Tatizo sio kusimamia. Liliagizwa lijengwe kwa shilingi ngapi? Je hicbo kiasi ndicho kinachotakiwa kujenga jengo la hospitali kwa ukubwa huo na standard inqyotakiwa? Hapi naona ni siasa inatumika kulaumu asiyestahili. Ukweli ukiwekwa wazi unaweza kuta hao wanaolaumu ndio wa kulaumiwa na sio watekelezaji.Waziri Mkuu anafanya vema kuonyesha usimamizi mbovu wa miradi.
Lakini nijiulize, nani alisimamia hili jengo hadi kukamilika?
Mfano unaweza kuta Halmashauri inahitaji majengo ya vyumba vya madarasa kumi na gharama za madarasa hayo ni sh milioni 300 lakini inaletwa hela milioni mia na unaambiwa lazima ijenge madarasa ku.mi na utumie force account yaani kila darasa milioni kumi. Afisa wa wilaya anamuita fundi na kumwambia nataka unijengee darasa kwa sh milioni 10 halafu darasa likikamilika kiongozi anataka liwe bora, mbao za milango na madirisha zikiwa ni sypras au bqti kikiwa geji 33 ushangae. Ndio maana mafundi wengine ukiwaambie wajenge kwa kiasi kidogo cha pesa wanakataa hiyo kazi kwa,sababu wanajua huko mbeleni itakuwa awama.
Utaratibu wa ujenzi jengo la umma lazima lichorwe, materials yote yatakayotumika yaainishwe na bei halisi za hayo meterials pamoja na gharama za ufundi ( BoQ inaandaliwa kabisa) ndipo anatqfutwa kqndarasi anajenga kwa kufuata michoro na anakaguliwa na consultant hatua kwa hatua na kulipwa kwa kila hatua, katika mazingira haya jengo likiwa halina viwango ni rahisi kumbana kandarasi na consultant aliyekuwa anaidhinisha kila hatua iliyojengwa kabla ya kandarasi kulipwa kwa kila hatua. Lakini force account haina michoro wala BoQ .