Imekaaje Waziri Mkuu kumkaripia Daktari kwa ujenzi hafifu wa Hospitali?

Waziri Mkuu anafanya vema kuonyesha usimamizi mbovu wa miradi.
Lakini nijiulize, nani alisimamia hili jengo hadi kukamilika?
Tatizo sio kusimamia. Liliagizwa lijengwe kwa shilingi ngapi? Je hicbo kiasi ndicho kinachotakiwa kujenga jengo la hospitali kwa ukubwa huo na standard inqyotakiwa? Hapi naona ni siasa inatumika kulaumu asiyestahili. Ukweli ukiwekwa wazi unaweza kuta hao wanaolaumu ndio wa kulaumiwa na sio watekelezaji.

Mfano unaweza kuta Halmashauri inahitaji majengo ya vyumba vya madarasa kumi na gharama za madarasa hayo ni sh milioni 300 lakini inaletwa hela milioni mia na unaambiwa lazima ijenge madarasa ku.mi na utumie force account yaani kila darasa milioni kumi. Afisa wa wilaya anamuita fundi na kumwambia nataka unijengee darasa kwa sh milioni 10 halafu darasa likikamilika kiongozi anataka liwe bora, mbao za milango na madirisha zikiwa ni sypras au bqti kikiwa geji 33 ushangae. Ndio maana mafundi wengine ukiwaambie wajenge kwa kiasi kidogo cha pesa wanakataa hiyo kazi kwa,sababu wanajua huko mbeleni itakuwa awama.

Utaratibu wa ujenzi jengo la umma lazima lichorwe, materials yote yatakayotumika yaainishwe na bei halisi za hayo meterials pamoja na gharama za ufundi ( BoQ inaandaliwa kabisa) ndipo anatqfutwa kqndarasi anajenga kwa kufuata michoro na anakaguliwa na consultant hatua kwa hatua na kulipwa kwa kila hatua, katika mazingira haya jengo likiwa halina viwango ni rahisi kumbana kandarasi na consultant aliyekuwa anaidhinisha kila hatua iliyojengwa kabla ya kandarasi kulipwa kwa kila hatua. Lakini force account haina michoro wala BoQ .
 
Wewe tatizo lako ni utoto unakusumbua. Daktari ni procurement entity na ni kiongozi, hivyo anatakiwa kujua hivi vitu!!!!!
 
Jidu La Mabambasi

Hueleweki unatetea nini katika andiko lako.

Je!
Ni waziri kumkaripia Daktari mkuu wa hospitali husika?

Au ni kuiponda "FORCE ACCOUNT"kwa sababu kuna namna inaondoa ule upigaji wa kimfumo?
Mkuu naona tatizo hulioni bayana!
Waziri Mkuu anasimamia miradi yote ndani ya serikali, hilo ni jukumu lake na kwa kweli hana makosa kumchukulia hatua mtu yeyote aliye chini yake , alimradi anavurunda.
Ndiyo kazi yake.

Lakini sera mbovu za utekelezaji wa miradi ndiyo imempelekea Waziri Mkuu kumkaripia Daktari ambaye hana taaluma yoyote katika ujenzi.
Thats the paradox!
Unamtandika punda kwa kushindwa kuogelea kama samaki.

Kimsingi inabidi serikali itambue kuwa haya ndio madhara ya sera za kuitumia Force Account kwenye miradi ya serikali, badala ya traditional project management and execution method.

Miradi ya Force Account , iliyosimamiwa na watu wasion na utaalam wa ujenzi inabidi yote ifanyiwe tathmini ya ubora wake, kabla hayajatokea madudu kama alivyoyaona Waziri Mkuu hadharani.
 
Labda huko kusini hakuna ma engineer mpaka madaktari wanafanya procurement Hadi usimamizi wa majengo.
Wafanye mpango waajiri regional engineer na district engineers.
 
Wewe tatizo lako ni utoto unakusumbua. Daktari ni procurement entity na ni kiongozi, hivyo anatakiwa kujua hivi vitu!!!!!
Procurement ya dawa na vifaa vya fani yake ya uDaktari, ndiyo haswa eneo lake.

Elewa kuwa daktari hawezi ku procure jengo la mabilioni.
Usipolielewa hilo basi hapo ulipo wewe ni mzigo.
 
Madaktari walipewa dhamana ya Kusimamia hiyo miradi kama ilivyo kwa wakuu wa shule.... Pesa ziliwekwa kwenye akaunti za taasisi husika hivyo kwa vyovyote vile daktari anahusika....
Je ilikuwa ni sahihi, madaktari kuwa wasimamizi wa miradi wasio na taaluma nazo ?!
 
Asante sana mkuu.
Umelieeza tatizo kwa njia rahisi na inayoeleweka kwa kile kinachofaanyika kule mikoani.
Tatizo wanasiasa wamelifumbia macho hili tatizo.
Makandarasi na wataalam wa ujenzi Engineers, Quantity Surveyors na Architects wamekuwa wakilililalamikia sana suala hili.
 
Procurement ya dawa na vifaa vya fani yake ya uDaktari, ndiyo haswa eneo lake.

Elewa kuwa daktari hawezi ku procure jengo la mabilioni.
Usipolielewa hilo basi hapo ulipo wewe ni mzigo.
Naongea kitu nafahamu dogo
 
Mkuu, labda niseme tu kwamba "waafrika bado tuna safari ndefu sana ya kuja kuwa kama wazungu kwenye suala zima la maendeleo"

Naongea kitu nafahamu dogo
Achana na huyo dogo ana kasumba ya migomo na maandamano. Hajui hata afisa manunuzi mkuu ni nani?
 
PM anatafuta publoc sympathy atupishe......amechafuka kashfa kibaoooo
 
Hakika ni ya ajabu sana
Nchi hii ya ajabu sana
Daktari anaacha taaluma yake anatakiwa kusimamia ujenzi
Mwalimu mkuu hafundishi kazi kusimamia ujenzi wa madarasa
Hivi ile PWD iliyokuwa inasimamia kazi zote za ufundi za serikali ilifia wapi?
 
Madaktari wala wakuu wa shule hawapaswi kusimamia miradi ya ujenzi kwani sio taaluma yao na pia wana majukumu mengine mazito na ya msingi zaidi.
Madaktari walipewa dhamana ya Kusimamia hiyo miradi kama ilivyo kwa wakuu wa shule.... Pesa ziliwekwa kwenye akaunti za taasisi husika hivyo kwa vyovyote vile daktari anahusika....
 
Atapigwa kama amewapa hiyo kazi ya kujenga vibaka wasiozingatia taaluma yao.
 
Waziri Mkuu anafanya vema kuonyesha usimamizi mbovu wa miradi.

Lakini nijiulize, nani alisimamia hili jengo hadi kukamilika?
Ishu hapa ni kumfokea mtu asiyestahili, MP was barking at a wrong tree.
 
Mafisadi yanamuwinda waziri mkuu ila hawindiki, analindwa na nguvu ya wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…