Tetesi: Inadaiwa uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane unaendelea

Tetesi: Inadaiwa uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane unaendelea

Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo ambayo yalitokea enzi za utawala wa awamu ya tano na hakuna aliyethubutu kuanzisha uchunguzi juu ya hilo kutokana na maelekezo maalum.

Sasa nawataarifu kuwa uchunguzi juu ya kupotea kwa kijana huyo unaendelea na ni moja ya ajenda muhimu zilizojadiliwa hapo kabla. Hivi karibuni jambo hilo litawekwa wazi.

Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo yanayofanya viongozi wastaafu wa ngazi za juu kukwepa kabisa kuuzungumzia na kuujadili utawala wa hayati John Magufuli. Imefahamika kuwa yapo mambo kadhaa yasiyo ya utu yalifanyika huku yakiwa na baraka za hayati John Magufuli tena kwa maelekezo maalum.

Wekeni masikio wazi siku chache zijazo mtasikia la mgambo.
Hii yaweza kuwa uchunguzi wa kupakana matope. Ila mmoja au baadhi ya watuhumiwa wanapogeuka kuwa marehemu, kesi inakosa nguvu, kwani upande wa pili hautasikika!
 
Ulisikiliza uchunguzi wa Zitto Kabwe kuhusu Ben Saanane?

Hapa akizungumzia Kupotea kwa Simon Kanguye.

Ukweli ni kwamba Jiwe ameacha machungu mengi kwa familia nyingi.
Nlishawahi kusema sehemu kwamba, Wafuasi wa Magufuli mlipata raisi ambae ni muwakilishi wa roho zenu za kikatili zilivyo, Kupitia yule mzee nmefahamu tunaishi na watu wengi wenye roho za kikatili sana, wasiojali utu hata kidogo.
Mtu akihoji auwawe, akipinga auwawe, Akitoa malalamiko auwawe,

Kwenu mauaji, umwagaji damu ni sawa.
Inasikitisha sana,Magu alikuwa katili aisee na wafuasi wake ni hatari zaidi.
 
Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo ambayo yalitokea enzi za utawala wa awamu ya tano na hakuna aliyethubutu kuanzisha uchunguzi juu ya hilo kutokana na maelekezo maalum.

Sasa nawataarifu kuwa uchunguzi juu ya kupotea kwa kijana huyo unaendelea na ni moja ya ajenda muhimu zilizojadiliwa hapo kabla. Hivi karibuni jambo hilo litawekwa wazi.

Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo yanayofanya viongozi wastaafu wa ngazi za juu kukwepa kabisa kuuzungumzia na kuujadili utawala wa hayati John Magufuli. Imefahamika kuwa yapo mambo kadhaa yasiyo ya utu yalifanyika huku yakiwa na baraka za hayati John Magufuli tena kwa maelekezo maalum.

Wekeni masikio wazi siku chache zijazo mtasikia la mgambo.
Uchunguzi uendelee na wanaohusika wapate adhabu kali haijalishi bado wapo hai au wamekufa, wapewe adhabu kali!
 
Sasa kama mwenyewe unasema ben saanane alipotea kwa baraka za jpm unataka uchunguzi wa nini?
Binafsi nasema ben saanane lolote lililomtokea alijitakia mwenyewe.
Kwanza alijipa kazi au kupewa kazi cdm ya kumtukana magufuli, kumchafua kwa kutumia maneno yasiyofaa. Awamu ya 5 wangetaka kumshitaki wangeweza maana alikua anavunja sheria kumkejeji na kumdhalilisha rais wa jamhuri. Alijikita kueleza kadamnasi kwamba jpm aligushi cheti chake cha Phd huku bila kuonyesha ushahidi wowote. Licha ya kuonywa kuhusu uongo wake dhidi ya binafsi ya rais alikaza shingo kujitia ushujaa.
Huenda dola wanajua nani kampoteza ben ila wananyamaza kumlinda mtu huko upinzani maana akitajwa nyie mnaotaka uchunguzi hamtoamini.
Kwa nini hawakumshtaki mahakamani ambapo angetakiwa kutoa ushahidi na hukumu stahiki kutolewa? Wewe unaona uamuzi binafsi wa Rais kuua mtu in cold blood ndio hatua sahihi?
 
Alikosa adabu kabisa. Huwezi kumdhalilisha mtu mwenye uwezo wa kukuzaa, tena Rais wa nchi kiasi kile. Lugha ilikuwa mbovu mno na ya dharau na kejeli. Hakutakiwa kuvumiliwa. Lazima adabu iwepo, Ben hakuwa na rika sawa na Magufuli mpaka amtusi kiasi kile.
Acha upumbavu nyinyi wafuasi wa jiwe mnapo shinda humu mnamtukana na kuwadhihaki mama na Kikwete mara mafisadi na wauza unga mbona hajawatafuta na kuwauwa au nyinyi mna kibali maalumu cha kuwadharirisha wengine kutoka kwa mungu?

Au unadhani anashindwa kutumia mamlaka yake kulifyeka hilo kundi lenu la sukuma gang linalo shinda mitandaoni likimtukana na kumdhihaki?
 
Nimesema kama Mbowe angehusika na kifo cha Ben(Kama yuvisisiemu wanayosema) basi angekuwa ashakamatwa ,hauwezi kufanya jambo kubwa la mauaji bila kuacha trace.

Bashite aliwasiliana na Ben na wakawa na mpango wa kukutana baada ya siku mbili kabla ya meeting akapotea.

Kuna namba ya voda ilimwambia Bensaanane kwamba aache kumtusi JIWE ikamsisitiza kwamba hes too young to die ,ikamwambia akiendelea ipo siku atajikuta mbele ya Chatu peke yake...ile namba haijawahi kuchunguzwa hata mara moja.
Loh![emoji29]
 
Back
Top Bottom