Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
(Democracy is written on paper?) Maneno ya kulaghai wajinga na wasio na uelewa. Nini maana ya utawala wa sheria na due process? Unataka kuaminisha watu kuwa Julian Assange angerejeshwa Marekani angefikishwa White House au kwenye dola kwa siri na kuuawa in cold blood?Marehemu naye alikuwa na ujasiri,wewe unamuona kabisa huyu mtawala siyo wa mchezomchezo unaenda kumpekua,sasa alitarajia kinachofuata ni nini?
Hakuna serikali isiyo ua Duniani,ukipambana na serikali ni mawili aidha uwe kilema au ufe,simple.
Ata Asange alivyoleta uhuni wake kwa serikali ya Marekani,kilichofuata wote tunajua!
"Democracy is written on papers but not in actions"
Unafahamu kesi za watu kama Aldrich Ames, Jonathan Pollard, Chelsea Manning, na wasaliti wengine kibao wa US? Michakato iliyotumika hadi kuwatia hatiani na kuadhibiwa? Au unajumlisha na mambo ya nchi za kikomunisti na ya hizi banana republics zetu?
Halafu tofautisha kupambana na serikali na kupambana na mtu binafsi. Marekani ukimtukana Joe Biden utapambana naye mahakamani na wanasheria wake binafsi. Lakini ukimtuhumu Rais wa Marekani kwa kosa lolote km kuagiza mauaji ya kiongozi wa dini fulani, hapo utakutana na taasisi husika za serikali - mahakamani (sio mafichoni).