Imekaaje Waziri Mkuu kumkaripia Daktari kwa ujenzi hafifu wa Hospitali?

Imekaaje Waziri Mkuu kumkaripia Daktari kwa ujenzi hafifu wa Hospitali?

Shukrani sana kwa kuniongezea msamiati, shoddy workmanship, nimekupata. Ukiwa nje unahisi Force Account inamsaidia mhitaji, ukiwa ndani ya mfumo utatambua fika kuwa force account ni kichaka cha kupigia fedha kwa wakubwa.

Yaani mtaalam wa Wizara au sekta fulani anasimamia mradi kwa kulipwa DSA (daily subsistence allowance), wakubwa wanabakia ofisini wakisubilia kuongeza sufuri kwenye figure ya BOQ.

Utasikia mradi huu umetekelezwa kwa kuwatumia wataalam wetu wa ndani, na tumeweza kuokoa kiasi fulani cha fedha, watu wote meno nje, hakuna anayejiuliza hili swali, baada ya kuokoa kiasi fulani cha fedha, kimepelekwa wapi na kufanya nini?

NAOMBA NA HILI MKALITIZAME😀😀😃
 
Daktari ana mzigo mkubwa sana wa kutoa huduma kwa wagonjwa atashughulikia mangap kwa mda mmoja...
Waziri mkuu kitaaluma ni mwalimu naye hana utaalamu wowote wa ujenzi lakini kaona hayo madudu bila kanuni za kihandisi, je tunahitaji kweli elimu ya uhandisi kujua ratio ya mchanga na simenti haipo sawa ili kubaini tofali lisilo na ubora?

Waziri mkuu asimuulize DED juu ya utumikaji wa pesa kwa kuwa DED sio mtaalamu wa fedha?
 
Ha ha ha !
Mbona unaunga mkono kilichaofanyika na kuhoji uhaali wake.
Jibu unalo!
nnachomaanisha me waziri matatizo yake naa daktari ana matatizo yake

waziri kasimama km kiongozi maana yake ana haki ya kuoji juu ya anaowaongoza.

ila daktari na yeye ilikuwaje kuwaje akapokea majukumu yasiyomuhusu au kwa vile aliskia kuna vipesa kdg akakujua na yy atalamba pesa kdg
 
Waziri mkuu kitaaluma ni mwalimu naye hana utaalamu wowote wa ujenzi lakini kaona hayo madudu bila kanuni za kihandisi, je tunahitaji kweli elimu ya uhandisi kujua ratio ya mchanga na simenti haipo sawa ili kubaini tofali lisilo na ubora?

Waziri mkuu asimuulize DED juu ya utumikaji wa pesa kwa kuwa DED sio mtaalamu wa fedha?

Aaaah🤔🤔🤔
 
nnachomaanisha me waziri matatizo yake naa daktari ana matatizo yake

waziri kasimama km kiongozi maana yake ana haki ya kuoji juu ya anaowaongoza.

ila daktari na yeye ilikuwaje kuwaje akapokea majukumu yasiyomuhusu au kwa vile aliskia kuna vipesa kdg akakujua na yy atalamba pesa kdg
Procurement officer wa taasisi ni mkuu wa sehemu husika kama ilivyo kwa accounting officer. Mkurugenzi sio mhasibu ila ndio accounting officer.
 
Kwenye makala yako hii nakunukuu, "Mkuu Wa mkoa tupo". Ina maana wewe ni miongoni mwao sa kwa nini uje kumsema Bosi wako huku ilhali we ni miongoni mwa wazembe?
 
Mganga yupo hapo hapo na anaona kinachoendelea kila siku sasa atashindwaje kupita hata wakati anaingia kazini asubuhi na kuwahi hata nusu kabla?

Wanajua ni msala wao huo maana hela zimeingia huko

Kweli wana majukumu mengi lakini hata kuangalia kinachoendelea kashindwa? Tuna matatizo ya akili wengi
 
View attachment 2391683

Kwanza nitangulie kusema kuwa sina chuki waka hila na mh. Waziri Mkuu Majaliwa. Waziri mkuu ndiye msimamizi wa shughuli ZOTE za kiserikali nchini.

Hata hivyo hili nililolisikia kwenye vyombo vya habari ndiyo vinaelezea ukakasi wa siasa tunazojiwekea zisivyoendana na kanuni na utaratibu wa hususan suala la ujenzi nchini.

Mh Waziri Mkuu anaonekana akimkaripia Daktari wa binadamu kwa ujenzi hafifu hasa milango katika hospitali ya Namtumbo huko Ruvuma.

Huyo Daktari anaonekana wala hajui kitasa na bawaba vinapatikana wapi!
Lakini inakuwaje madudu haya hakakuonekana mapema, ilhali wasimamizi wa mradi wapo, Mtendaji wa Halmashauri yupo, Mkuu wa Wilaya Yupo, Mkuu wa Mkoa tupo.
Waziri Mkuu atakagua yeye mwenyewe miradi mingapi kuibuua madudu?

Hata hivyo, tunavuna tulichopanda, shoddy workmanship na ukanjanja katika ujenzi.

Hayo ndio matokeo ya FORCE ACCOUNT tuliyopigia kelele sana huko nyuma.

Jengo limekamilika ndiyo kwa fedha kiduchu, wanasiasa wanasema "value for money".
Lakini sasa ndio tunaona the real poor value for cheap and shoddy works, cannot endure durability in time of say 10 yrs.

Kifupi wanasiasa walioingiza FORCE ACCOUNT arbitralily katika sekta ya ujenzi watavuna matokeo mabaya hata kabla ya kumaliza muda wao madarakani.

Kitaalam tunahitaji kuwa na Technical Audit kwa miradi yote iliyotekelezwa kwa Force Account ili yafanyiwe tathmini na marekebisho kama hilo alilogundua Waziri Mkuu.
😁😁
Kwamba daktari anatakiwa kuwa na taaluma ya uhandisi🤔
Tatizo ni kuwa wanasiasa hawataki kuheshimu taaluma za watu.
Yeye apelekwe theater hospitalini akasimamie upasuaji wa mgonjwa tuone kama ataweza
 
Madaktari walipewa dhamana ya Kusimamia hiyo miradi kama ilivyo kwa wakuu wa shule.... Pesa ziliwekwa kwenye akaunti za taasisi husika hivyo kwa vyovyote vile daktari anahusika....
Mkuu, udaktari na masuala ya ujenzi mbona kama haviendani?
 
Hata kama ni chuki kwa waziri mkuu sasa zimekuzidi mpaka zinakuondoa akili kabisa ya kufikiria.

Naomba nikujibu kama utanielewa. Mara zote muwajibikaji mkuu ni mkuu wa sehemu husika ambao ni CEO au DG au DED na vivyo...
Mkuu jiridhishe kwamba wewe ni mbumbumbu wa kazi za miradi.

Mradi unapojengwa huwa unakuwa chini ya Clien(serikali)t, ambapo hapo ni wizara ya Afya na siyo Daktari.
Na Client hawezi kuhamishia majukumu ya usimamizi wa mradi kwa mtu ambaye hajauasisi.

Na hio ndio tatizo la viongozi/wanasiasa wengi.

Wao wanafikiria kiserikali kazi yao ni kutafuta fedha tu, usimamizi utafanywa na kilaza yeyote aliyekaribu, na mara nyingi hajui hata mradi wenyewe.

Katika hili, Daktari hapo hajui msingi unajengwaje wala wapi dawa ya mchwa unaokula mbao, na hata mix ya zege inaendaje.

Ujenzi wa mradi kiserikali katika miaka ya karibuni umefanywa kiholela kabisa kwa kutumia ati Force Account.
Kuna madudu mengi tu tutayagundua huko mbele ya safarai.

Mradi unapokwisha , sasa ndio operational staff wanaingia, yaani wakabidhiwa mradi wanaingia, madaktari na manesi, na waiguzi , wanapewa jengo lao.

Inabidi tukuelimisheni fani hii ya ujenzi, siyo lelemama.


Kwa utkekezaji wa mradi
 
Hata kama ni chuki kwa waziri mkuu sasa zimekuzidi mpaka zinakuondoa akili kabisa ya kufikiria.

Naomba nikujibu kama utanielewa. Mara zote muwajibikaji mkuu ni mkuu wa sehemu husika ambao ni CEO au DG au DED na vivyo...
Mkuu, labda niseme tu kwamba "waafrika bado tuna safari ndefu sana ya kuja kuwa kama wazungu kwenye suala zima la maendeleo"
 
Kwenye makala yako hii nakunukuu, "Mkuu Wa mkoa tupo". Ina maana wewe ni miongoni mwao sa kwa nini uje kumsema Bosi wako huku ilhali we ni miongoni mwa wazembe?
Imeahihishwa mkuu!
Mimi mbeba zege!!
 
waziri namlaumu kwa kushindwa kuchukua hatua na kuishia kukaripia watu

kuna milango kakuta ndo imepakwa vanish siku iyo
hapo ilitakiwa mkurugenzi, mkuu wa wilaya na wahusika wengine kuwaondoa kazini ye anaishia kuwakaripia
 
Mkuu, kwa hiyo daktari akijenga nyumba yake binafsi atapigwa sana sababu hajui chochote kuhusu ubora kwenye ujenzi, pamoja na kwamba si taaluma yake na yeye ana macho anaona na pia anayo nafasi ya kufanya consultation kwa wataalamu husika ndani ya halmashauri na wengine wengi wamejaa huko mitaani.​
Mkuu, yaani mradi wa serikali mtu akaombe consultation mtaani? Kila mmoja aifanyie kazi taaluma yake. Kuna vijana wengi sana ambao ni civil engineers hawana ajira mnaoweza kuwapa kazi hizo kwa muda kama mlivyofanya kwa makarani wa sensa.
 
Shukrani sana kwa kuniongezea msamiati, shoddy workmanship, nimekupata. Ukiwa nje unahisi Force Account inamsaidia mhitaji, ukiwa ndani ...
Mkuu uliloibua ni suala la msingi sana ambalo wanaobeba bango la kupendelea Force Account hawapendi lionekane kwa vile wanafaidika kwa pesa ya mradi.
 
Jidu La Mabambasi

Hueleweki unatetea nini katika andiko lako.

Je!
Ni waziri kumkaripia Daktari mkuu wa hospitali husika?

Au ni kuiponda "FORCE ACCOUNT"kwa sababu kuna namna inaondoa ule upigaji wa kimfumo?
 
Back
Top Bottom