John the Baptist ni wale wale- anatetea bila utafiti! Hajafikiwa na mikasa kama hii! TRA wakitaka na wanataka kupiga hela, wanamtafuta mmiliki wa kampuni (Managing/Executive Director) na hawataki Auditors/Accountants, wanakuita kwenda kwenye majadiliano- kabla ya majadiliano watakutumia taarifa refu yenye mahesabu kichaa, wanakupa siku 30 uzisome- bila shaka utakuwa umepata fursa ya kujadiliana na watalaam wako. Kisha utawajibu kwa maandishi na wao watakuita kwenye kikao KAMA MMILIKI! Hapo utachezewa kimahesabu na vijana wadogo, mwisho watakupa barua nyingine ' Notice of Discussion' ambayo itabidi usaini wewe na watu wao watatu! Kwa Mbowe - walimwandikia yeye binafsi akiwa jela na mambo mengi hayakuwezekana! Wizi tu! Sasa John hawezi kuona hili???? Ondoa hizo pamba masikioni John!