Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa

Ni hatari sana. Watu wanaponywa Ukimwi na Kansa pale.

Ukimwi gani?. Kansa unaijua?. Mwamposa hana uponyaji wowote zaidi ya maluelue. Sijui nilimwaga maji yakatoka majoka mengi ,au vyura wengi etc. Tuache kudanganya watu.

Yesu Kristo rekodi yake haiwezi kuguswa hata robo ya robo. Mwambie Mwamposa afunge siku arobaini bila kula au akafufue wafu waliokufa siku tatu. Acheni propaganda ule usanini ndio mnaita uponyaji?.
 

Punguza stori, Hakuna wakumfikia Yesu Kristo kwenye uponyaji. Huyo Paulo unayemsema alipata hiyo nguvu baada ya kukutana na Yesu Kristo kwa njia ya mwanga akiwa njiani akapigwa upofu na ndio huduma ya Paulo, Sasa ukamlinganishaje na Yesu Kristo?.

Hao mitume walishindwa kutoa pepo mpaka Yesu Kristo akalalamika, ikabidi awasaidiea. Rekodi ya Yesu Kristo haitafikiwa, Hawa wajanja wakutumia maji na keki ndio unawalinganisha na Yesu Kristo?.

Halafu nikusahishe, Yesu Kristo aliposema watafanya makubwa kuliko Mimi alikuwa anajishusha, na kutojikweza Kama hao kina Mwamposa.
 
Sasa huyu msenge kwanini anauza maji wakati Imeandikwa ni bure ana utani na maandiko ?
 
Kweli jamaa ni Bulldozer.
Mungu anamtumia kwa kiwango cha hali ya juu.
Jamaaa anachokifsnya ni kuhakikisha watu waone matatizo yao ni marahisi sana mbele za Mungu.

Hakuna Mungu pale. Mungu hawezi kutumia maji na keki kuponya. Ni jina moja tu la Yesu Kristo ndilo tulilopewa kulitumia kwenye uponyaji na usio maji na mafuta etc. Ndio maana leo mmeanza kujiongelesha kuwa Mwamposa anazidi Yesu Kristo maana hatumii jina lake bali vitu vya kimazingara.
 

Wale nguvu zao zina limitations kwenye eneo analofanyia huduma. Nje ya hapo hana chochote.
 
Mungu hawezi kuwauzia watu maji na keki ili wapate uponyaji, Imeandikwa umepewa bure toa bure sasa ni MUNGU gani anaeuzia watu maji ili wapone yule ni mfanyabiashara sio mchungaji Wala mganga wa kienyeji anaetumia jina la Yesu bila uoga
 
Dada mmoja nafanya naye kazi. Hazai. Kaunda hospital kubwa South Africa mara 2. Na hospital zote kubwa hapa bongo . Mwisho kaenda kwa mwamposa kaishia kufanyiwa mazingaombwe ya kutolewa chura ukeni basi hamna cha kuzaa wala upuuzi gani.

Aiseeh! Happ atahangaika Sana na maroho ya Mwamposa mpaka achoke.
 
Upo sahihi Ila kwanini anatumia jina la Yesu kwenye biashara yake au kwa sababu ni jina ambalo halina hatimiliki ?

Analitumia Kama cover, lakini yeye haliamini ndio maana anatumia maji, mafuta na keki ya upako. Siku akiacha kutumia hivyo vitu ndipo nitamuondoa kwenye kundi la Cult.
 
Mungu hawezi kuwauzia watu maji na keki ili wapate uponyaji, Imeandikwa umepewa bure toa bure sasa ni MUNGU gani anaeuzia watu maji ili wapone yule ni mfanyabiashara sio mchungaji Wala mganga wa kienyeji anaetumia jina la Yesu bila uoga

Amina
 
Aende akaponye watu hospitali, walipo wagonjwa wa kweli na sio waigizaji
 
Ile madhabahu ina nguvu(siwezi jua kama ni ya kimungu au ya kivingine) ila tuu kiukweli inatenda.
Lakini si kwa kila mtu,inaangalia imani yako na zaidi nyota yako.
Sababu ni kwamba wewe ufanikiwe kisha ulete chochote pale madhabahuni.
Hakuna cha bure kama kwa Yesu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…