Nilimwelewa Mwanasheria wa Serikali kwamba ziara ya Mwenezi imemfumbua ufahamu kwamba wananchi wana changamoto nyingi sana ambazo hazijapatiwa ufumbuzi.
AG alienda mbali na kusema ataunda kikosi kazi ili kutatua changamoto hizo ambazo nyingi ni za kisheria, haki, wajibu na uwajibikaji.
Binafsi, ziara za Makonda zimenifundisha kitu, kwamba wananchi hawana tatizo lingine kubwa zaidi ya kukosa sehemu ya kupeleka kero zao.
Wenyeviti wa Vitongoji, Watendaji wa Mitaa/Vijiji, Kata na Katibu Tarafa wanahitaji waongeze nguvu katika kushughulika na kero za wananchi.