Tetesi: Inadaiwa uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane unaendelea

Tetesi: Inadaiwa uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane unaendelea

Marehemu naye alikuwa na ujasiri,wewe unamuona kabisa huyu mtawala siyo wa mchezomchezo unaenda kumpekua,sasa alitarajia kinachofuata ni nini?

Hakuna serikali isiyo ua Duniani,ukipambana na serikali ni mawili aidha uwe kilema au ufe,simple.

Ata Asange alivyoleta uhuni wake kwa serikali ya Marekani,kilichofuata wote tunajua!

"Democracy is written on papers but not in actions"
(Democracy is written on paper?) Maneno ya kulaghai wajinga na wasio na uelewa. Nini maana ya utawala wa sheria na due process? Unataka kuaminisha watu kuwa Julian Assange angerejeshwa Marekani angefikishwa White House au kwenye dola kwa siri na kuuawa in cold blood?

Unafahamu kesi za watu kama Aldrich Ames, Jonathan Pollard, Chelsea Manning, na wasaliti wengine kibao wa US? Michakato iliyotumika hadi kuwatia hatiani na kuadhibiwa? Au unajumlisha na mambo ya nchi za kikomunisti na ya hizi banana republics zetu?

Halafu tofautisha kupambana na serikali na kupambana na mtu binafsi. Marekani ukimtukana Joe Biden utapambana naye mahakamani na wanasheria wake binafsi. Lakini ukimtuhumu Rais wa Marekani kwa kosa lolote km kuagiza mauaji ya kiongozi wa dini fulani, hapo utakutana na taasisi husika za serikali - mahakamani (sio mafichoni).
 
Hakika 100%! Kwanza Ben lugha aliyokuwa akiitumia ilikuwa ya kidhalilishaji, na mbovu sana. Hakuwa na adabu kwa mtu mwenye rika la kumzaa, kama haitoshi Rais wa nchi.

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
Ndio auwawe? Mbona yeye Magufuli rais mzima hakujiheshimu wala kuheshimu taasisi ya urais hadi anaiba rambirambi nakujidhalilisha?
 
Ndiyo rais anayetakiwa kwa kizazi hiki cha sasa awe dictator mzalendo [emoji380]
Anatakiwa na nani ? Kama anatakiwa kwa nini Mungu ameruhusu akafa kizembe vile?

Magufuli alikuwa anaharibu nchi yetu kwa kuleta ubaguzi wa kiitikadi, kikanda na kikabila. Hata kunyanga'anya matajiri fedha ilikuwa anaipeleka nchi pabaya sana
 
..... zilizokutwa kwenye viroba....
Ukiona hivyo, ujue sababu...
====

Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo yanayofanya viongozi wastaafu wa ngazi za juu kukwepa kabisa kuuzungumzia

Gazeti la Mtanzania liliwahi kuandika kama nukuu ilivyo kwenye blog hii


===
Tuwe makini tunapokuwa kwenye nyumba ya vioo. Tusiwaudhi waliokaribu kokoto!
 
Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo ambayo yalitokea enzi za utawala wa awamu ya tano na hakuna aliyethubutu kuanzisha uchunguzi juu ya hilo kutokana na maelekezo maalum.

Sasa nawataarifu kuwa uchunguzi juu ya kupotea kwa kijana huyo unaendelea na ni moja ya ajenda muhimu zilizojadiliwa hapo kabla. Hivi karibuni jambo hilo litawekwa wazi.

Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo yanayofanya viongozi wastaafu wa ngazi za juu kukwepa kabisa kuuzungumzia na kuujadili utawala wa hayati John Magufuli. Imefahamika kuwa yapo mambo kadhaa yasiyo ya utu yalifanyika huku yakiwa na baraka za hayati John Magufuli tena kwa maelekezo maalum.

Wekeni masikio wazi siku chache zijazo mtasikia la mgambo.
Dam inanuka utawala wa Tano tu? Nadhani hamjuwi na mnataka kujuwa ila kwa kuwasaidia anzeni kuondoa haki ya viongozi wakuu kutoshitakiwa ili Taifa linuke harufu mbaya ya dam na dhuluma tangu kuanza kwa misingi ya Taifa hili. Kama kuna Rais hajamwaga dam basi awe wakwanza msemea vibaya Magufuli. Kama Kuna kiongozi team yake haijatoa watu roho awe wakwanza kunyoosha mkono kwa Magufuli... Kama Taifa hili halijanuka uvundo wa ajabu.
Kiufupi yeyote anaye hangaika na Magufuli basi haujuwi mfumo na kama anajuwa amefunga macho kutaka iondoa amani yetu.
Hayati Mandela akakumbuka maovu ya kutafuta uhuru wa SA akasema tupatane mapatano ambayo yalimfanya kumuacha mke wake kipenzi. Why dam dam dam. Jamani tuachane na haya Magufuli hayupo kama alitenda kwa haki au kwa dhuluma Mungu ndie muamuzi wa yote. Ila tujifunze pale tumekosea yasijirudie. Wakati haya Magufuli hajaoza wapo watu wanafanya Yale Yale kwa kificho cha Uzalendo. God have a meryon Us God have a Mercy on president of this republic it is not easy job.
 
Anatakiwa na nani ? Kama anatakiwa kwa nini Mungu ameruhusu akafa kizembe vile?

Magufuli alikuwa anaharibu nchi yetu kwa kuleta ubaguzi wa kiitikadi, kikanda na kikabila. Hata kunyanga'anya matajiri fedha ilikuwa anaipeleka nchi pabaya sana
Kwa nchi gani ya kuharibiwa? Mbona tunataka kuaminishana kuwa matatizo ya nchi hii ni Magufuli tu?
 
Mama hawezi achia hii ripot.atachofanya ataiomba msamaha familia kimya kimya .Na kuilipa fidia .report itatumika kama ushahidi wa kutoa hela ya serikali tu.lakini kwa ukubwa wa cheo cha rais anajua 100% juu ya mbwa ya chato kumuua huyu kijana kwa kuhoji phd yake
Okey alihoji phd ya babu tale na msukuma
 
Ulisikiliza uchunguzi wa Zitto Kabwe kuhusu Ben Saanane?



Hapa akizungumzia Kupotea kwa Simon Kanguye.


Zitto alikuwa na ujasiri sana, ukiangalia hapo unaona sura za mawaziri na wabunge zilivyo wasiwasi na uoga kwa yale anayoongea Zitto.
 
Kwa nchi gani ya kuharibiwa? Mbona tunataka kuaminishana kuwa matatizo ya nchi hii ni Magufuli tu?
Nchi imeharibiwa na CCM kwa miaka mingi Magufuli akiwemo.

Yeye baada ya kuwa Rais akaendeleza na kuzidisha uharibifu kwa kufanya maovu mengi kama yalivyoelezwa na waliotangulia.
 
Back
Top Bottom