Inafikirisha sana kuona viatu vinakupwaya lakini unajipa matumaini ya kuendelea na safari ya uongozi kwa Watanzania

Inafikirisha sana kuona viatu vinakupwaya lakini unajipa matumaini ya kuendelea na safari ya uongozi kwa Watanzania

Ccm wasikubali ujinga wa kusema huyo mwanamke aachwe aendelee muhula wa pili bila mchakato wa chama kushindanisha wagombea kufanyika. Hilo linapaswa kuwa kwa yule kiongozi aliyechaguliwa ila huyu aliyerithi madaraka lazima ieleweke anachofanya ni kukamilisha muhula wa yule aliyetangulia. Isije kuonekana kama huu ni mhula wake, je, vipi kama mtangulizi wake angefariki mwaka mmoja kabla ya uchaguzi hapo 2025, je, huyu angeachwa kuw mgombes bila kushindanishwa!?
Na hii ndo hoja yangu kubwa Mkuu! Kwani CCM wanaasisi utamaduni wanachama kupenda kutawala kwa Dezo? Kama anajinadi kuwa yeye Ni mwanamke aliyekuwa tu amenyimwa Fursa na wanaume lakini yeye anao uwezo kuwazidi hao wanaume Ni kwani asishindane na wenzie katika Chama? Anaogopa nini? Mtu mwenye uwezo naye huogopa? Kwa nini wanafiki wanamficha kwenye Koti la kusema awamu ya pili Ni utamaduni wa CCM kuachiwa agombee pekee? Kwani kama hii kweli Ni awamu Yake ya kwanza amegombea na nani?
 
H
swari la msingi,ni kwann aanze kujitangaza rasmi kuwa atagombea 2025,ikiwa hata robo ya muhula haijaisha!?,je ni kuweka mazingira ya kuwatisha wengine wasioneshe nia!,je ni kuomba huruma kwa wengine wasigombee/au kuonyesha nia ya kuingia kwenye kinyang'anyilo ndani ya chama !? Kuna majuzi hivi nimemskia naibu wazir fulani nae akisema hadharani kuwa,kwa kuwa mama ataendelea Hadi 2030!! Nashangaa haya Mambo yanatoka wapi kuanza kumnadi mtu na wakati/muda bado haujafika wa kujinadi!!sijajua katiba ya chama inasemaje na inalitazama vipi hili swala !! Kama hii picha haitawekwa sawa na chama ,wajitafakali Sana ,Leo yeye ,kesho namwingine nae atafanya vivyohivyo,mwisho wa siku litakuja kulipuka bonge la bomu .....chama wanatakiwa kuliweka sawa hili Jambo ndani ya kamati zao za maadili na miongozo !!
[emoji120]
Hatari Yake inaweza kuwa Ni kwamba kila Makamu wa Raisi atatamani au kufanya mipango Raisi afe ili yeye atawale moja kwa moja kwa vipindi viwili kimteremko bila kushindanishwa na wengine katika Chama.
 
🤣🤣

Endelea kuufukuza upepo

Katiba ,mila na ada ya CCM si kila mwanachama anaweza kuomba urais haswa pale ambapo aliyepo madarakani ana muhula mmoja.....

Ndio taratibu hizo muraaa......
Kwa hiyo, huyu mnakubali atakuwa wa kwanza kuupata kidezodezo?
 
Na hii ndo hoja yangu kubwa Mkuu! Kwani CCM wanaasisi utamaduni wanachama kupenda kutawala kwa Dezo? Kama anajinadi kuwa yeye Ni mwanamke aliyekuwa tu amenyimwa Fursa na wanaume lakini yeye anao uwezo kuwazidi hao wanaume Ni kwani asishindane na wenzie katika Chama? Anaogopa nini? Mtu mwenye uwezo naye huogopa? Kwa nini wanafiki wanamficha kwenye Koti la kusema awamu ya pili Ni utamaduni wa CCM kuachiwa agombee pekee? Kwani kama hii kweli Ni awamu Yake ya kwanza amegombea na nani?
Na ndio maana nimeuliza pia, vipi kama Magufuli angefariki miezi michache kabla ya kumaliza term yake ya pili, huyu makamu wake ambaye amerithi urais angeachwa kugombea bila kushindanishwa!?
 
Karejee kuisoma katiba ya chama,uone inasemaje,usijibu kwa sababu una mahaba nae Sana,hatukatai kuwa na mahaba nae ni haki yako ya kikatiba ,lakini usipotoshe miongozo na katiba ya chama inavyosema/kuelekeza. katiba ya chama na miongozo yake ni kubwa kuliko mwejkt wa chama.hoja yako inatoa picha kuwa mwjkt wa chama hapaswi kuguswa na katiba/yuko juu ya katiba ya chama!! Hoja uliyoitoa inaonyesha uchanga kwenye tasnia ya siasa,uongozi na utawala bola!
Kama ana ubavu Mkuu ajipime na wenzie. Achana na wanaume ajipime tu na wanawake wenzie humo chamani aone kama atatoboa. Mambo ya kujishaua haya na kulingishia watu sifa zisizokuwepo.
 
H
Na ndio maana nimeuliza pia, vipi kama Magufuli angefariki miezi michache kabla ya kumaliza term yake ya pili, huyu makamu wake ambaye amerithi urais angeachwa kugombea bila kushindanishwa!?
Hili Swali watoke CCM Walijibu. Chama kinaelekea kuwa cha hovyo kwa kujenga hoja za hovyo hovyo.
 
Tukubali baada ya "Mwendazake" sasa anayemrithi anakiri hadharani kuwa uwezo wake msiuwekee matumaini sana kama ambavyo tulifanya kwa "Mwendazake"?

Si kila viatu vinavyokutosha unatakiwa uvivae.

Si kila viatu visivyokutosha vinakufaa.

Si kila viatu vinavyokutosha vitakupendeza.

Huwezi kuta mwanaume analalamika viatu vya mkewe vingemtosha angeenda navyo kazini.

Kiongozi wa sasa viatu alivyovaa vina miezi sita.

Asiwaze mabuti ya asiyekuwepo hatakama alivyonavyo havifai kupigia mitama.
 
Nikiunganisha na hiyo Avatar naona maoni yako yana msukumo wa udini
Dini yako inasemaje? Inakueleza ?kuwa Kjongozi anajiteua tu na kujipachika? Mtume Muhammad alijiteua au alipewa utume na Malaika Jibrili kama inavyoadithia Kurani?
 
Si kila viatu vinavyokutosha unatakiwa uvivae.

Si kila viatu visivyokutosha vinakufaa.

Si kila viatu vinavyokutosha vitakupendeza.

Huwezi kuta mwanaume analalamika viatu vya mkewe vingemtosha angeenda navyo kazini.

Kiongozi wa sasa viatu alivyovaa vina miezi sita.

Asiwaze mabuti ya asiyekuwepo hatakama alivyonavyo havifai kupigia mitama.
Alitakiwa ayajue haya. Kile kitendo cha kulilia Viatu vya wengine vimjae ndio kuonyesha uwezo Mdogo na hapa ndio Makala imelala
 
Ni ukweli uliokuwa wazi kuwa hata kabla ya yeye kushika wadhifa huo wa juu wa Nchi watu wengi hawakuwahi kuutambua uwezo wake. Uwezo ni jambo ambalo huwezi kuuficha mithili ya Sindano kwenye Koti. Mungu wetu angalikuwa wa ajabu sana kwa uwezo wake mkuu alionao kama angaliumba wanadamu halafu uwezo wao ukafikichika halafu kisha akatutaka tuongazane. Tungaliongozana vipi kama uwezo wa kila mmoja wetu ungalikuwa umefichika?

Uwezo wa mwanadamu uko wazi. Uwezo wa kufikiri,kutenda,kuamua, kusaidia. Huo uko wazi wazi. Unasomeka waziwazi. Uwezo wa kuongoza wengine ni tabia na Sifa ambazo toka kuumbwa mwanadau Mungu anauweka hadharani. Ni kama tabia ya Ucheshi, Upole, Ukali, moyo wa kusaidia, Moyo wa huruma na moyo wa Ibada na Sifa zinginezo zilivyo wazi kupitia macho,kutembea kwa mtu, kuongea kwa mtu, kusikiliza kwa mtu, kula kwa mtu,kuvaa kwa mtu na kadhalika.

Kama nilivyotangulia kusema awali, watu wengi ndani na nje ya chama chake hawakuwahi kukunwa na utendaji wake licha ya kwamba alifanikiwa kushika Nyadhifa kadhaa huko nyuma kwa upande wa pili wa Nchi yetu. Na hata alipoingia kiwadhifa upande huu wa Nchi bado watu hawakuwahi kukunwa na utendaji wake kiasi cha kufikiria kuwa tunaweza kufikiria kumpa kazi ya kutuongoza katika nafasi nzito kama hii ya sasa. Wanaomjua vizuri ndani ya Chama wanakueleza kuwa ndio maana hata mwaka 2015 hakuwa miongoni mwa waliotia nia ya kugombea Uongozi wa juu wa Nchi kwa sababu hata yeye aliamini hana uwezo huo. Ni kwa sababu hata yeye mwenyewe alijua toka sakafu ya moyo wake kuwa Viatu vya Nchi yetu kwa mazingira ya sasa na yajayo vinampwaya. Ilikuwaje basi akateuliwa kuwa Msaidizi wa Mvaa viatu Mkuu wakati ule?Swali hilo sio sehemu ya mjadala wa leo bali siku nyingine.

Basi,imeshatokea yaliyotokea na hakukuwa na namna ya kufanya Zaidi ya kuangalia Katiba yetu inasemaje, Ilitarajiwa basi kwa kujitambua kuwa hata wale waliokwisha kufanya naye kazi wanamjua kuwa uwezo wake sio wa kutisha na wa kuvutia, angalivaa uungwana wa kusema ngoja mimi nishike tu mpaka mwisho wa Muhula wa Kikatiba na kisha nisimamie mchakato wa kumpata mtu mwingine mwenye uwezo sawia au zaidi ya yule ambaye nimeziba pengo lake. Kinyume chake na kwa mshangao mkubwa, tumesikia tu anajitangaza kuwa ATAGOMBEA ifikapo Mwaka 2025! Na la kushangaza Zaidi hajasema kuwa ataruhusu na wengine nao wagombee ili kushindanisha Sifa na uwezo wa kiuongozi kama ilivyotokea kwa yule aliyeziba pengo lake.

Kingine cha kushangaza Zaidi, amesema atatumia BAHATI HIYO ALIYOPEWA NA “MUNGU” (yeye anaiita bahati toka kwa Mungu kwa mwenzie kufa na yeye kisha kurithi utawala) kuhakikisha wanawake nao sasa wanatawala Nchi rasmi kwa kuchaguliwa kwa kura ili kuonyesha kuwa nao wanao uwezo wa kuongoza Nchi. Ilitarajiwa kuwa kama anaridhika kuwa kweli wanawake wanao uwezo wa kutuongoza (na kweli wapo wanawake wenye uwezo) angalisema wakati anajitangaza kuwa mchakato wa kugombea uongozi wa Nchi hapo mwaka 2025 katika Chama chake utahusisha wanawake wengine pia na yeye akiwemo.

Kilele cha kushangaza lakini ukiwa ndio ukweli ambao mtaani unajulikana kwa kila Mtanzania aliye hai (bila hata kuhitaji mashine kama CT SCAN kuchunguza uwezo wake) yeye mwenyewe ameutangazia ulimwengu na Taifa kwa ujumla kuwa viatu vya Mtangulizi wake VINAPWAYA SANA! Huu ni ndio ukweli. Ukimuuliza mtu yeyote mtaani hata wale wanaotafuta kuteuliwa au wale wanaomsaidia ili waweze kupata ujira wao kutoka kwenye sakafu ya mioyo yao watakueleza kuwa uwezo wake ni wa kawaida sana kulinganisha na nafasi alionao.

Kwa hiyo, Bandiko hili nimelenga kukiuliza maswali ya msingi sana Chama chake. Ni muhimu chake kijitokeze kujibu maswali haya kwa faida ya taifa letu na kizazi kijacho. Na bandiko hili ninakaribisha pia maswali mengine yaulizwe dhidi ya Chama chake. Na Zaidi, vile vyombo vinavyohusika na masuala ya Uchaguzi, maswali haya yasipojibiwa na Chama husika na wasipoghairisha uamuzi wake huo, watoke watuthibitishie kuwa ikiwa atapitishwa na Chama chake kugombea bila kushindanishwa na wengine na akanyimwa kura (na watanzania wengi ambao mpaka sasa hawaamini uwezo wake na wala hawapendi kuona mtu kama huyo akipata tena miaka mitano) watamtangaza bila woga mtanzania tofauti na yeye toka Vyama vingine atakayekuwa ameaminiwa kwa uwezo wake?


SASA hebu tuuulizane. Hivi, Chama cha Mapinduzi,CCM:



1. Mlipofanya tathimini baada ya uchaguzi wa Mwaka 2010 na kuamua chama kijisafishe kwa kuwaondoa waliokuwa wanakichafua Chama na matokeo yake ikawa ni kuondolewa kwa akina Lowasa na Mafisadi wengine chamani na matokeo ikawa ni Marehemu Magufuli kukibeba Chama, kabla ya uchaguzi wa Mwaka 2025 mtafanya tathimini tena kuona jinsi halisi kabisa ya jinsi uchaguzi wa Mwaka jana mlivyoshinda au mlivyoshindwa?

2. CCM ikiwa mtafanya tathimini ya ukweli kabisa na kugundua kuwa pamoja na kwamba Marehemu Magufuli alikuwa na uwezo mkubwa sana kiuongozi,kimaono na Kifalsafa (viatu vilikuwa vinamtosha) na aliwafanyia watanzania mambo mengi na makubwa vile kwa muda mfupi lakini bado alihenyeshwa sana na wapinzani, je, huyu mgombea wenu anayetarajia kuwa peke yake chamani (au aliyekwisha kujitangaza kuwa mgombea) ataweza kweli kukivusha Chama kwenye Uchaguzi huo wa mwaka 2025?

3. CCM, kwa kuwa mgombea wenu mwenyewe akiwa na sound Mind amekiri kuwa “Viatu” vya Marehemu Raisi Magufuli vinampwaya anataka kugombea hapo mwaka 2025 ili kufanya nini hasa ikiwa anakiri hadharani kuwa spidi aliyokuwa amelionyesha Taifa letu Marehemu raisi Magufuli kuwa ndio spidi ambayo watanzania wanahitaji kuwa nayo kimaendeleo Na yeye haimudu?

4. CCM, mnapoongea juu ya Chama mnakuwa mnamaanisha nini hasa? Je, chama chenu siku hizi chama ni mwenyekiti au wanachama?

5. Hivi, CCM kwenye Chama chenu Mwenyekiti maana yake ni nini? Ni muongoza wanachama au kufikia kutoa maamzi au yeye ni mtoa maamuzi wa mwisho na tena bila Vikao na akishasema jambo hapingiwi kama jambo lenyewe haliko sawa?

6. Je, Mwenyekiti wenu mlienza kusema hatakiwi kupingwa ndani ya Chama mwaka 2025, kwa misingi ya kwamba wanachama wote ndani ya Chama wana haki sawa, mnaweza kuitisha Mkutano maalumu na kumuuliza ni kwa nini ametangaza kugombea uraisi kabla ya muda? Ni kwa nini mumekaa Kimya bila kumuita kwenye kamati ya maadili ili kumuhoji sababu za kujitangaza ilhali chama hakijaanza mchakato wa ndani wa uchaguzi wa mwaka 2025?

7. Je, CCM hivi na wanachama wengine wa chama chenu wakianza kusimama huko majimboni na kujitangaza kugombea Ubunge na udiwani mtakaa kimya kama mlivyokaa kimya kwa huyu Mgombea wenu pekee wa Raisi?

8. Hivi, CCM Mtu anayejitangaza kuwa ni mgombea anayetaka kuonyesha kuwa wanawake wanaweza ila tu kwa muda mrefu wanaume ndo wamewakandamiza, anawezaje wakati huo huo tena kusimama na kusema uwezo wake haulingani kabisa na wa Raisi ambaye alilinyanyau Taifa letu na Chama chenu angalau kuweza kupewa kura na watanzania kwa sababu watu walikuwa wanamuamini yeye na sio Chama?

9. Mhe. Pole Pole, Katibu Mwenezi wa zamani wa CCM, unayeendesha Shule ya Uongozi(na nikiri napenda Falsafa yako juu ya maendeleo ya Nchi yetu kutegemea rasilimali za Nchi kuliko kuamini kuwa tunaweza kuendelea kwa kubeba mabakuli ya misaada) unaweza kujitokeza katika vipindi vyako vijavyo vya shule ya Uongozi kuchambua kasumba na tabia hii ya Mwanachama Mwenzako kujitangaza yeye mwenyewe kuwa anao uwezo badala ya Chama kumuona kuwa anao uwezo?Je, ukiwa utaogopa kufanya hivyo, Uongozi na Falsafa yako ya kusema Ukweli daima, itakuwa bado na maana na unadhani wanachama wenzio watastahili kuendelea na kuyaamini bado hayo mavipindi yako?

10. CCM, itakuwa ni nidhamu au ndio heshima kwa kuogopa kumuita Mwanachama wenu kumuuliza ni kwa nini amekiuka Taratibu, Miiko na kanuni za Chama kwa kujitangaza mapema kama Mgombea Mwanamke ilhali alishawazuia wanachama wengine kuacha mara moja kuhangaika na jambo hilo kabla ya muda wake?

11. Katibu Mkuu wa CCM,Komredi Daniel Chongolo kama mtunza Dira, Falsafa na Maono ya Chama wakati ule marehemu Holace Kolimba aliposema Chama chenu kilikuwa kimepoteza dira aliitwa Dodoma kujieleza, wewe kwa nafasi yako ya mchora Falsafa ya Chama umekusudia kuchukua hatua gani dhidi ya mwanachama wako aliyejitangaza mgombea wa Uraisi mwaka 2025 kabla Chama hakijakaa na kuruhusu wanachama kuanza kujitangaza?Je, Ukishindwa kuchukua hatua kama zile ulizoelekeza dhidi ya wale wanachama ulioelekeza vikao vya maadili viwajadili kwa kile kilichoonekana kukosa maadili utakuwa bado unaonekana kama Katibu wa Chama mwenye dhamana ya kulinda na kutetea Falsafa,Itikadi, sera, miongozo na maono ya Chama kwa Ujumla?

12. Katibu Mkuu wa Chama, Komredi Chongolo, kwa kuwa tumezoea Kila awamu ya Uongozi wa nchi yetu kupitia Chama chenu, kutanguliwa na uchaguzi au mchujo wa wagombea na kisha awamu ya pili ndio mhusika aliyepeperusha Bendera ya Chama chenu kuwa mgombea pekee wa Chama chenu kama ilivyotokea kwa Maraisi Mwinyi, Mkapa, Kikwete, na hatimaye Raisi Magufuli, je, mtaelekeza mgombea wenu mwaka 2025 agombee baada ya kushindanishwa na wenzie chamani kwa sababu bila kufanya hivyo atakuwa ni mgombea ambaye ataweka historia ya kugombea bila kutoka jasho kama wenzie? Je, Mkimruhsu agombee awamu ya pili bila kushindanishwa uwezo na wenzie chamani hamuoni kuwa mtakuwa mmetunga kanuni na muongozo mpya kuwa ikitokea mtu amerithi nafasi ya marehemu katika nafasi ya uraisi, basi anakuwa amepata mteremko kutawala?

13. CCM, Chama cha Mapinduzi ile ahadi yenu ya kuwaletea watanzania wagombea wenye uwezo wanaopatikana kwa kushidanishwa uwezo mnaelekea kuitelekeza na badala yake hamuoni kama mnaelekea kuasisi aina ya Uongozi wa mtelemko au Uongozi Dezo,yaani uongozi wa wanachama wenu labda kufikia kuwa anaomba Dua ili kiongozi aliye juu yake afe ili achukue madaraka kiulaini kwa kuamini awamu inayofuata atagombea peke yake?

14. CCM, mgombea wenu huyu ikiwa atakuwa wa pekee, mumefanya utafiti mtaani ni kweli anachagulika? Ni mgombea ambaye akishindanishwa na vyama vingine makini mnaweza kusema kwa dhati kuwa kweli atatoboa kabla hata Jogoo hajawika?Ni kwa nini hamumuelezi ukweli kuwa hachaguliki?

15. CCM, mgombea wenu ikiwa atagombea ndani ya chama chenu pekee, akitegemea wanawake wenzie kumbeba, anafahamu kuwa ni wanawake hao hao ambao hawampendi na wanamsema vibaya huku mitaani?

16. CCM, ni kwa nini Mgombea wenu hakujitokeza wakati Marehemu Magufuli yupo hai kutangaza hadharani kuwa angegomembea ifikapo mwaka 2025 ili kudhihirisha kuwa wanawake wakiongozwa na yeye wanao uwezo kwa kuliongoza Taifa hili? Alikuwa anaogopa nini? Kwa nini alificha nia hiyo? Je, Kiongozi anayejiamini anastahili kuficha Nia yake njema katika kuwaonyesha watu wake kuwa anataka kuwapeleka hatua Fulani kimaedeleo au Kiongozi anayejiamini anastahili kutaka kuongoza kwa kuvizia au kunyatianyatia na kujifichajificha?


Itoshe basi. Nimehoji sana na hata nikisema niendelee sitamaliza. Nina maswali mengi sana juu ya Chama chenu na mienendo yenu juu ya jinsi wanachama wenu mnavyokusudia wapatikane kuanzia sasa.Hii Nchi ni yetu sote. Mungu hajawahi kuandika Memorandumu of Understanding na Chama cha Mapinduzi kuwa ninyi ndo muvae pekee nira ya Kuwaletea watanzania maendeleo. Na wala Mungu hajawahi kuufanya Uongozi wa viumbe wake sisi kama fashion. Yeye mwenyewe kupitia mwanaye Yesu Kristu,Mungu kweli kutoka kwa Mungu, hakupata kuridhia nafasi yoyote ya Kiuongozi kwa yoyote yule kujitangazia Uongozi wa Kondoo wake bali yeye mwenyewe aliwaweka wale aliowaona wanafaa na ni mfano huo huo aliotuachia sisi Wakristu na wanadamu wote kupitia Kanisa lake Takatifu na ndio maana hakuna Kasisi au Askofu wa Kanisa lake Takatifu anajiteua katika nafasi yoyote bali anaombewa kuwa Kiongozi katika Kanisa. Tabia hii ya kujisimika madarakani na huku wakati huo huo mkikiri kuwa uwezo wenu ni wa kawaida muiache. Tanzania sasa sio uwanja wa watu kuhitaji kuongoza ilhali wanaamini hawana uwezo unaolingana na matarajio ya wapiga kura.

Kila zama na mambo yake. Mama yetu chapa kazi achana na hao kama huyu
 
Chuki ya nini na dhidi ya nini na nani? Mtu amesema Viatu vya mtangulizi wake vinampwaya sasa sisi kuhoji kama vinampwaya anatafuta nini tena kwa kuhitaji kuvivaa Viatu hivyo hivyo na hiyo ndo imekuwa Chuki?

Huo ni msemo tu. Rais Mstaafu Mwinyi Aliwahi kusema yeye ni kichuguu na Nyerere ni mlima. Panua uelewa wako.
 
Hivi unamkumbuka mh.Membe?!!

Kipi kilimkuta baada ya KUTAKA KUGOMBEA URAIS NDANI YA CCM?!!

Usijitoe ufahamu kama mtoto mdogo "mlizi".....

Kama watanzania tunastahili rais bora.

Rais bora si kwa mawazo ya mtu mmoja au hata kikundi chochote bali kupitia ushindani wa wazi na haki tutampata mtu huyo.

Kwa nini hamtaki tupate mtu bora kupitia ushindani huru na ulio wa haki?
 
Kama watanzania tunastahili rais bora.

Rais bora si kwa mawazo ya mtu mmoja au hata kikundi chochote bali kupitia ushindani wa wazi na haki tutampata mtu huyo.

Kwa nini hamtaki tupate mtu bora kupitia ushindani huru na ulio wa haki?
Wanaogopa ushindani na hapo hapo hawakomi kujiita Viongozi Bora! Unakuwaje bora kama hakuna wa kujipima Naye?
 
In short watu wa namna hii hawafai. Nia yao ni kuwaengua wengine kimzengwe mzengwe tu.
Halafu Ni tabia kama ya MbwaKoko kukoromea baadhi ya Mbwa tu huku wengine akiwagwaya. Wao wanajitia kimbelembele kuwakoromea wapinzani wanamuogopa Mgombea aliyejitangaza kabla ya muda
 
Back
Top Bottom