Inakuaje vijana Wamarekani hawana hamasa na kazi za jeshi Marekani?

Inakuaje vijana Wamarekani hawana hamasa na kazi za jeshi Marekani?

Huenda ikawa sio kazi yenye maslahi makubwa wala heshima ...ila kwa Tz jeshi ni ulaji ni heshima pia kua mwanajeshi japo 29 october waliivua heshima yao.
Kwamba haina maslahi duh. Wabongo asee kwa kuchekesha !
 
Vijana wengi tayari wana access ya maisha bora, mfumo wao wa elimu, kazi, n.k

Wengi kuingia jeshini wanaona kama ni risk according na yanayoendelea huko.

Kwa Tanzania, ajira ni chache so the last option mtu anayokuwa nayo baada ya ku-hustle sana mtaani ni kujiunga na jeshi au uaskari.
Jeshi au uaskari ndo nini?
 
Hawapendi kwa sababu marekani inashiriki sana kwenye vita ndiyo maana wanaogopa kujiunga tofauti na Tanzania hakuna vita japo Afcon ikianza tunakiwasha ili hawa wanajeshi wetu goigoi tuwachangamshe
Maiti mtarajiwa
 
Jinsi ambavyo huwa naona hapa bongo watu wanavyogombania kazi za jeshini hadi wengine wanahonga, wanaenda kwa vimemo na wengine kutapeliwa huwa nashangaa sana jinsi jeshi la Marekani linvyoshindwa kufikia malengo yake ya kuajiri wanajeshi wapya hadi inabidi kubembeleza watu au kushusha vigezo.

Mwaka huu wameongeza kikomo cha umri wa kuingia jeshini kutoka miaka 35 hadi miaka 42, pia hata kama imethibitika ni mvuta bangi wanakupokea tofauti na zamani!

Raia wa Tanzania ni wazalendo kuliko Wamarekani hadi kupenda hivyo kazi za jeshi?

View attachment 3569971
1. Vijana Marekani wana option za kufanya kazi nyingi. Uchumi wa Marekani ulivyo, sehemu nyingi, tangu ukifikisha miaka 17 hukosi kazi ya kufanya wakati bado uko high school.
Katika uchumi wenye kazi nyingi za kufanya, si kazima watu wajilundike jeshini. Tanzania kuna watu wengi wanalundikana kufanya kazi jeshini si kwa sababu wanaoenda jeshi (ingawa hawa nao wapo) bali kwa sababu jeshi ni sehemu ya kuoata ajira tu.

2. Vijana wa Kimarekani wengi wanaona jeshini ni sehemu ya kuipigania nchi ambayo pengine haisimamii misingi ya falsafa zao. Sasa hivi si vijana walio nje ya jeshi tu wanaogomea kuingia kwenye jeshi, hata walio jeshini wanatoka jeshini. Kwa uchumi wa Marekqni mtu ana uhuru wa kiuchuni kusema anaona kazi ya jeshi haiendani na falsafa zaje anatoka jeshini. Tanzania sifikiri kuwa juna uhuru huo.

3. Tanzania ni nchi inayoendeshwa kwa sadism. Kuwa mwanajeshi ni nafasi ya kufanya sadism. Mwanajeshi anautumia uanajeshi wake kufanya sadism bila kushikwa shati kwa sababu ni mwanajeshi. Marekani kuna sheria mwanajeshi hana nguvu ya kurusha watu kichurachura kijingajinga.
 
Hii point ya tatu inasikitisha sana, na hii ipo kwa nchi nyingi sana za KiAfrica, labda kuna jambo zaidi ya kuwa ni sadism kwa sababu pia huwa naona kwa raia wengi ubabe wa wanajeshi dhidi ya raia ni jambo la kawaida au hata linalofurahiwa na kuhusudiwa na raia wengi.
 
Hii point ya tatu inasikitisha sana, na hii ipo kwa nchi nyingi sana za KiAfrica, labda kuna jambo zaidi ya kuwa ni sadism.
Watu masikini ukiwapa nafasi ndogo tu wana uwezekano mkubwa wa kuwa sadists kwa sababu hawana control na mambo mengi duniani maisha yamewapiga sana mwishowe na wao wanatafuta mnyonge wao kummalizia hasira zao tu.

Wewe hushangai hata kwenye vifungo vinavyotolewa kwa wahalifu nchi tajiri vifungo si vikubwa, jela ziko kama hoteli. Lengo linakuwa kumrekebisha tabia mtu.

Halafu angalia huku kwetu sasa watu wanakomoana. Gereza lilivyokaa ukifungwa hata miaka mitano tu ni kama unafungwa hukumu ya kifo tu.
 
Back
Top Bottom