Imekaaje Waziri Mkuu kumkaripia Daktari kwa ujenzi hafifu wa Hospitali?

Kwa hio atibu binadamu na hapo hapo asimamie ujenzi.. khee
 
Halafu hiyo milango usiione hivyo, haifungi. Jana nimeona mara tatu PM anaamuru mlango ufungwe halafu unafunguka wenyewe kila ukifungwa; mara tatu. Yaani mimi ilibidi nicheke kwa sababu sikuwepo kwenye tukio. Huwezi ukacheka ukiwepo LIVE.
Milango ya kusimamiwa na daktari wakati wa fosi akaunti!
 
Ma"engineer" wamekosa uaminifu kwa sababu walikuwa wanapiga Sana huko nyuma ...

NI MARA KUMI PROJECT ISIMAMIWE NA NON-ENGINEER PROFIT INAONEKANA KULIKO HAWA ENGINEERS WETU WA MICHONGO
Utakuwa mwansiasa wewe, kajijengee basi na jengo ulilolibuni wewe mwenyewe.
 
hapo wa kwanza alikuwa mkurugenzi,engineer halafu pia daktari.huyo daktari alitakiwa kujiridhisha na ubora wa kazi ile sababu ndo mwenye ofisi na engineer anatakiwa kuwajibishwa na mkurugenzi wake. vitasa vinajulikana tu wapi vinapatikana sababu naamini huyo daktari amewahi kujenga lkn pia anaishi kwenye nyumba.hivi vitu ni very simple kama akili yako iko sawa.unaona kabisa mlango una nafasi na kitasa kimekaa kiajabu huwezi hoji hapa kulikoni!hapana vitu vingine vinafanya viongozi kuwa vichaa sababu ya upuuzi tu mdogomdogo.kwani waziri mkuu ni injia lkn kaonaje hiyo kasoro si ni uzoefu tu.jamani hebu tuwe serious wakati mwingine.
 
N Nyie watoto wa juzi hamjui kuwa katika kuajiriwa kuna kitu kinaitwa Job Description.
Mtu anapewa ajira na madaraka kulingana na fani aliyosomea.
 
Yaani huo ni ujinga tu na kutafuta umaarufu mbele ya kamera.
Ukiangalia hii nchi yetu inakabiliwa na upungufu au uchache wa madaktari katika sekta ya afya, hospital Moja si ajabu ukute wagonjwa 200 na daktari mmoja. Alafu huyo huyo daktari mmoja anaweza kuwa tegemezi vituo vya afya zaidi ya kimoja. Je huo mda wa kusimamia ujenzi unatoka wapii??

Yaan hii nchi basi tu. Ni kama gari inayo endeshwa na walevi.
 
Mkuu hizo ndo kasoro za serikali yenyewe kujifanyia maamuxi yasiyo na tija kiutendaji.
Force Account inabidi ipigwe marufuku, amasivyo Waziri Mkuu akakague mwenyewe miradi yote ya serikali.
 
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hayo mambo yalianzishwa na boss ya huyu PM sababu rejea kisa cha kule bandari yule mama alivyoambiwa unanijibu mimi hivyo?

Yaani mama yuko kitengo kingine anaulizwa maswali ya kitengo kingine si maajabu hayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…