Inafikirisha sana kuona viatu vinakupwaya lakini unajipa matumaini ya kuendelea na safari ya uongozi kwa Watanzania

Na hii ndo hoja yangu kubwa Mkuu! Kwani CCM wanaasisi utamaduni wanachama kupenda kutawala kwa Dezo? Kama anajinadi kuwa yeye Ni mwanamke aliyekuwa tu amenyimwa Fursa na wanaume lakini yeye anao uwezo kuwazidi hao wanaume Ni kwani asishindane na wenzie katika Chama? Anaogopa nini? Mtu mwenye uwezo naye huogopa? Kwa nini wanafiki wanamficha kwenye Koti la kusema awamu ya pili Ni utamaduni wa CCM kuachiwa agombee pekee? Kwani kama hii kweli Ni awamu Yake ya kwanza amegombea na nani?
 
H
Hatari Yake inaweza kuwa Ni kwamba kila Makamu wa Raisi atatamani au kufanya mipango Raisi afe ili yeye atawale moja kwa moja kwa vipindi viwili kimteremko bila kushindanishwa na wengine katika Chama.
 
🤣🤣

Endelea kuufukuza upepo

Katiba ,mila na ada ya CCM si kila mwanachama anaweza kuomba urais haswa pale ambapo aliyepo madarakani ana muhula mmoja.....

Ndio taratibu hizo muraaa......
Kwa hiyo, huyu mnakubali atakuwa wa kwanza kuupata kidezodezo?
 
Na ndio maana nimeuliza pia, vipi kama Magufuli angefariki miezi michache kabla ya kumaliza term yake ya pili, huyu makamu wake ambaye amerithi urais angeachwa kugombea bila kushindanishwa!?
 
Kama ana ubavu Mkuu ajipime na wenzie. Achana na wanaume ajipime tu na wanawake wenzie humo chamani aone kama atatoboa. Mambo ya kujishaua haya na kulingishia watu sifa zisizokuwepo.
 
H
Na ndio maana nimeuliza pia, vipi kama Magufuli angefariki miezi michache kabla ya kumaliza term yake ya pili, huyu makamu wake ambaye amerithi urais angeachwa kugombea bila kushindanishwa!?
Hili Swali watoke CCM Walijibu. Chama kinaelekea kuwa cha hovyo kwa kujenga hoja za hovyo hovyo.
 
Tukubali baada ya "Mwendazake" sasa anayemrithi anakiri hadharani kuwa uwezo wake msiuwekee matumaini sana kama ambavyo tulifanya kwa "Mwendazake"?

Si kila viatu vinavyokutosha unatakiwa uvivae.

Si kila viatu visivyokutosha vinakufaa.

Si kila viatu vinavyokutosha vitakupendeza.

Huwezi kuta mwanaume analalamika viatu vya mkewe vingemtosha angeenda navyo kazini.

Kiongozi wa sasa viatu alivyovaa vina miezi sita.

Asiwaze mabuti ya asiyekuwepo hatakama alivyonavyo havifai kupigia mitama.
 
Nikiunganisha na hiyo Avatar naona maoni yako yana msukumo wa udini
Dini yako inasemaje? Inakueleza ?kuwa Kjongozi anajiteua tu na kujipachika? Mtume Muhammad alijiteua au alipewa utume na Malaika Jibrili kama inavyoadithia Kurani?
 
Alitakiwa ayajue haya. Kile kitendo cha kulilia Viatu vya wengine vimjae ndio kuonyesha uwezo Mdogo na hapa ndio Makala imelala
 

Kila zama na mambo yake. Mama yetu chapa kazi achana na hao kama huyu
 
Chuki ya nini na dhidi ya nini na nani? Mtu amesema Viatu vya mtangulizi wake vinampwaya sasa sisi kuhoji kama vinampwaya anatafuta nini tena kwa kuhitaji kuvivaa Viatu hivyo hivyo na hiyo ndo imekuwa Chuki?

Huo ni msemo tu. Rais Mstaafu Mwinyi Aliwahi kusema yeye ni kichuguu na Nyerere ni mlima. Panua uelewa wako.
 
Hivi unamkumbuka mh.Membe?!!

Kipi kilimkuta baada ya KUTAKA KUGOMBEA URAIS NDANI YA CCM?!!

Usijitoe ufahamu kama mtoto mdogo "mlizi".....

Kama watanzania tunastahili rais bora.

Rais bora si kwa mawazo ya mtu mmoja au hata kikundi chochote bali kupitia ushindani wa wazi na haki tutampata mtu huyo.

Kwa nini hamtaki tupate mtu bora kupitia ushindani huru na ulio wa haki?
 
Kama watanzania tunastahili rais bora.

Rais bora si kwa mawazo ya mtu mmoja au hata kikundi chochote bali kupitia ushindani wa wazi na haki tutampata mtu huyo.

Kwa nini hamtaki tupate mtu bora kupitia ushindani huru na ulio wa haki?
Wanaogopa ushindani na hapo hapo hawakomi kujiita Viongozi Bora! Unakuwaje bora kama hakuna wa kujipima Naye?
 
In short watu wa namna hii hawafai. Nia yao ni kuwaengua wengine kimzengwe mzengwe tu.
Halafu Ni tabia kama ya MbwaKoko kukoromea baadhi ya Mbwa tu huku wengine akiwagwaya. Wao wanajitia kimbelembele kuwakoromea wapinzani wanamuogopa Mgombea aliyejitangaza kabla ya muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…