Inabidi mtu awe mpumbavu kushawishika na kusema kuwa hakuna Mungu!

mpolekabisa

Senior Member
Joined
Oct 18, 2023
Posts
161
Reaction score
225
Biblia inasema kwenye Zaburi 24:1. "Mpumbavu amesema moyoni mwake hakuna Mungu .........".

Kuna watu wanaamini kabisa kuwa hakuna Mungu!! Wanashawishika kwa mioyo yao yote kuwa hakuna Mungu!! Ukimwuliza kwa nini vitu vilivyopo ulimwenguni huitwa VIUMBE? Maana yake vimeumbwa, je muumbaji ni nani? atakuambia vimetokea tu, kwa mabadiliko (evolution). Lakini hicho kilichopitia mabadiliko kilitokeaje? hapo hana jibu!

Ni sawa na mtu akawa na kitabu cha hadithi fulani halafu mtu akadai kilitokea tu wala hakuna mtunzi!!

Ni mpumbavu tu mtu anayeweza kuamini hivyo!!
 
Unaelewa kwamba, ukitoa hoja kwamba vilivyo complex haviwezi kuwepo tu, ni lazima viwe vimeumbwa, hapo umetoa hoja kwamba Mungu muumba vyote hawezi kuwepo?

Unaelewa mantiki hii au unahitaji kufafanuliwa zaidi uelewe?
 
Unaelewa kwamba, ukitoa hoja kwamba vilivyo complex haviwezi kuwepo tu, ni lazima viwe vimeumbwa, hapo umetoa hoja kwamba Mungu muumba vyote hawezi kuwepo?

Unaelewa mantiki hii au unahitaji kufafanuliwa zaidi uelewe?
LIKUD
 
Kwanza kabisa hakuna imani ya kwamba hakuna Mungu!!

Uchi siyo style ya uvaaji.

Ujinga wa mwanadamu ndiyo ulipelekea kumuumba Mungu tena kwa mfano wa mwanadamu.

Neno viumbe halina kigezo cha kukufanya uhoji kwamba "ni nani kaviumba"

Umeshajiuliza kwamba kama tukibadili lugha, maybe in English,
Neno hilo "Viumbe" (living things) lingeweza kutengeneza ngeli ya kuuliza kama ulivyouliza kwenye kiswahili?

Unatukana watu kwa vitu usivyovielewa tu.

This is your assignment

1. Mungu aliumbwa na nani?

2. Unaweza halalisha madai yako ya kwamba viumbe hai hivyo vimeumbwq na huyo Mungu kwa kumthibitisha uwepo wake?
 
Biblia ni nini? Kaandika nani?
Kwa nini wasiwe wapumbavu wanaeaminishwa kuwa Mungu yupo? Huku wakiulizwa Mungu ni nini na yuko wapi hawajui!? Wenzao badala ya kujibu wanasema dhibitisha kutokuwepo kwake?!
 
Biblia ni nini? Kaandika nani?
Kwa nini asiwe mpumbavu anaeaminishwa kuwa Mungu yupo? Huku akiulizwa Mungu ni nini na yuko wapi hajui!?
Thibitisha kwamba Mungu hayupo. Acha porojo wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…