Imekaaje Waziri Mkuu kumkaripia Daktari kwa ujenzi hafifu wa Hospitali?

Imekaaje Waziri Mkuu kumkaripia Daktari kwa ujenzi hafifu wa Hospitali?

Shukrani sana kwa kuniongezea msamiati, shoddy workmanship, nimekupata. Ukiwa nje unahisi Force Account inamsaidia mhitaji, ukiwa ndani ya mfumo utatambua fika kuwa force account ni kichaka cha kupigia fedha kwa wakubwa.

Yaani mtaalam wa Wizara au sekta fulani anasimamia mradi kwa kulipwa DSA (daily subsistence allowance), wakubwa wanabakia ofisini wakisubilia kuongeza sufuri kwenye figure ya BOQ.

Utasikia mradi huu umetekelezwa kwa kuwatumia wataalam wetu wa ndani, na tumeweza kuokoa kiasi fulani cha fedha, watu wote meno nje, hakuna anayejiuliza hili swali, baada ya kuokoa kiasi fulani cha fedha, kimepelekwa wapi na kufanya nini?

NAOMBA NA HILI MKALITIZAME😀😀😃

Ulitegemea nini kwa mtu ambae anasema yeye ni Muislamu, akaingia msikitini siku tukufu ya Ijumaa akiwa amevalia kinadhifu sana kisha akasimama mbele ya membar na imam wa msikiti na akathubutu kusema kuwa Rais wa Tanzania ni mzima na anawasalimu ilhali akijua wazi kuwa Rais ni mgonjwa/ameshaaga dunia?
 
  • Kicheko
Reactions: BRB
Hata kama ni chuki kwa waziri mkuu sasa zimekuzidi mpaka zinakuondoa akili kabisa ya kufikiria.

Naomba nikujibu kama utanielewa. Mara zote muwajibikaji mkuu ni mkuu wa sehemu husika ambao ni CEO au DG au DED na vivyo hivyo kwa upande wa hospitali za mikoa na wilaya ni waganga wafawidhi. Hao waganga wafawidhi ndio wasimamizi wa uendeshaji wa shughuli na ndio wawajibikaji wakuu wa maeneo hayo.

Pale waziri mkuu hajamkaripia daktari kama unavyotaka kupotosha ila amekaripiwa mtu ambaye alitakiwa kuhakikisha ubora na ufanisi.

Najua utaniuliza mganga mfawidhi atajuaje ubora wa vifaa vya ujenzi? Kwanza alitakiwa kufanya kazi kwa karibu na wataalamu ili wamsaidie vyema. Pia, kilichofanyika kwenye hiyo milango ni uhuni kabisa na wala hahitaji kuwa na elimu kubwa kujua kuna ubovu.

Mwisho, mpaka suala linaloonekana kwa macho kabisa kwamba ni bovu na bado wahusika hawakuona kuna mawili either milango hiyo ilikusudiwa kuwekwa kwa namna hiyo au kuna upigaji wa kutisha?
Sasa una muwajibisha daktari wa binadamu kwenye issue ya ubora wa kazi ya ujenzi utakua na akili kweli?
 
Achana na huyo dogo ana kasumba ya migomo na maandamano. Hajui hata afisa manunuzi mkuu ni nani?
Ni aibu mtu anajipambanua kujua wakati hajui. Vijana wakiwa shule hii kitu inafundishwa maana wanategemewa kuwa ma Afisa Masuhuri. Accounting Officers na kutokana na PPRA huwezi jitetea ati wewe umesomea ukulima etc! Barikiwa
 
Waziri

Hebu zitaje kashfa tatu tu tusikie
Namsaidia moja Kawadanganya kwa makusudi mazima waislamu na watanzania kwa ujumla siku ya ijumaa kasimama mbele ya kibla na mbele ya imamu wa msikitini na akasema uongo juu ya hali ya Magufuli
 
waziri ana haki ya kumkalipia daktari km daktari ndio alipewa dhaman ya kusimamia ujenzi wa hospital.

ila je kwa akil ya kawaid tu daktari anaweza kusimamia maswala la ujenzi [emoji848]
Ndio maana utagundua wanasiasa wa bongo ni vimeo. Nilitarajia ded aitwe na ded amuite injinia wake wa ujenzi. Baada ya hapo ndio injinia wa ujenzi atoe maelezo.
 
Mkuu, kwa hiyo daktari akijenga nyumba yake binafsi atapigwa sana sababu hajui chochote kuhusu ubora kwenye ujenzi, pamoja na kwamba si taaluma yake na yeye ana macho anaona na pia anayo nafasi ya kufanya consultation kwa wataalamu husika ndani ya halmashauri na wengine wengi wamejaa huko mitaani.​
Tunaongelea kituo cha afya cha serikali na sio nyumba binafsi.
 
Kwanza nitangulie kusema kuwa sina chuki waka hila na mh. Waziri Mkuu Majaliwa. Waziri mkuu ndiye msimamizi wa shughuli ZOTE za kiserikali nchini.

Hata hivyo hili nililolisikia kwenye vyombo vya habari ndiyo vinaelezea ukakasi wa siasa tunazojiwekea zisivyoendana na kanuni na utaratibu wa hususan suala la ujenzi nchini.

Mh Waziri Mkuu anaonekana akimkaripia Daktari wa binadamu kwa ujenzi hafifu hasa milango katika hospitali ya Namtumbo huko Ruvuma.

Huyo Daktari anaonekana wala hajui kitasa na bawaba vinapatikana wapi!

Lakini inakuwaje madudu haya hayakuonekana mapema, ilhali wasimamizi wa mradi wapo, Mtendaji wa Halmashauri yupo, Mkuu wa Wilaya Yupo, Mkuu wa Mkoa yupo.
Waziri Mkuu atakagua yeye mwenyewe miradi mingapi kuibua madudu?

Hata hivyo, tunavuna tulichopanda, shoddy workmanship na ukanjanja katika ujenzi.

Hayo ndio matokeo ya FORCE ACCOUNT tuliyopigia kelele sana huko nyuma.

Jengo limekamilika ndiyo kwa fedha kiduchu, wanasiasa wanasema "value for money".
Lakini sasa ndio tunaona the real poor value for cheap and shoddy works, cannot endure durability in time of say 10 yrs.

Kifupi wanasiasa walioingiza FORCE ACCOUNT arbitralily katika sekta ya ujenzi watavuna matokeo mabaya hata kabla ya kumaliza muda wao madarakani.

Kitaalam tunahitaji kuwa na Technical Audit kwa miradi yote iliyotekelezwa kwa Force Account ili yafanyiwe tathmini na marekebisho kama hilo alilogundua Waziri Mkuu.
Napingana na wewe kuhusu Force Acvount maana hata hao wakandarasi unao wataka wewe pia miradi yao inamapungufu MENGI TU
 
Napingana na wewe kuhusu Force Acvount maana hata hao wakandarasi unao wataka wewe pia miradi yao inamapungufu MENGI TU
Uwe concise, hatuongelei makandarasi, tunaongeea ujenzi mzima.
Kwa kufuatilia Ujenzi na kanuni zake, mkandarasi hawezi kurupuka kwenda kujenga kama hakuna-
- Architect(Mbunifu majengo),
-Consulting/Design Engineer(Engineer anayefanya mahesabu ya nondo, zege zinazoingia kwenye jengo)
-Quantity Surveyor(Mkadiriaji gharama za jengo),
-Clerk of Works( Msimamizi wa mradi kil siku
- na vile vile kazi kukaguliwa na mamlaka tofauti zihusuzo ijenzi kama AQRB, ERB, CRB na mamlaka nyingine.

Huo ndio ujenzi tunaoufhamu , sasa Fosi Akaunti mlie tu.
 
Namsaidia moja Kawadanganya kwa makusudi mazima waislamu na watanzania kwa ujumla siku ya ijumaa kasimama mbele ya kibla na mbele ya imamu wa msikitini na akasema uongo juu ya hali ya Magufuli
Uongo upi aliosema. We unajuaje kama ulikua uongo?
 
Madaktari walipewa dhamana ya Kusimamia hiyo miradi kama ilivyo kwa wakuu wa shule.... Pesa ziliwekwa kwenye akaunti za taasisi husika hivyo kwa vyovyote vile daktari anahusika....

MAMBO YA AJABU KABISA,Daktari na ujenzi wapi na wapi!!!!!!!!!!upumbavu wa hali ya juu!!huyu Waziri atakua CHOKO
 
Tatizo sio kusimamia. Liliagizwa lijengwe kwa shilingi ngapi? Je hicbo kiasi ndicho kinachotakiwa kujenga jengo la hospitali kwa ukubwa huo na standard inqyotakiwa? Hapi naona ni siasa inatumika kulaumu asiyestahili. Ukweli ukiwekwa wazi unaweza kuta hao wanaolaumu ndio wa kulaumiwa na sio watekelezaji.

Mfano unaweza kuta Halmashauri inahitaji majengo ya vyumba vya madarasa kumi na gharama za madarasa hayo ni sh milioni 300 lakini inaletwa hela milioni mia na unaambiwa lazima ijenge madarasa ku.mi na utumie force account yaani kila darasa milioni kumi. Afisa wa wilaya anamuita fundi na kumwambia nataka unijengee darasa kwa sh milioni 10 halafu darasa likikamilika kiongozi anataka liwe bora, mbao za milango na madirisha zikiwa ni sypras au bqti kikiwa geji 33 ushangae. Ndio maana mafundi wengine ukiwaambie wajenge kwa kiasi kidogo cha pesa wanakataa hiyo kazi kwa,sababu wanajua huko mbeleni itakuwa awama.

Utaratibu wa ujenzi jengo la umma lazima lichorwe, materials yote yatakayotumika yaainishwe na bei halisi za hayo meterials pamoja na gharama za ufundi ( BoQ inaandaliwa kabisa) ndipo anatqfutwa kqndarasi anajenga kwa kufuata michoro na anakaguliwa na consultant hatua kwa hatua na kulipwa kwa kila hatua, katika mazingira haya jengo likiwa halina viwango ni rahisi kumbana kandarasi na consultant aliyekuwa anaidhinisha kila hatua iliyojengwa kabla ya kandarasi kulipwa kwa kila hatua. Lakini force account haina michoro wala BoQ .
Kwa hiyo unataka kutuambia kwamba chumba kimoja cha darasa milioni kumi haijengi?
 
Uongo upi aliosema. We unajuaje kama ulikua uongo?
Kwani Magu alionekana tena akiwa hai toka siku ile. Amka wewe hadi lini mtakuwa namna hii? Tanzania inahitaji mabadiliko na mabadiliko hayaji kama mtakaa tu mkikubali kudanganywa kijinga bila ya kutumia akili zenu. Kila mnachoambiwa na Viongozi wenu mnaamini tu hamuulizi masuali na wala hamjumlishi moja na moja mkapa 2. Amkeni!!!!!
 
Tulia wewe, swala la Magu kuonekana na alichosema waziri mkuu vina uhusiano gani? Waziri mkuu alisema Rais yupo anafanya kazi zake, prove kuwa alidanganya. We unajua Rais alikua wapi na akifanya nini muda waziri mkuu anaongea hivyo? Unasema alidanganya based on what? Wewe unaongea tu kwasababu upo nyuma ya keyboard, wewe ndio ungekua waziri mkuu ungesemaje? Unadhani taarifa inayohusiana na rais wa nchi unajiropokea tu kama unamuongelea gigi money au juma nature?
 
Ni ujinga. Daktari siyo engineer.

Hii nchi viongozi wamejenga tabia ya kutafuta sifa na umaarufu kwa kufoka mbele ya kamera ama kusimamisha mtu kazi ndiyo .

Kila wilaya kuna mhandisi qmbaye kazi yake ni kusimamia ujenzi na kukagua ubora wa miradi iweje alaumiwe daktari?

Yaani huu ujinga utatuchelewesha Sana.
Ma"engineer" wamekosa uaminifu kwa sababu walikuwa wanapiga Sana huko nyuma ...

NI MARA KUMI PROJECT ISIMAMIWE NA NON-ENGINEER PROFIT INAONEKANA KULIKO HAWA ENGINEERS WETU WA MICHONGO
 
Kwanza nitangulie kusema kuwa sina chuki waka hila na mh. Waziri Mkuu Majaliwa. Waziri mkuu ndiye msimamizi wa shughuli ZOTE za kiserikali nchini.

Hata hivyo hili nililolisikia kwenye vyombo vya habari ndiyo vinaelezea ukakasi wa siasa tunazojiwekea zisivyoendana na kanuni na utaratibu wa hususan suala la ujenzi nchini.

Mh Waziri Mkuu anaonekana akimkaripia Daktari wa binadamu kwa ujenzi hafifu hasa milango katika hospitali ya Namtumbo huko Ruvuma.

Huyo Daktari anaonekana wala hajui kitasa na bawaba vinapatikana wapi!

Lakini inakuwaje madudu haya hayakuonekana mapema, ilhali wasimamizi wa mradi wapo, Mtendaji wa Halmashauri yupo, Mkuu wa Wilaya Yupo, Mkuu wa Mkoa yupo.
Waziri Mkuu atakagua yeye mwenyewe miradi mingapi kuibua madudu?

Hata hivyo, tunavuna tulichopanda, shoddy workmanship na ukanjanja katika ujenzi.

Hayo ndio matokeo ya FORCE ACCOUNT tuliyopigia kelele sana huko nyuma.

Jengo limekamilika ndiyo kwa fedha kiduchu, wanasiasa wanasema "value for money".
Lakini sasa ndio tunaona the real poor value for cheap and shoddy works, cannot endure durability in time of say 10 yrs.

Kifupi wanasiasa walioingiza FORCE ACCOUNT arbitralily katika sekta ya ujenzi watavuna matokeo mabaya hata kabla ya kumaliza muda wao madarakani.

Kitaalam tunahitaji kuwa na Technical Audit kwa miradi yote iliyotekelezwa kwa Force Account ili yafanyiwe tathmini na marekebisho kama hilo alilogundua Waziri Mkuu.
Halafu hiyo milango usiione hivyo, haifungi. Jana nimeona mara tatu PM anaamuru mlango ufungwe halafu unafunguka wenyewe kila ukifungwa; mara tatu. Yaani mimi ilibidi nicheke kwa sababu sikuwepo kwenye tukio. Huwezi ukacheka ukiwepo LIVE.
 
Back
Top Bottom