IMF yatoa orodha ya nchi 15 zenye uchumi mkubwa Afrika. Tanzania yashika namba 9 ikiwa na uchumi wa Dola Bilioni 80

Aisee haya mambo ya uchumi haya balaa tupu. Uchumi wa ukweli mimi naona boora upimwe na uwezo wa watu kupata mahitaji yao ya kila siku huku kukiwa na thamani ya hela yao ila haya ya kuambiwa kwenye makaratasi mmh!!
 
Kwamba kwa hali hii tunayoiona Tanzania tupo top ten ya largest economies za Africa?

Basi Africa ni masikini sana.
Afrika ni masikini sana. GDP yetu Tanzania ni hela ya bilionea mmoja tu wa Marekani. Mfano Elon Musk alitoa Cash USD Bilioni 44, yaani zaidi ya nusu ya GDP yetu kununua twitter na bado ana utajiti wa kutosha. Yaani mtu atoe nusu ya utajiri wa Tanzania kama vile ananunua pipi na bado hatetereki.
 
Familia A ina watu 3 na assets zenye thamani ya dola milioni 3.

Familia nyingine ina watu 10 na assets zenye thamani ya dola milioni 5.

Umeona tofauti hapo?
That is okay but inapokuja kwenye uhalisia haiko hivyo maana itategemea nani anamiliki hiyo GDP inayozaa huo mgawanyo.

Huko Equatorial Guinea 90% ya uchumi wao ni Mafuta na pesa zote zinaingiza Serikalini.

Je Serikali inawagawia pesa? Jibu ni hapana so hata Kama Kwa calculation Wana per Capita income kubwa ila ukweli ni kwamba uchumi wao unamilikiwa na Serikali,real perchasing power Yao ni zero.

Mwisho GDP isalie kuonesha Ukubwa wa Uchumi wa Nchi ila isitumiwe kupata Per Capita kama Kipimo Cha loving standards hapana Bali Itumike HDI walau Ina components nyingi Zenye uhalisia.
 
Aisee haya mambo ya uchumi haya balaa tupu. Uchumi wa ukweli mimi naona boora upimwe na uwezo wa watu kupata mahitaji yao ya kila siku huku kukiwa na thamani ya hela yao ila haya ya kuambiwa kwenye makaratasi mmh!!
Of course ndio Uchumi wa kweli,ukisema utumie GDP na GDP per Capita utadanganywa maana inategemea zaidi hiyo GDP inamilikiwa na nani.

Eg unakuta Migodi michache ya Wazungu huko Shinyanga inasoma uchumi wa Shinyanga ni mkubwa ila tukija kwenye uhalisia Sasa unakuta wao ni mafukara afadhari ya mkulima wa koroshi wa Tandahimba.

So unapojadili hizi perameters za Uchumi uwe makini na uzielewe.
 
Acheni kujidanganya. Tanzania sisi tu masikini sana. Ethiopia GDP per Capita $ 1,900 while Tanzania $1,400. Tuna kazi kubwa mbele yetu. Tuombe Mungu stupatie viongozi maana mpaka sasa hatuna.
 
Unaonekana mjinga ,unaijua hata formular ya GDP?
View attachment 2973664
Nakusamehe kwa sababu hujui uchumi. Hizo data kwenye Citizen zina-reflect mazalisho - past investment na production, hebu tuambie mradi mmoja tu wewe Bibi ushungi umeubuni umezalisha ni upi? GDP inakuja kwa kuangalia investment na kuzalisha mali. Mwezio alikuwa anakopa anazalisha wewe unakopa unatoa ruzuku na kuwafidia vyeti fake
 
Issue sio una pato kubwa kiuchumi, issue ni uchumi wako umetapakaa kiasi gani kwenda sambamba na idadi ya watu waliopo.

Mfano rahisi ni huu.
Kuna kijiji A, ambapo kuna mabilionea wawili wakiishi wakiishi hapo wenye utajiri wa shilingi Trilioni 1 (bilioni 1000) na katika kijiji hicho hicho kaya zingine zilizobakia ziko 98 zenye utajiri usiozidi bilioni moja. (Hivyo pato la kijiji A ni bilioni 1001, yaani zaidi trilioni moja)
Jirani na hapo kuna kijiji B chenye pato la utajiri wa shilingi bilioni 200 huku utajiri huo ukiwa una milikiwa na kaya 100 zilizopo kwenye kijiji hicho (Hivyo pato la kijiji B ni bilioni 200).
Sasa kwa takwimu za kiuchumi kijiji A kina pato kubwa (lakini watu wake wengi hawana hicho kipato) na kijiji B kina pato kidogo zaidi (lakini watu wake wengi wana kipato kikubwa zaidi).

Hivyo sio jambo la ajabu kwa 100% kwa Kenya, Ethiopia, Angola, Nigeria au Tanzania (kupanda) kuwa na pato kubwa lakini umaskini upo mkubwa.
 
Hapana, hapo unadanganya. Wazungu hata wazawa wote wanalipa kodi, hata CSR zinalpwa. Kiukweli kwa nini wananchi ni fukara? Tatizo ni matumizi, wizi na rushwa. Kila mzungu analipa kodi, hizo pesa zinaenda wapi? Ofcourse to yourself and your son Abdul and cronies
 
Uchumi wa Nchi ila isitumiwe kupata Per Capita kama Kipimo Cha loving standards hapana Bali Itumike HDI walau Ina components nyingi Zenye uhalisia.
Mwisho wa siku utagundua kwamba HDI inawiana tahisili (directly proportional) na GDP.

Serikali maskini inakamua pesa kwa wananchi wake ili kujikimu na kujiendesha.

Serikali inayohodhi sehemu ya vyanzo vikuu vya mapato ni rahisi kujitegemea kuliko kuwaelemea raia wake.
 
Kitu kama mwaka 2022 kurudi nyuma Ghana alikuwa ana tukimbiza Tanzania ile mbaya ila sasa hivi tume mpita.
Ghana:
GDP $76.7bil. GDP per Capita $2,300
Tanzania:
GDP $85bil. GDP per Capita $1,400
Sasa tumewapita kwa kigezo kipi?
 
Japokuwa mimi binafsi simkubali mama Samia, hususani kwenye uwajibikaji, lakini kiukweli kwenye Uchumi, Siasa na Jamii amefanya pakubwa zaidi ya Magufuli.
Mama ameweza kuifungua nchi iliyokuwa gizani, kifungoni na kaburini. Yule mwamba wa Chato alituzika shimoni tukiwa wazima huku chawa wake wa kijani wakishangilia.
 
Ahsante mkuu
 
Aisee haya mambo ya uchumi haya balaa tupu. Uchumi wa ukweli mimi naona boora upimwe na uwezo wa watu kupata mahitaji yao ya kila siku huku kukiwa na thamani ya hela yao ila haya ya kuambiwa kwenye makaratasi mmh!!
Kipimo kizuri cha ubora wa maisha ya watu ni Human Development Index(HDI)
 
Hapo kwenye orodha ya pili
  • Misri,Algeria,Tunisia,Morocco na South Africa...pumzi zao ndiyo zimeishia hapo hawana kipya cha kufanya uchumi wao ukue kwa zaidi ya 7%
  • D.R.C na Ethiopia, hizi na za kuogopwa kwa maana zina utajiri wa kutosha na Idadi kubwa ya Rasilimali watu,
  • Machafuko nchini mwao yakipungua, zitakua kileleni
  • Nigeria ina nafasi ya kuwa kwenye Top 3 ,bado ina dirisha kubwa la kukua. Waache Rushwa, Utekaji
  • Kenya,Tanzania,Ivory Coast na Ghana ni mwendo wa kubadilishana nafasi tu.Hazipo serious ....
  • Tunisia ni ya 15 ,lakini ina miundombinu na huduma bora kuliko nusu ya nchi zilizo juu yake.
IIla naunga mkono hoja ya ERoni ,Afrika bado Maskini sana ....
Yani nchi yetu jinsi tunavyolia shida,,,Shule hazina matundu ya vyoo lakini ni moja ya nchi 10 Tajiri Afrika.
 
Kweli
Sisi bado masikini wa kutupa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…