Yaani ukifatilia mambo ya Katibu Mwenezi Paul Makonda utaishia kucheka tu. Sometime hata kupatwa na hasira au huzuni.
Katibu Mwenezi hana ajenda wala hajajipanga. Anajitwangia tu.
Tumesikia Mwanasheria akilalamika kuhusu utendaji wake. Si yeye tu wapo wanachama wengi wenye heshima zao ndani ya chama hicho wamekosoa mienendo ya kile kinachoitwa uenezi.
Tulitarajia Awe na Agenda zinazogusa Maslahi ya Wananchi kama vile
1. Hali ya Uchumi kudorora
2. Utitiri wa kodi na kupanda bei za bidhaa
3. Maendeleo ya huduma za kijamii hasa Maji, Umeme na Afya
4. Elimu bora na maIngira bora ya watendaji hasa walimu.
5. Utawala wa Haki, Sheria na kuzingatia Katiba.
Badala yake akikuta daraja limeanguka analivaa.....akikuta barabara imejaa vumbi analo.
Akikuta Eng wa Nkoa kagombana na mke wake basi yeye anakuwa msuluhishi.
Mimi naona kama Katibu Mwenezi ame loose focus na kukosa Mwelekeo.
Kama Chama kingekuwa kinategemea Kura kurudi madarakani basi huu ndio Ungekuwa Mwisho wa Uhai wa ccm.
Huyo Jaji Mkuu aliyelalamika ni Mnafiki tu japo ni home boy wangu, ni Mnafiki sawa na Mtoa mada....!
System ya Nchi na Viongozi wa Umma na namna wanavyofaya kazi kwa mazoea, kwa Upendeleo, ndo Wamechangia Matatizo yote haya ambayo tunaona namna Wananchi Masikini wakijaribu bahati yao kwa Makonda kuona labda Watasaidika....!
Anachokifanya Makonda si Kigeni, Mfano nilikua nasikia Malalamiko ya Mmoja ya Watumishi wa Halmashauri moja ambaye amestaafu miaka mingi ilopita, Manispaa kupitia Mkurugenzi wamegoma Kumlipa pesa zake, huyu Mwana Mama hakuna office hajaenda, kuanzia kwa Diwani, Mbunge, Mkuu wa Wilaya mpaka Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi mwenyewe akikataa kumlipa malipo yake, mtu kama huyu ataenda wapi tena kudai haki zake, bahati Makonda kaenda, katatua tatizo lake mbele ya Mkutano na Mkurugenzi anaulizwa sababu za kushindwa kumlipa mama wa watu hana hata cha kujitetea, kapewa maelekezo amlipe mdai siku iliyofuata.
Leo pia nimeangalia Mzabuni akiidai Manispaa ya Sumbawanga, Deni la toka mwaka 2012, just imagine, huyu naye kahangaika kila sehemu, bila mafanikio, anaitwa Mkurugenzi anasema watamlipa mwaka wa fedha 2024, Makonda akasema haiwezekani kwanza anadai muda mrefu, katoa maelezekezo kwa Mkurugenzi kesho yake asubuhi, awe ameandaa Cheque ya Mdai...!
Hiyo ni mifano michache kati ya Mingi, sasa wananchi masikini kama hawa wataenda wapi kudai haki zao dhidi ya Mfumo wa Uongozi ulio fail..!?
Always nasema, siipendi CCM, simkubari Makonda, lakini nakubaliana na anachofanya, kile anafanya ni Masikini tu ndo ataelewa...!
Mtu kama Jaji Mkuu, na yeye office haijawahi kushughurika na Masikini wa Nchi...! Nakubaliana na Majibu ya Makonda kwa wote, kuwa kila mtu afanye Yake....!