Tetesi: Inadaiwa uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane unaendelea

Tetesi: Inadaiwa uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane unaendelea

Ikapatikana miili ya watu mto Ruvu maeneo ya bagamoyo
Na Waziri wa mambo ya ndani unataka atolee maelezo yaliyoandikwa na waandishi wa Gazeti la Mwananchi la Ijumaa ya tarehe 06/01/2023 katika ukurasa wa pili(2)?

Habari hiyo upo sehemu ya juu ya ukurasa huo. Na waandishi hawa kwa mujibu wa ukurasa huo wanapatikana kwa barua pepe ya mwananchipapers@mwananchi.co.tz
 
Nchi imeharibiwa na CCM kwa miaka mingi Magufuli akiwemo.

Yeye baada ya kuwa Rais akaendeleza na kuzidisha uharibifu kwa kufanya maovu mengi kama yalivyoelezwa na waliotangulia.
Sasa kwa nini tusishughulike na mzizi wa tatizo? Kama ccm imekuwa ikiharibu nchi kabla ya Magufuli hajawa rais na ccm hiyo hiyo ndio ikatuletea Magufuli kwanini tusipambane na Ccm badala ya kuangaika na Magufuli? Leo hii tunaona baadhi ya matatizo ya awamu ya nne yanarudia tena katika awamu hii na ni mambo ambayo yalipigiwa kelele wakati huo, ndio maana tudeal na ccm ikiwa kweli hatutaki mambo ya ajabu ajabu kujirudia.
 
Kuna post ukizisoma zinakuharibia siku. Mpumbaf tuu ndio anaweza kusema hivi kuhusu Mbowe.
Yaani Mbowe amchukie hadi kumpoteza msaidizi wake aliyekuwa anambana na kumnyima raha Magufuli mitandaoni? Kwa maana hiyo Mbowe na Magufuli ni maswahiba?
Acheni utoto!
Mkuu wewe ni Mkongwe humu halafu bado unahangaika na watu sampuli hiyo?

Mara mia umu ignore au piga dislike.
 
Kwenye mambo ya msingi ukiona mtu mzima kama huyo ana leta comedy tena mahali maisha ya mtu yamepotezwa ujue kuna walakini katika makuzi yake na mfumo wake wa maisha. Msamehe na kumpuuza
Mkuu hata walioshiriki kumteka wanaweza wakawa ndo hao hao unaowasoma humu.
 
Dam inanuka utawala wa Tano tu? Nadhani hamjuwi na mnataka kujuwa ila kwa kuwasaidia anzeni kuondoa haki ya viongozi wakuu kutoshitakiwa ili Taifa linuke harufu mbaya ya dam na dhuluma tangu kuanza kwa misingi ya Taifa hili. Kama kuna Rais hajamwaga dam basi awe wakwanza msemea vibaya Magufuli. Kama Kuna kiongozi team yake haijatoa watu roho awe wakwanza kunyoosha mkono kwa Magufuli... Kama Taifa hili halijanuka uvundo wa ajabu.
Kiufupi yeyote anaye hangaika na Magufuli basi haujuwi mfumo na kama anajuwa amefunga macho kutaka iondoa amani yetu.
Hayati Mandela akakumbuka maovu ya kutafuta uhuru wa SA akasema tupatane mapatano ambayo yalimfanya kumuacha mke wake kipenzi. Why dam dam dam. Jamani tuachane na haya Magufuli hayupo kama alitenda kwa haki au kwa dhuluma Mungu ndie muamuzi wa yote. Ila tujifunze pale tumekosea yasijirudie. Wakati haya Magufuli hajaoza wapo watu wanafanya Yale Yale kwa kificho cha Uzalendo. God have a meryon Us God have a Mercy on president of this republic it is not easy job.
Nakumbuka wewe ulikuwa kinara wa kumpiga biti Ben Saanane humu JF kuwa atapotezwa. Vipi unaweza kutupa clue ni kitu gani kilimkuta Ben?, Alipigwa risasi?, nyundo kichwani au alifungwa katika kiroba akatupwa baharini?
 
kuna kijana alikamatwa Muhimbili na genge la yule muuaji Magu ( alijitengenezea kundi la wauaji nje ya mfumo) bahati baada ya mateso makubwa huko kwenye safe house zao nadhani mikoa ya Mtwara wakaona walikosea hakuwa yeye waliye mkusudia wakaja kumtupa usiku maeneo ya Mbagala..Yule dogo akikusimulia ukatili waliokuwa wakifanyiwa huwezi kabisa kumsifia yule Mzee.
Alituambia alimuoana jamaa flani ambae kwao alipotea alimkuta kule kachakaa kwa kichapo na kweli baada ya kama wiki mbili mwili wa jamaa ukaokotwa COCO BEACH kwenye gunia.
Yule kijana mpaka leo yupo maeneo ya Muhimbili anawafanyia wagonjwa maombi na Dua.
Kile kifo ilikuwa ni nguvu ya maombi na vilio vya wahanga ndio maana alikufa kwa shida hadi kujinyea
Kuna kijana alikuwa anamsema jiwe kule Kimara akiwa kwenye baa maeneo ya karibu na jiwe alipokuwa anahutubia kwenye mkutano. Na kwa kawaida, maeneo jirani na mikutano hao jamaa wanakuwepo kwenye bars, groceries, mahotelini nk.

Ghafla hao jamaa wakatokea na kumzingira, na kumpiga, by the time anaondolewa kupelekwa kwenye Noa, uso ulikuwa umeumuka, kisha wakaondoka naye.

Dogo hakuonekana kwa muda mrefu hata familia ikaingiwa na wasiwasi. Baada ya muda, walimchukuwa wakaenda kumtelekeza maeneo karibu na nyumbani kwao. Dogo alikuwa ametokea huko Kibosho.

Walimfanya kitu mbaya maana hakumbuki chochote, bali anakumbuka tu kulishwa ugali. Akili zake hazimo sawa na pia walimuhasi.

This is a true story!
 
Kuna mnyetishaji anadai kwamba Jiwe aliamuru kijana Ben Sa8 akamatwe apelekwe jumba jeupe. Ile kufika tu huyu nduli jiwe alichomoa bastola na kumtoa roho Ben Sa8. Jiwe alimuua Ben kwa mkono wake mwenyewe.

Kama huo uchunguzi utatenda haki basi haya tutayasikia.

Tukisema jiwe alikuwa nduli muuaji muwe mnaelewa.
Ushahidi wa hili unalosema
 
Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo ambayo yalitokea enzi za utawala wa awamu ya tano na hakuna aliyethubutu kuanzisha uchunguzi juu ya hilo kutokana na maelekezo maalum.

Sasa nawataarifu kuwa uchunguzi juu ya kupotea kwa kijana huyo unaendelea na ni moja ya ajenda muhimu zilizojadiliwa hapo kabla. Hivi karibuni jambo hilo litawekwa wazi.

Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo yanayofanya viongozi wastaafu wa ngazi za juu kukwepa kabisa kuuzungumzia na kuujadili utawala wa hayati John Magufuli. Imefahamika kuwa yapo mambo kadhaa yasiyo ya utu yalifanyika huku yakiwa na baraka za hayati John Magufuli tena kwa maelekezo maalum.

Wekeni masikio wazi siku chache zijazo mtasikia la mgambo.
Duuh bora wawe walimfunga tu sehemu lakini awe hai Mungu saidia
 
Mshauri mkuu wa rais ni makamu wake. Hata leo Mpango hawezi kukwepa anayoyafanya Samia kwa kuteua watu wa dinni moja. Rejea mawaziri watano toka mkoa mmoja wa Tanga huku mawaziri wawili toka mikoa ya Mwanza Mara Simiyu Shinyanga na Kagera.

Vivyo hivyo aliyekuwa makamu kipindi cha JPM ashughulikiwe.

Sijui alikuwa nani na ni nani sasa hivi
Mbona kwenye kujenga Ikulu dodoma mnasema ni Jpm tu?
 
Aliyeua kwa upanga naye leo hayupo. Asante Mungu (au wanadamu wenye walioingia kati) kwa kutuondolea mbali lile dubwasha lililoitwa JPM.

Kwangu 17 March,2021 ilikuwa siku ya furaha sana na itabaki hivyo milele.
Halima hiyo 17 March ya mwaka wowote utaondokewa na mtu wako wa karibu tuone kama itaendelea kuwa siku ya furaha kwako
 
Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo ambayo yalitokea enzi za utawala wa awamu ya tano na hakuna aliyethubutu kuanzisha uchunguzi juu ya hilo kutokana na maelekezo maalum.

Sasa nawataarifu kuwa uchunguzi juu ya kupotea kwa kijana huyo unaendelea na ni moja ya ajenda muhimu zilizojadiliwa hapo kabla. Hivi karibuni jambo hilo litawekwa wazi.

Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo yanayofanya viongozi wastaafu wa ngazi za juu kukwepa kabisa kuuzungumzia na kuujadili utawala wa hayati John Magufuli. Imefahamika kuwa yapo mambo kadhaa yasiyo ya utu yalifanyika huku yakiwa na baraka za hayati John Magufuli tena kwa maelekezo maalum.

Wekeni masikio wazi siku chache zijazo mtasikia la mgambo.
Hii taarifa imemuibua Sirro kwenda kuhojiwa ITV Dk 45.

Unganisheni nukta kujitokeza kwa Balozi Sirro kujibu hoja za waliopotea alipokuwa IGP
 
Back
Top Bottom