IMF yatoa orodha ya nchi 15 zenye uchumi mkubwa Afrika. Tanzania yashika namba 9 ikiwa na uchumi wa Dola Bilioni 80

IMF yatoa orodha ya nchi 15 zenye uchumi mkubwa Afrika. Tanzania yashika namba 9 ikiwa na uchumi wa Dola Bilioni 80

Ameyumba sana miaka 2 iliyopita Hadi Kushindwa kulipa.madeni.

Japo Kwa Uchumi wao huo na idadi ya watu ukitafuta per Capita income wametuzidi parefu japo ukija kwenye real term value let say purchasing power parity naona wako vibaya Kwa sababu ya very high inflation(kwamba pesa Yao inanunua vitu vichache kuliko ya kwetu).
Aisee haya mambo ya uchumi haya balaa tupu. Uchumi wa ukweli mimi naona boora upimwe na uwezo wa watu kupata mahitaji yao ya kila siku huku kukiwa na thamani ya hela yao ila haya ya kuambiwa kwenye makaratasi mmh!!
 
Kwamba kwa hali hii tunayoiona Tanzania tupo top ten ya largest economies za Africa?

Basi Africa ni masikini sana.
Afrika ni masikini sana. GDP yetu Tanzania ni hela ya bilionea mmoja tu wa Marekani. Mfano Elon Musk alitoa Cash USD Bilioni 44, yaani zaidi ya nusu ya GDP yetu kununua twitter na bado ana utajiti wa kutosha. Yaani mtu atoe nusu ya utajiri wa Tanzania kama vile ananunua pipi na bado hatetereki.
 
Familia A ina watu 3 na assets zenye thamani ya dola milioni 3.

Familia nyingine ina watu 10 na assets zenye thamani ya dola milioni 5.

Umeona tofauti hapo?
That is okay but inapokuja kwenye uhalisia haiko hivyo maana itategemea nani anamiliki hiyo GDP inayozaa huo mgawanyo.

Huko Equatorial Guinea 90% ya uchumi wao ni Mafuta na pesa zote zinaingiza Serikalini.

Je Serikali inawagawia pesa? Jibu ni hapana so hata Kama Kwa calculation Wana per Capita income kubwa ila ukweli ni kwamba uchumi wao unamilikiwa na Serikali,real perchasing power Yao ni zero.

Mwisho GDP isalie kuonesha Ukubwa wa Uchumi wa Nchi ila isitumiwe kupata Per Capita kama Kipimo Cha loving standards hapana Bali Itumike HDI walau Ina components nyingi Zenye uhalisia.
 
Aisee haya mambo ya uchumi haya balaa tupu. Uchumi wa ukweli mimi naona boora upimwe na uwezo wa watu kupata mahitaji yao ya kila siku huku kukiwa na thamani ya hela yao ila haya ya kuambiwa kwenye makaratasi mmh!!
Of course ndio Uchumi wa kweli,ukisema utumie GDP na GDP per Capita utadanganywa maana inategemea zaidi hiyo GDP inamilikiwa na nani.

Eg unakuta Migodi michache ya Wazungu huko Shinyanga inasoma uchumi wa Shinyanga ni mkubwa ila tukija kwenye uhalisia Sasa unakuta wao ni mafukara afadhari ya mkulima wa koroshi wa Tandahimba.

So unapojadili hizi perameters za Uchumi uwe makini na uzielewe.
 
Kuna mda amefafanua vizuri kwenye comments za hapo awali.

Ethiopia Ina Pato ghafi kubwa na imeendelea sana tuu isipokuwa Wingi wa watu ukija kugawa na Pato lake Bado Iko kwenye Nchi maskini zaidi LDC ambako sisi Tanzania hatupo.

Ila ukienda kwenye Miji Yao na kulinganisha na sisi wametuzidi sana tuu but Kwa kuwa maendeleo sio mjini tuu na maendeleo ni watu popote waliopo basi tumewazidi ubora wa Maisha.
Acheni kujidanganya. Tanzania sisi tu masikini sana. Ethiopia GDP per Capita $ 1,900 while Tanzania $1,400. Tuna kazi kubwa mbele yetu. Tuombe Mungu stupatie viongozi maana mpaka sasa hatuna.
 
Unaonekana mjinga ,unaijua hata formular ya GDP?
View attachment 2973664
Nakusamehe kwa sababu hujui uchumi. Hizo data kwenye Citizen zina-reflect mazalisho - past investment na production, hebu tuambie mradi mmoja tu wewe Bibi ushungi umeubuni umezalisha ni upi? GDP inakuja kwa kuangalia investment na kuzalisha mali. Mwezio alikuwa anakopa anazalisha wewe unakopa unatoa ruzuku na kuwafidia vyeti fake
 
Issue sio una pato kubwa kiuchumi, issue ni uchumi wako umetapakaa kiasi gani kwenda sambamba na idadi ya watu waliopo.

Mfano rahisi ni huu.
Kuna kijiji A, ambapo kuna mabilionea wawili wakiishi wakiishi hapo wenye utajiri wa shilingi Trilioni 1 (bilioni 1000) na katika kijiji hicho hicho kaya zingine zilizobakia ziko 98 zenye utajiri usiozidi bilioni moja. (Hivyo pato la kijiji A ni bilioni 1001, yaani zaidi trilioni moja)
Jirani na hapo kuna kijiji B chenye pato la utajiri wa shilingi bilioni 200 huku utajiri huo ukiwa una milikiwa na kaya 100 zilizopo kwenye kijiji hicho (Hivyo pato la kijiji B ni bilioni 200).
Sasa kwa takwimu za kiuchumi kijiji A kina pato kubwa (lakini watu wake wengi hawana hicho kipato) na kijiji B kina pato kidogo zaidi (lakini watu wake wengi wana kipato kikubwa zaidi).

Hivyo sio jambo la ajabu kwa 100% kwa Kenya, Ethiopia, Angola, Nigeria au Tanzania (kupanda) kuwa na pato kubwa lakini umaskini upo mkubwa.
 
Of course ndio Uchumi wa kweli,ukisema utumie GDP na GDP per Capita utadanganywa maana inategemea zaidi hiyo GDP inamilikiwa na nani.

Eg unakuta Migodi michache ya Wazungu huko Shinyanga inasoma uchumi wa Shinyanga ni mkubwa ila tukija kwenye uhalisia Sasa unakuta wao ni mafukara afadhari ya mkulima wa koroshi wa Tandahimba.

So unapojadili hizi perameters za Uchumi uwe makini na uzielewe.
Hapana, hapo unadanganya. Wazungu hata wazawa wote wanalipa kodi, hata CSR zinalpwa. Kiukweli kwa nini wananchi ni fukara? Tatizo ni matumizi, wizi na rushwa. Kila mzungu analipa kodi, hizo pesa zinaenda wapi? Ofcourse to yourself and your son Abdul and cronies
 
Uchumi wa Nchi ila isitumiwe kupata Per Capita kama Kipimo Cha loving standards hapana Bali Itumike HDI walau Ina components nyingi Zenye uhalisia.
Mwisho wa siku utagundua kwamba HDI inawiana tahisili (directly proportional) na GDP.

Serikali maskini inakamua pesa kwa wananchi wake ili kujikimu na kujiendesha.

Serikali inayohodhi sehemu ya vyanzo vikuu vya mapato ni rahisi kujitegemea kuliko kuwaelemea raia wake.
 
Kitu kama mwaka 2022 kurudi nyuma Ghana alikuwa ana tukimbiza Tanzania ile mbaya ila sasa hivi tume mpita.
Ghana:
GDP $76.7bil. GDP per Capita $2,300
Tanzania:
GDP $85bil. GDP per Capita $1,400
Sasa tumewapita kwa kigezo kipi?
 
Japokuwa mimi binafsi simkubali mama Samia, hususani kwenye uwajibikaji, lakini kiukweli kwenye Uchumi, Siasa na Jamii amefanya pakubwa zaidi ya Magufuli.
Mama ameweza kuifungua nchi iliyokuwa gizani, kifungoni na kaburini. Yule mwamba wa Chato alituzika shimoni tukiwa wazima huku chawa wake wa kijani wakishangilia.
 
Kuna mda amefafanua vizuri kwenye comments za hapo awali.

Ethiopia Ina Pato ghafi kubwa na imeendelea sana tuu isipokuwa Wingi wa watu ukija kugawa na Pato lake Bado Iko kwenye Nchi maskini zaidi LDC ambako sisi Tanzania hatupo.

Ila ukienda kwenye Miji Yao na kulinganisha na sisi wametuzidi sana tuu but Kwa kuwa maendeleo sio mjini tuu na maendeleo ni watu popote waliopo basi tumewazidi ubora wa Maisha.
Ahsante mkuu
 
Aisee haya mambo ya uchumi haya balaa tupu. Uchumi wa ukweli mimi naona boora upimwe na uwezo wa watu kupata mahitaji yao ya kila siku huku kukiwa na thamani ya hela yao ila haya ya kuambiwa kwenye makaratasi mmh!!
Kipimo kizuri cha ubora wa maisha ya watu ni Human Development Index(HDI)
 
Shirika la Fedha la Kimataifa IMF liketoa orodha ya Nchi 15 Zenye Uchumi Mkubwa Barani Afrika huku Tanzania ikishika nafasi ya 9.

Kwenye orodha hiyo Nchi ya Afrika Kusini imeongoza na kuzipita Nigeria na Misri ambazo zimekuwa zikiongoza Kwa miaka Mingi.

Pia takwimu hizo zinaonesha kufanya vizuri Kwa Nchi Tajiri ya Rasilima ya Algeria ambayo imeshika nafasi ya 3 juu ya Nigeria.

Kana kwamba haitoshi Nchi ya Ivory Coast imezipita Ghana na Tanzania na kushika nafasi ya 8 kutoka nafasi za chini zaidi.

Uchambuzi zaidi imeonesha Angola imeporomoka kiuchumi kutokana na sababu ambazo jazijabainishwa.
View attachment 2973637

My Take
Takwimu hizi Huwa zinabadilika Kila mwaka kutegemeana na Taasisi inayotoa takwimu.

Mathalani WB Huwa wanakadiria Uchumi wa Tanzania kuwa Dola Bilioni 85 na sio 80 zinazotajwa na IMF kama inavyosomeka kwenye taarifa hii hapa IMF/WB: Ukubwa Wa Uchumi wa Tanzania Wafikia Dola Bilioni 85.4 Mwaka 2023 kutoka Dola Bilioni 70 Mwaka 2021

-----
View attachment 2973631

In 2024, Africa's economic landscape showcases a mix of resilience and challenges, with South Africa emerging as the continent's largest economy according to the latest IMF data. The International Monetary Fund (IMF) has released its rankings, highlighting the economies in Africa based on GDP figures for the year. These rankings shed light on the economic trajectories of various nations and forecast future trends within the region.

Top 15 African Economies

The IMF's latest report reveals the following ranking of Africa's largest economies in 2024:

Despite facing persistent macroeconomic challenges, the overall economic outlook for Africa remains stable. The IMF's projections indicate that South Africa, Egypt, Algeria, and Nigeria will maintain their positions as Africa's top four economies until 2030. Notably, South Africa is poised to surpass Nigeria and Egypt to become the continent's largest economy, benefiting from energy supply improvements and logistical enhancements.

Nigeria, once Africa's largest economy, has slipped to the fourth position in 2024. The nation is grappling with multiple economic hurdles, including a soaring inflation rate of 33%, a weakening currency, and the aftermath of government economic reforms. Last year, the Nigerian government implemented significant policy changes, such as ending petrol subsidies and allowing market forces to dictate the currency exchange rate, leading to a surge in living costs.

Furthermore, Nigeria faces acute dollar shortages crucial for imports, exacerbating its dependence on foreign goods. The Nigerian Naira remains substantially devalued against the dollar, impacting both consumer purchasing power and import-dependent sectors.

To combat rising inflation, the Central Bank of Nigeria recently raised interest rates to 24.75% and eliminated electricity tariff subsidies. These measures aim to stabilize prices and restore economic confidence amidst challenging circumstances.

Meanwhile, Egypt, which held the top economic position in 2023, is projected to slide to the second spot behind South Africa due to successive currency devaluations. Despite this setback, the IMF forecasts that Egypt could reclaim the top position by 2027, underscoring the country's economic resilience and recovery potential.

Looking ahead, the IMF's World Economic Outlook emphasizes the need for sustained reforms and investments to bolster Africa's economic resilience. Countries like Kenya are expected to climb in the rankings, surpassing economies such as Angola in the coming years. Ethiopia's economy, holding steady in the fifth position, is projected to maintain its standing until 2030.

Africa's economic trajectory underscores the importance of strategic policies and investments to mitigate challenges and unlock growth opportunities across the continent. As nations navigate complex economic landscapes, sustained reforms and international partnerships will play a pivotal role in shaping Africa's economic future.

Chanzo: Africa View Facts
Hapo kwenye orodha ya pili
  • Misri,Algeria,Tunisia,Morocco na South Africa...pumzi zao ndiyo zimeishia hapo hawana kipya cha kufanya uchumi wao ukue kwa zaidi ya 7%
  • D.R.C na Ethiopia, hizi na za kuogopwa kwa maana zina utajiri wa kutosha na Idadi kubwa ya Rasilimali watu,
  • Machafuko nchini mwao yakipungua, zitakua kileleni
  • Nigeria ina nafasi ya kuwa kwenye Top 3 ,bado ina dirisha kubwa la kukua. Waache Rushwa, Utekaji
  • Kenya,Tanzania,Ivory Coast na Ghana ni mwendo wa kubadilishana nafasi tu.Hazipo serious ....
  • Tunisia ni ya 15 ,lakini ina miundombinu na huduma bora kuliko nusu ya nchi zilizo juu yake.
IIla naunga mkono hoja ya ERoni ,Afrika bado Maskini sana ....
Yani nchi yetu jinsi tunavyolia shida,,,Shule hazina matundu ya vyoo lakini ni moja ya nchi 10 Tajiri Afrika.
 
Kweli
Tatizo la watanzania (baadhi, hasa chawa) ni kupenda kujisifu kwa vitu hata wasivyoelewa. Wanachojua tu ni 'pongezi kwa mama '. GDP, kama ilivyoletwa hapo na mleta mada ni pato ghafi jumla la taifa, ambalo ukigawia kwa idadi ya raia wa taifa husika, unapata Pato la wastani kwa kila raia wa nchi hiyo (GDP per Capita). Mfano: Tanzania GDP = $85 bil. ÷ 60mil. (population) =$ 1,417 approx; ndio pato la wastani la mtanzania kwa mwaka. Nchi ya Equatorial guinea GDP = $10bil. ÷ 1.7mil. (population) = $ 5.9mil. approx; ndio pato la Equato Guinean kwa mwaka. Kwa hiyo utaona Pato la wastani kwa raia wa E. Guinea ni zaidi ya mara nne ya lile la mtanzania. Tanzania ni nchi masikini- tena sana, ila hatungepaswa kuwa masikini- kiasi hiki kwa vile tuna rasilimali nyingi mno. Tatizo ni viongozi tulip nao (serikali ya ccm), ndio wa kulaumiwa. Serikali inapaswa kusimamia vizuri rasilimali za taifa hili, na kuwa na sera nzuri za kuvutia uwekezaji wenyewe tija, si Kila kitu unampa mwarabu kwa bei ya kutupa. Sasa hapa watu kazi kuimba tu mapambio mara pongezi, anaupiga mwingi, haijawahikutokea nk. Nasikia kuna 'slim' alisema 'nipeni hiyo bandari kila mwaka niwape pesa inayotosha bajeti yenu na mimi nibaki na faida'. Hata kama sio kweli angeweza kutupa pesa nyingi hivyo, lakini angalia ni kiasi gani anatudharau kwamba hatuwezi kusimamia rasilimali zetu.
Sisi bado masikini wa kutupa.
 
Back
Top Bottom