Dada mbishi wewe...
Wasanii wengine kusema wanafanya anachofanya Diamond, bado hawafanyi japo kuna wachache wanaojitahidi kwa mbaaaali..
Tofauti na jina kubwa alilonalo diamond na mafanikio yake kimuziki, jamaa kwenye social media anafuatiliwa sana na ndio sehemu mojawapo ya kutangaza bidhaa.. Chukulia mfano facebook alikiba anamashabiki elfu themanini na kitu 80,000+ wakati Diamond anamashabiki zaidi ya milioni moja, laki na tisini 1,190,000+, ukija instagram diamond anawatu milioni mbili, huku alikiba anawatu milioni moja kama ni kuchagua kampuni itamkimbilia yupi???? labda wajivishe ubasata ndio watakimbilia kwa alikiba, otherwise HAWAWEZI
Umeona picha alipokuwa anasaini mkataba wa Red gold tomato sauce??? Amesaini kwenye ofisi zake mwenyewe za WCB wasafi, sasa swali kwako msanii gani anayo ofisi angalau hata iwe ya kutisha kwa wadau kipindi wanapo bargain price??? HAKUNA
Uliliona tangazo la voda? Kuanzia audio, video, photoshoot, vyote vimefanyika kwenye ofisi zake za WCB kitu kinachoonesha ni kwa kiasi gani brand ilivyojikamilisha, na baada ya hapo video ikawekwa youtube kwenye account ya diamond yenye mashabiki zaidi ya 260,000+ akiwa msanii wa tatu Afrika baada ya psquare na davido, huku tanzania hakuna msanii aliyefikia hata mashabiki 50,000 na ndani ya video kuna added advantage ya kuonekana kwa Zari, Tiffah na mama Diamond, Je kuna familia ipi ya mwanamuziki wa bongo wenye publicity inayokaribia familia ya Diamond??? HAKUNA.. Kitaani watu wanamfahamu princess tiffah vizuri kuliko hata baadhi ya mastaa
KAMA ULIYAFICHA MADESA YAKO SEHEMU NENDA KAFEKENYUE, MAJOR AIM OF BUSINESSES IS TO MAKE PROFIT SASA SIJUI UNATAKA BIASHARA IYUMBE KISA TEAM ZA KIJINGA?