M/kiti amekuwa mwiba kwa ccm, hawalali wanamuota Mbowe kuwa watamuondoaje Chadema, Mbowe amekuwa nguzo muhimu kwa chadema na mageuzi kwa ujumla hapa Tanzania, ccm Kama kawaida yao wamezoea siasa za mtelemko lkn kwa Mbowe wamechemka sasa kazi ni moja, propaganda za kumchafua Mbowe zinazoongozwa na chakubanga, sasa hivi ukimuliza chakubanga ccm ina wanachama wangapi yeye atakujibu Mbowe hafai kabisa, ni mbinafsi, yaani mzimu wa Mbowe ndani ya viunga vya lumumba unatembea, siajabu mtu akikurupushwa usingizini anaweza kumtaja Mbowe. Chaajabu ukikutana na watu wa lumumba kati ya viongozi wa vyama ni yupi kakaa mrefu wao watakimbilia kusema ni Mbowe, hebu tuangalie :-
1. Cuf - m/kiti wake yupo pale miaka mingapi?
2. UDP -
3. TLP -
4. UPDP -
Wote hawa hawajawahi kubadilishwa kwanini Mbowe? Kuna jambo, chadema kuweni makini na mkakati wa ccm. Tujiulize, kuna mtu anaruhusiwa kugombea uenyekiti wa ccm? Au kuhoji kofia mbili za uongozi wa kitaifa? Kama haiwezekani kwao, kwanini wahoji kwa wenzao?