IMF yaidhinishia Tanzania mkopo wa Trilioni 2.4
Tufahamu tu hizo ni pesa za mkopo tena zina msururu wa masharti kutoka kwa wakopeshaji, hivyo tutapaswa kuzilipa kwa faida na kufuata masharti yao.
Swali linakuja.
1. Tutazilipaje?
2. Zina masharti gani?
Hayatakusaidia maishani mwako, we tafuta hela za wajukuu wako.
Usiipende sana nchi
 
Habari inasema mkopo ni sehemu ya:

Extended credit facility (clearly kuna cash flow issues) na wamekwambia balance of payments.

Nchi inatakiwa ku implement sera za IMF kupata huo mkopo (SAP) na kiasi kadhaa cha hiyo hela inatumika kulipa matured debt payments.

In short nchi imefilisika, halafu watu wanashangilia. Kibaya zaidi kuna wizara zina tumia hela ovyo raisi anawaangalia tu.

Ni hivi huyu bibi wa ki Zanzibar hajali kuhusu mustakabali wa Tanzania ya kesho, kila siku tunajichimbia shimo. Yeye ilimradi wahuni wamlindie uraisi wake na wao waharibu nchi wanavyoweza in return.
 
Muwe mnafuatilia mipango ya Serikali nyie watu wajinga wajinga wa miaka hii..

Nani aje akutafute wewe as an individual? Serikali imeandaa mipango na inawalenga wakulima lakini kutafuta fursa ni wewe hapo sio Serikali ikutafute, vinginevyo mtaishia kulalamika hovyo mitandaoni..

Moja ya hizo fursa ni hizi hapa [emoji116]
Kijana punguza majibu ya kejeli kwa wenzako. Nyakati hupita. Kama unalamba asali kwa sasa acha kuwaita wenzako ambao wamekosa fursa kua ni "watu wajinga wajinga wa miaka hii". Kumbuka nothing is permanent na hakuna shida isiyoisha. Leo unajiona mwamba kwa kuwadharau wengine, ipo siku utawalilia hao hao unaowadharau wakusaidie wewe au kizazi chako.

Hayo ni maoni yangu tu ukipenda yachukue ukiona hayafai achana nayo.
 
Kwani kabla ya hapo ushoga haukuwepo? Tanzania hakuna ushoga?
Tofautisha kati ya mtu kuamua kuwa shoga na Ushoga kukubalika rasmi kwenye nyaraka za serikali hivyo ndoa za jinsia moja kutambulika rasmi na kufungishwa na wasajili wa ndoa na kupewa vyeti vya ndoa hizo. Nadhani umenielewa!

Ushoga upo kwa kiasi fulani kila nchi. Lakini Hauna baraka za serikali.
 
Tofautisha kati ya mtu kuamua kuwa shoga na Ushoga kukubalika rasmi kwenye nyaraka za serikali hivyo ndoa za jinsia moja kutambulika rasmi na kufungishwa na wasajili wa ndoa na kupewa vyeti vya ndoa hizo. Nadhani umenielewa!

Ushoga upo kwa kiasi fulani kila nchi. Lakini Hauna baraka za serikali.
Kuna athari Gani ikiwa hivyo? Japo hili haliwezekani kutokea hapa Tanzania..

Mfano wa Malawi sio sahihi kwa sababu za umuhimu wa Tanzania kwenye geopolitics.
 
Kuna athari Gani ikiwa hivyo?
Ebo! kumbe naongea na mtu ambaye hajui athari za kuruhusu ushoga rasmi!! Yaani mwanamume aolewe na mwanamume halafu wewe haujui athari zake? Ni kweli? Subiri mtoto wako wa kiume aolewe na dume mwenzake halafu usubiri wajukuu!!!
 
Waendelee kukopa sana, ila na sisi mtukopeshe huku kwenye kilimo. Una degree, una shamba, shamba lina miti ya miaka 10, unapeleka hati bank lakini bado unazungushwa kupewa hata milioni 1, ya kuimalisha kilimo. Sasa kama ajira hakuna basi tuwezesheni mikopo. Serikali inakopa, basi nasi tukopeshwe.
Sijui kwanini nguvu kubwa haipelekwi huko

Ova
 
Muwe mnafuatilia mipango ya Serikali nyie watu wajinga wajinga wa miaka hii..

Nani aje akutafute wewe as an individual? Serikali imeandaa mipango na inawalenga wakulima lakini kutafuta fursa ni wewe hapo sio Serikali ikutafute, vinginevyo mtaishia kulalamika hovyo mitandaoni..

Moja ya hizo fursa ni hizi hapa [emoji116]
Hizo ulizozionyesha hapo(Tamizi), ni stori tu katika nchi hii, watajijaza watoto wa wakubwa tu. Tumepewa Elimu ili itukomboe katika umasikini wetu, ndio maana tupo shamba na hiyo elimu yetu mwaka wa 12 huu. Kuhusu bank ya kilimo, au bank za serikali katika nchi hii huwa hazishughuriki na masikini au graduates, hukopeshana wao kwa wao. Ok, nimeweka elimu pembeni nimelima kwa nguvu zangu, nimewekeza kitu cha mamilioni, naenda benki ili nianze mnyololo wa kilimo biashara, benki inakubali, inanipitishia pesa , nasaini mkataba lakini inashindwa kuni - disburse, sababu ni hofu, inasita kwamba haituamini graduates ki vile. Nimegundua tatizo ni sera za nchi, ya kwamba inawaambia Vijana wajiajiri, huku haituamini kutuwezesha kupata nyenzo za kujiajilia(fedha/mitaji). Najua upo pazuri ndio maana umeniona mi mjinga, kula nchi brother.
 
Nikwambie kitu: Watazitoa kwa miezi 40 kwa kuwa mkopo huo ni mtego pia!! Watataka tukubaliane na mambo fulani fulani. Mkopo wenyewe unadai ni wa kufidia athari za vita vya urusi na Ukraine! Hapo ujue kabisa kutakuwa na sharti la kuilaani Urusi vinginevyo watatishia kuzuia mkopo! Wanaanza kwa kukulambisha kwanza kwa dola milioni 151.7 ili usikilizie utamu wake!! Ili sasa watakapokuwa wanatishia uwe unakumbukia utamu ulioonjeshwa!! Pili pamoja na kutakiwa kuilaani urusi kwa uvamizi wake kwa ukraine, watatutaka tuunge mkono vikwazo vya kiuchumi kwa urusi!! Kwa maneno mengine mkopo huu unaenda kutunyang'anya uhuru wetu!. Na mwisho tukitia ngumu tutatishiwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi wenyewe!! Huwezi ukaonjeshwa pesa ya beberu halafu ujifanye kichwa ngumu!! Tumejiweka kwenye hali ngumu sana!!
Mwacheni mama yenu akope tu ila siku yaja bendera ya rangi za upinde itavikwa kwenye V8 ya mama mkabala na bendera ya Tanzania kuwa imekubali na kuunadi Umende.
 
Nchi yangu TANZANIA ni TAJIRI.

Nataka kusikia ikikopesha mataifa mengine.

Nataka kusikia dhahabu, almasi na madini mengine Nchi ikiingia ubia na kupata 80% na mwekezaji alipata 20%.

Nataka kusikia Nchi yangu ikiilisha Africa nzima Kwa chakula, mapato ya ndani yasaidie kilimo Cha kisasa.

Nataka kusikia matumizi ya Serikali yakipungua na wakikipa Kodi.

Nataka kusikia ELIMU ya shule za selikali ikiwa Bora kuliko itolewayo na sekta binafsi kama enzi za mwl Nyerere.
Yote hayo ni kama kumpigia mbuzi gitaa katika awamu hii ya walamba asali.😂😂😂
 
Bodi ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeridhia Mkopo wa Dola za Marekani Bilioni 1.046 (Takriban Tsh. 2,422,536,000,000) kwa Tanzania katika kipindi cha miezi 40 kusaidia kukabiliana na athari za vita ya Urusi na Ukraine. Kiasi cha Dola za Marekani Milioni 151.7 kitatolewa mara moja.

Taarifa ya IMF inaeleza kuwa, vita hiyo inakwamisha Uchumi wa Tanzania kuimarika kufuatia mlipuko wa COVID-19, hivyo kuleta changamoto zaidi katika Maendeleo.

Tanzania ilishapokea Mkopo wa Dola Milioni 567 mwishoni mwa 2021 ili kukidhi mahitaji yake ya dharura wakati Mlipuko wa Virusi vya Corona ulipoathiri Maendeleo ya Kiuchumi, hususan Sekta ya Utalii kwa kiasi kikubwa

=========

The International Monetary Fund said Monday it has granted Tanzania a $1.046-billion loan over 40 months, primarily to help the country cope with the consequences of the war in Ukraine.

"Spillovers from the war in Ukraine are stalling the Tanzanian economy's gradual recovery from the Covid-19 pandemic, exacerbating the country's development and reform challenges to unleash its economic potential," the IMF said in a statement.

As a result, the fund's experts believe that the African country will need help to carry out reforms and "unleash its economic potential."

Tanzania is to immediately receive the equivalent of $151.7 million. It had already received a loan of $567 million at the end of 2021 to meet its most urgent needs, when the Covid-19 pandemic had severely hampered its economic development, particularly in the tourism sector.

The war in Ukraine has caused food and fuel prices to soar worldwide, and the rise in wheat prices is "particularly worrying," said the IMF in a recent report entitled "A new shock and little room for maneuver," because sub-Saharan Africa imports 85 percent of its cereal consumption, with particularly high amounts going to Tanzania, Ivory Coast, Senegal and Mozambique.

The project that was announced on Monday, which is part of the Extended Credit Facility (ECF), should help finance reforms to improve Tanzania's financial stability, carry out public investments and support the private sector.

"Recognizing Tanzania's strong track record in reform implementation, directors supported the authorities' requests for an ECF arrangement to meet pressing financing needs," said Bo Li, an IMF official quoted in the statement.

Among other objectives, he also mentioned the importance of continuing vaccination campaigns on a larger scale

Source >>> IMF greenlights $1 bn loan to Tanzania
Nawaza tu kimya kimya kunasiku like neno LA yule boss aliyeabdikishwa kufutwa kazi lutatimilika.. Shart moja LA kuoga kwa mwafrika lazima avue nguo..
B
 
Back
Top Bottom