Inakuwaje CCM yenye wabunge zaidi ya 250 inashindwa kujitosheleza kwa sifa za uwaziri hadi hadi wanateuliwa wapinzani na akina Mwigullu kurudi tena?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kwa idadi ya wabunge wa CCM ambao ni zaidi ya 259 inashangaza kwanini wanashindwa kujaza nafasi zisizozidi 50 kwenye baraza la mawaziri.

Imefika wakati Rais Magufuli amelazimika kumteua Mwita Waitara aliyekuwa Chadema kabla ya kuhamia CCM na pia kuwarejesha barazani mh Simbachawene na Mwigullu Nchemba ambao awali aliwatumbua.

Hii inamaanisha CCM ina idadi kubwa ya wabunge lakini wenye ubora mdogo.

Niwaombe wanaccm mwaka huu tusirudie makosa ya kuwarundika bungeni mbumbumbu.....tujali ubora siyo wingi.
Watu wasio minesterial material wanastahili kuwepo upinzani siyo Chama tawala.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wabunge ni wakina Msukuma wanaojinasubu kuwa wana elimu ya darasa la saba.

Wengine wanashindwa kuhoji hoja ya Zitto kuwaomba IMF wasitishe mkopo wa maendeleo ya elimu kwa Tanzania wanaomba Zitto auliwe.
 
Wabunge ni wakina Msukuma wanaojinasubu kuwa wana elimu ya darasa la saba.

Wengine wanashindwa kuhoji hoja ya Zitto kuwaomba IFM wasitishe mkopo wa maendeleo ya elimu kwa Tanzania wanaomba Zitto auliwe.
Tangu lini IFM ikajihusisha na utoaji wa fedha za mikopo? IFM iko magogoni pale
Ni IMF bana! [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]

[emoji2398]ᵃʳᵉᵉᵐ [emoji769]
 
Nangojea misukule ije kutetea kama kawaida
 
It seems CCM kuna uhaba wa viongozi ndiyo maana wewe mwenyewe jana ulileta hapa uzi wa kumuomba John Mnyika ajitoe CDM aje kuwaongoza huko CCM
J J Mnyika ndio aliiandikia barua CCM kuomba kujiunga......alikubaliwa na ubunge atagombea mkoani siyo Kibamba!
 
Ushahidi mwingine huu hapa, Tulia, Kabudi, Mahiga, Mpango, Ndalichako. Hawa ni watu wameteuliwa na kushika nyadhifa za uwaziri/naibu spika baada ya kuona hapati watu wa aina hii kutoka kwa wabunge!!
Nimekuelewa bwashee!
 
Wabunge wa CCM wengi ni wabunge ndio wengine wapo kwaajiri ya maslahi yao binafsi, kwa watawala na posho... Wazalendo Ni wachache...

Usishangae waziri kutumbuliwa au kuhamishwa wizara au ofisi nyingine sababu ya kuharibu au skendo... Jiulize je wengine hawapo?.. jibu utapata kuwa Ni uzoefu!!! Uzoefu wa nn ufisadi au?!

CCM Ni Ile Ile kubadilika itachukua muda.
 
Ukweli ni kwamba CCM ni Mbuzi ya kukunia Nazi! Wabunge wengi wa CCM wamekunwa na kubaki vifuu vya Nazi! Mmoja alikuwa Professor Sasa anasema hadharani kuwa aliokotwa Jalalani.
 



Ni world bank au IMF ??!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…