Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Hizi Taasisi kubwa kama IMF na Benki ya Dunia huwa wana taratibu za kujidhihirisha kabla ya kumpokea mgeni kutoka nchi fulani ambae huteuliwa kuwa waziri wa fedha.
Dr Phillip Mpango ni mwenyeji katika taasisi hizi za fedha duniani.
Ukiongelea masuala ya uchumi na Dr Mpango hupati shaka kwamba ameiva kiuchumi na anafahamu kazi yake.
Dr Mpango amewahi kuongoza TRA, tume ya mipango, naibu katibu mkuu wizara ya fedha, mshauri wa raisi katika masuala ya uchumi na pia mchumi mwandamizi katika Benki ya Dunia.
Dr Mpango pia amekuwa mjumbe katika kamati mbalimbali za mabenki kama Benki ya maendeleo ya Afrika, taasisi ya uwekezaji ya MIGA na mjumbe wa kikundi cha benki ya dunia au World Bank Group.
World Bank Group ni taasisi maalum iliyo chini ya umoja wa mataifa inayoshughulikia madeni nafuu kwa nchi zinazoendelea.
Hivyo Dr Mpango ana uzoefu wa kukaa meza moja na taasisi hizi na kutoa ushawishi wake dhidi ya madeni mabivu au makali na yanayoumiza.
Nimezikiliza mahojiano kati ya waziri wa fedha wa sasa Dr Mwigulu Nchemba katika kipindi cha Clouds na naweza kusema kuwa hafai kuendesha wizara ya fedha.
Dr Mwigulu hana taarifa mkononi kwa majibu yake maalum khasa jibu la tozo ya miamala.
Masuali mengi ya kiuchumi Dr Nchemba ameyatolea majibu yasiyo ya kiuchumi yaani yasiyo na ushahidi khasa katika suala la kwanini tozo za mafuta na miamala zimewekwa sasa hivi na yeye asisitiza uzalendo.
Endapo bado vyombo vya IMF na World Bank bado havijaridhishwa na uteuzi wa Dr Nchemba, wale wanohusika na kupendekeza majina wafirie upya juu ya majina haya mawili Dr Nchemba na Dr Mpango.
Dr Nchemba (kuanzia dakika ya 30) adai eti nchi hii ina walipa kodi wakubwa 500,000 na walipa kodi wa kawaida wakiwemo wafanyakazi wapatao milioni 3.
Kama kweli nchi ina walipa kodi wakubwa laki tano na walipa kodi wa kawaida (waloandikishwa rasmi) milioni 3.1 ndani ya idadi ya watanzania milioni 66, basi nchi hii ina shida kubwa huko mbele.
Inawezekana kulikuwepo na kupitiwa katika kuangalia ni yupi awe makamu wa raisi na yupi aende Hazina.
Ila kwenye hili washauri mmepotea na mrudi ubaoni twaita "going back to the drawing board".
Taasisi za kimataifa kama IMF na World Bank zahitaji watu makini na huwa ni lazima wajiridhishe na ntu atakaeketi nao mezani kufanya mazungumzo.