miradi mingapi kuibua madudu?
Hata hivyo, tunavuna tulichopanda, shoddy workmanship na ukanjanja katika ujenzi.
Hayo ndio matokeo ya FORCE ACCOUNT tuliyopigia kelele sana huko nyuma.
Jengo limekamilika ndiyo kwa fedha kiduchu, wanasiasa wanasema "value for money".
Lakini sasa ndio tunaona the real poor value for cheap and shoddy works, cannot endure durability in time of say 10 yrs.
Kifupi wanasiasa walioingiza FORCE ACCOUNT arbitralily katika sekta ya ujenzi watavuna matokeo mabaya hata kabla ya kumaliza muda wao madarakani.
Kitaalam tunahitaji kuwa na Technical Audit kwa miradi yote iliyotekelezwa kwa Force Account ili yafanyiwe tathmini na marekebisho kama hilo alilogundua Waziri Mkuu.