Ni kweli huu utetezi wa wanacdm wengi kuhusu Mbowe kukaa muda mrefu madarakani. Lakini tujiulize je ni kweli bila Mbowe cdm itayumba? Hivi inge/ikitokea Mbowe akafariki ndio mwisho wa cdm? Hivi hatuona kuwa kitendo cha Mbowe kumleta Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais ni ndio imechangia leo hii cdm kuongea kitu na watawala kuwapuuza? Huwezi kufananisha cdm ya kabla ya Lowassa na cdm baada ya kuwasili Lowassa. Inahitaji ushabiki wa kisiasa kuendelea kumpigia debe Mbowe kuwa mwenyekiti. Ni kweli amefanya mazuri mengi sana kukifikisha chama hapo kilipo, lakini kiukweli sasa ni wakati wa yeye kukaa pembeni na wala sio kwa matakwa ya ccm bali kutokana na uhalisia tu.