Mungu hayupo. OvaWao wenyewe walitoka wapi? Usifanye hili swali rahisi lionekane gumu.
Uhai ni nini na nini chanzo chake?
Hiyo ni mitazamo potofu kuhusu Mungu, na wala Mungu haishi kwa vigezo vyako wewe.
Mbona kila mkiulizwa alipo hamtaki kutuelekeza mnabaki tu kupiga chenga? Tutafataje mtu/kitu na matakwa yake bila kujua alipo na kujihakikishia uwepo wake? Mna nini lakini? Kisa tu tuunge tela? Hatudanganyikiii
Dunia hii imepitia uongo/utapeli/propaganda kubwa sana na zikapita lakini uongo pekee uliodumu kwa muda mrefu ni huu:
Hebu fikiria unaambiwa kuna MUNGU muweza wa yote yupo sahihi na hajawahi kukosea
Ameumba dunia kwa ajili yetu na ana mpango wa kuiangamiza kwa moto.
Alijua ataiangamiza dunia kabla hata hajaiumba lakini aliiumba hivyo hivyo ili aje kuiangamiza(kama vile hajielewi),
Ameumba moto wa jehanamu kwakuwa ametuumba tukosee ili atuchome moto japo alikua na uwezo wakutuumba tusiwe wakosefu ili atuumbie pepo tu tukale bata
Anajua tunacho hitaji lakini lazima tumuombe ili atupe, lakini hata tukimuomba hatupi tunavyotaka sisi maana tayari amekwisha tupangia kila mtu atampa nini, ataishije na atakufaje
Ndio muumba wa kila kitu(magonjwa, bangi, majini,umalaya,ukahaba, ulabu nk) na anaweza kudhibiti chochote lakini anamlaumu msaidizi wake muasi(Shetani) kuleta mambo hayo mabaya duniani (magonjwa nk) kwa watu wake aliyewaumba wakati yeye ndiye aliye mtupa msaidizi wake huyo huku duniani( inaelekea huyu hajiwezi mpaka awe na msaidizi mhuni,amuache tu amchanganyie habari)
Yaani yeye kashindwana naye huko mbinguni kaja kumtupa kwetu sisi viumbe dhaifu tupambane naye(lipo wazi huyo shetani anamzidi nguvu na uelewa) na tukishindwa tutachomwa moto milele, lakini anasisitiza anatupenda sana kama mtu anavyopenda na kujali mboni ya jicho lake
Hebu tafakari hili, kawaumba Adam na Hawa na wakati bado wageni duniani akawatupia Nyoka(Shetani) ili awarubuni(kama nyoka tunayemjua ndo alikuwa anaishi na huyo Mungu na kusaidizana nae, vuta hiyo picha), na kwa ugeni wao wakarubunika matokeo yake katupa adhabu ya shuruba watu wote hata ambao tulikua hatupo na hata ambao hawajazaliwa chamoto watakiona...... Not fair
Mungu muweza wa yote hayupo WAZI PASI NA SHAKA kwa watu wote kujua huyu ndio MUNGU badala yake Mungu ndio amekua sehemu kubwa ya mgawanyiko wa watu na kusababisha kuwa na imani za MIUNGU zaidi ya milioni dunia nzima
Na kibaya zaidi unatakiwa tu kumuamini, usihoji wala kuwa na shaka juu ya uwepo wake(ni laana na kufuru) vinginevyo moto wa milele unakuhusu
Yaani kuna mtoto wa fundi Kapenta mmoja huko Galilaya eti kafa kwaajili ya dhambi za watu wote duniani.... Seriously ?
Akaitwa neno. Neno huyo alikua Mungu, mtoto wa Mungu lakini Mungu huyu akajaribiwa na shetani na akapatikana. Shetani aliemuumba mwenyewe ndo akawa amemmaliza.
Mtoto huyu wa fundi kampenta, hakuandika kitabu chochote ila wahuni walio kuwa wanampinga ndio wakaja kuandika vitabu kuhusu dogo huyu na vinaitwa “Bibilia Neno la Mungu takatifu”
Mabilioni ya watu dunia kote wanakesha makanisani wakimlilia na kumuomba awape uponyaji, mali, waume/wake nk
Hebu fikiria huko Arabia kuna maamuma mmoja hajui kusoma wala kuandika alidai anashushiwa maagizo na Mungu kukata vichwa watu wote watakaopinga na kutokutii maagizo yake, “akashushiwa” aya za vitisho na neema kwa watakao tii, yaani ukifa unampigania Mungu unakwenda kupewa mabikra 72 kazi yako ni kuzagamua tu.
Mabilioni ya watu duniani wanasujudu mara 5 kwa siku na kushinda njaa mwezi kila mwaka ili wakale naye bata Peponi
Kwamba maisha yako hapa duniani ni ya mpito tu maisha yako yapo baada ya kufa. Hatujawahi sikia aliyekufa akirudi kuhadithia hayo maisha ya badae
Unachotakiwa kufanya ni kumuamini na kufanya aliyoagiza ili ukale bata sana baada ya kufa