Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

Nimefuatilia maandiko mbalimbali kuhusu ukabila, udini na Sasa ruzuku ya chama Chadema na kubaini upo umuhimu wa kuwa na kiongoz imara ndipo uwe na chama imara.

Ni ajabu kwa viongozi wa nchi hii kuanzia DC hadi katibu mwenezi na uvccm kutaka kuamisha Watanzania kwamba mwenyekiti wa Chadema ni mwizi ila hawana uwezo wa kumpeleka kwa pilato.

Nimefuatilia kama Mbowe Ana Kinga ya kushtakiwa nakubaini hana Kinga na ndio maana hadi Sasa anaudhuria kisutu toka mwaka Jana kwa kesi ya Aqwilina. Kama hana kinga na ni mwizi wa ruzuku kwanini TAKUKURU hawajamfikisha mahakamani?

Kama Mbowe ni mbaya kwa wana CCM na siyo mwenyekiti wao wanaumia nini akiwaongoza wana Chadema?Mbona hakuna anayesema Mbowe akiomba kujiunga CCM hatopokelewa? Kwann ukiwa upinzani ndo unakuwa mbovu ukiingia CCM tunaaminishwa wewe ni mwema na unapewa hadi uongozi?

Hii inanifanya niamini kuwa kamanda Mbowe ni mwiba kwa CCM na hata wakihama wote kwenda Chadema na akabaki mwenyewe bado CCM hawatolala maana wanajua tatizo ni uimara wa mwenyekiti, wabunge hata wakiondoka wote Leo ila wakabaki watu imara bado Chadema itabaki kuwepo.

Mbowe hata wakikuacha wote usitetereke ipo siku upande wa pili utawachuja na watakuja kukupigia magoti .Kama walimtema katibu mwenezi watashindwa nn kuwatenga hao wasaka tonge?
Takataka,unafaidika na uhalifu wa mwenyekiti wako makengeza
 
Sssssss
tapatalk_1539011417405.jpeg
 
Tunataka Komu apewe uenyekiti CDM.Kama Lipumba alivyopewa CUF.
 
Siyo CCM tu hata Mungu anataka hivyo kwa sababu muda wake umekwisha na anapaswa kupisha wengine kama yeye walivyompisha pia, vinginevyo afute neno ,,demokrasia” kwenye chadema.
Nendeni kwa cheyo,dovutwa lipumba,na mrema
 
Ajenda yao halisi ni kuondoa Mbowe waweke mamluki wao.
Kukalia kiti muda mrefu mbona hawawasemi akina mrema, cheyo, lipumba waliodumu muda mrefu zaidi?
Kuhusu ruzuku, hyo ya Cdm hata haitoshelezi mahitaji..
Ukiwauliza wao wanachukua ngapi na wanatumiaje utashangaa
 
Ujinga ni kumtetea Mbowe, wakati mnajua kabisa kavunja katiba ya Chama kwa kupitiliza ukomo wa Uongozi.

Chadema sio Saccos kwamba mtu anaweza kuendesha maisha yake yote, Chadema ni Chama cha wananchi kinachoendeshwa na kodi za wananchi....hivyo sheria lazima zifuatwe kwenye uendeshaji wake.

Naona wafuasi wa Mbowe mnavyohangaika kumpa uhalali boss wenu kuendelea kutafuna ruzuku.

Mara Kubenea,Kom ama CCM hamjui mchawi wa Mbowe ni Mbowe mwenyewe.... Demokrasia tunayoililia kila siku lazima tuwe tayari kuiishi hata kama Chungu.

Wewe mfuasi wa nani?
 
Mbowe ni kikwazo; ni lazima kuweka shinikizo ang'oke ili tujaribu kuweka mtu ambaye tutaelewana naye kwenye baadhi ya masuala hasa ya kisiasa!!
 
Back
Top Bottom