Inakuaje vijana Wamarekani hawana hamasa na kazi za jeshi Marekani?

Inakuaje vijana Wamarekani hawana hamasa na kazi za jeshi Marekani?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Jinsi ambavyo huwa naona hapa bongo watu wanavyogombania kazi za jeshini hadi wengine wanahonga, wanaenda kwa vimemo na wengine kutapeliwa huwa nashangaa sana jinsi jeshi la Marekani linvyoshindwa kufikia malengo yake ya kuajiri wanajeshi wapya hadi inabidi kubembeleza watu au kushusha vigezo.

Mwaka huu wameongeza kikomo cha umri wa kuingia jeshini kutoka miaka 35 hadi miaka 42, pia hata kama imethibitika ni mvuta bangi wanakupokea tofauti na zamani!

Raia wa Tanzania ni wazalendo kuliko Wamarekani hadi kupenda hivyo kazi za jeshi?


20260409_144315.jpg
 
Hiyo Nchi opportunity ni Nyingi tu za kumake more than ukiwa kwenye Jeshi.

Kingine wananchi wengi wako na common sense, Jeshi na common sense haviivi saaana.
One thing for sure , US army walikuwa na utaratibu wa kuchukua watu cream kwenye jamii. Hii hatua ya kusajili wavuta bangi si dalili nzuri.
 
Kujiunga na jeshi ndani ya USA ni highly risk coz USA regime ni warmongers.

Contestant yeyote anayetaka kuiongoza USA lazima abainishe kwa marefu na mapana jinsi gani atakabiliana na ugaidi na masuala mazima ya vita dhidi ya mahasimu wa USA.
So kuwa mjeda USA ni direct ticket ya kwenda vitani.

Tanzania ni nadra sana kuingia vitani. Wapo wanajeshi wengi tu wamekuwa recruited na kulitumikia jeshi hadi kustafu pasipo kushiriki vita yeyote zaidi zaidi vita wanayopigana ni maigizo ya kuvunja matofali kwa ugoko na kulea vitambi.
 
Back
Top Bottom