Unaelewa ziara ya Mheshimiwa mwamba mwenyewe na Jabali wa siasa na jasiri kusini mwa jangwa la sahara Mheshimiwa Makonda imelenga nini? Imedhamilia nini?
Ngoja nikujibu kwa ufupi tu kulingana na ufupi wa akili yako.
Ziara ya Mheshimiwa Makonda ina lengo kwanza la kukagua utekelezaji wa ilani ya chama.kwa hiyo chama kina angalia namna miradi mbalimbali inayotekelezwa,kasi yke katika utekelezaji wa miradi pamoja na kuangalia uwajibikaji wa viongozi na watendaji wa serikali katika utekelezaji wa majukumu yao.
Pili ni kusikiliza na kutatua papo kwa papo kero za wananchi. Kwa hiyo ziara hiyo ya chama inakwenda kwa wananchi kuwasikiliza kero zao zote,ikiwa ni pamoja na namna wanavyohudumiwa na serikali yao, changamoto zao zinavyotatuliwa.ndio maana unaona namna ambavyo chama kimeendelea kuwapokea watu wa aina mbalimbali wenye kero na kutatua kero zao lakini katika mchakato huo chama kinatoa maagizo kwa viongozi wa serikali mikoani kuanzisha kliniki ya kupokea na kusikiliza kero za wananchi pamoja na kutatua ,ambapo agizo hilo la chama limetekelezwa haraka sana na kwa sasa kliniki hizo zimeshaanza kazi mikoa yote hapa nchini.
Tatu ziara hiyo imekuwa katika kuangalia uhai wa chama,l wa namna kinavyokubalika, kupendwa,kuungwa mkono na nguvu yake .ambapo chama kimeona kuwa bado kina nguvu kubwa sana ya ushawishi kwa wananchi,bado kinaaminika,bado kinaungwa mkono,bado kinapendwa sana na mamilioni ya watanzania na ndio maana watu wanamiminika na kufurika kwa wingi sana katika mikutano ya CCM inayoongozwa na Mheshimiwa Makonda katika ziara hiyo ya kihistoria hapa nchini.
Kwahiyo usikurupuke katika kuandika vitu usivyo vielewa.ni bora ingetuuliza wenye chama chetu ili tukupatie majibu.