Inakuwaje CCM yenye wabunge zaidi ya 250 inashindwa kujitosheleza kwa sifa za uwaziri hadi hadi wanateuliwa wapinzani na akina Mwigullu kurudi tena?

Inakuwaje CCM yenye wabunge zaidi ya 250 inashindwa kujitosheleza kwa sifa za uwaziri hadi hadi wanateuliwa wapinzani na akina Mwigullu kurudi tena?

Mkuu acha kuuliza majibu, unategemea rais anaweza kuteua kile kiazi cha mtela au msukuma kuwa waziri!
 
Waitara alikua ccm,akaenda chadema halafu akarudi
Katiba haimpangii Rais wateule,hao wote ni ccm,hata mbowe anayo.kadi ya ccm
Hiyo haiondoi ukweli kwamba Mwita Waitara alikimbia kumpikia chai Nchimbi na kuhamia Chadema!

Hata Kibajaji alitoka CCM akaenda Cuf kisha Chadema na kurudi tena CCM lakini uwaziri anausoma tu magazetini.

Nakutakia Dominica yenye baraka!
 
Siyo jambo dogo kutoa manaibu waziri watatu ambao wamepikwa kisiasa hapo Ufipa na hatimaye jicho la mamlaka kuwaona.

Pamoja na kuhamia CCM niwaombe sana manaibu waziri hawa mh Shonza, mh Waitara, na mh Dr Mollel muwe mabalozi wazuri kwa kile chema ambacho mlijifunza na kukipata wo mlipokuwa Chadema.

Niwapongeze pia Prof Kitila, mama Mgwira, Kafulila, Dr Slaa na mh Hamad Rashid wa Zanzibar kwa kusimamia vema utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ni kweli kabisa, na kupitia hapo, tunajifunza na hata kuweza kujifunza jinsi chadema lilivyo tanuru la kupika viongozi ili wewe na uwezo wa juu sana ukilinganisha na wale walikulia ccm?

Hiyo pia inatusaidia tuweze kufanya comparative analysis ya wale waliojengwa na chadema dhidi ya wale waliojengwa na ccm na kujua yupi ni yupi na kipi ni kipi.ukimuangalia mtu kama Mwita au Patrobas, ikiifikiria na Chadema na wanayoyasema, unajifunza mambo mengi muhimu.

Tujisahihishe.
 
Hapana mkuu.

Alikatwa ccm kwenye kura za maoni 2015 ndio hasira zake akahama ccm. Labda useme alipelekwa kwa mkopo CDM.
 
Siyo jambo dogo kutoa manaibu waziri watatu ambao wamepikwa kisiasa hapo Ufipa na hatimaye jicho la mamlaka kuwaona.

Pamoja na kuhamia CCM niwaombe sana manaibu waziri hawa mh Shonza, mh Waitara, na mh Dr Mollel muwe mabalozi wazuri kwa kile chema ambacho mlijifunza na kukipata wo mlipokuwa Chadema.

Niwapongeze pia Prof Kitila, mama Mgwira, Kafulila, Dr Slaa na mh Hamad Rashid wa Zanzibar kwa kusimamia vema utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Na ndio maana tangu wamechaguliwa hawajaharibu au kutumbuliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku hizi CCM haifanyi building capacity ya vijana wao...maana wengi wao ni wajuvi wa kuporomosha mitusi na dhihaka kwa viongozi wa upinzani huku wakishidwa kabisa kuzijibu hoja za wapinzani.

Asante Rais kwa kuliona hilo...CDM ni kama mtibwa sugar kwenye mambo ya soka...ni mtambo wa kuzalisha viongozi vijana kwa hazina ya Taifa.
 
Hivi kweli uongoze serikali yenye wabunge kama mlinga unategemea nini?? Yeye akiona mbunge wa upinzani anachangia lazima ainuke na miongozo yake kama amekunywa gongo, kale kajamaa kamejaza makamasi kichwani. Kuna wakati hadi najiuliza wabunge aina ile wameingiaje bungeni??
 
Kwa idadi ya wabunge wa CCM ambao ni zaidi ya 259 inashangaza kwanini wanashindwa kujaza nafasi zisizozidi 50 kwenye baraza la mawaziri.

Imefika wakati Rais Magufuli amelazimika kumteua Mwita Waitara aliyekuwa Chadema kabla ya kuhamia CCM na pia kuwarejesha barazani mh Simbachawene na Mwigullu Nchemba ambao awali aliwatumbua.

Hii inamaanisha CCM ina idadi kubwa ya wabunge lakini wenye ubora mdogo.

Niwaombe wanaccm mwaka huu tusirudie makosa ya kuwarundika bungeni mbumbumbu.....tujali ubora siyo wingi.
Watu wasio minesterial material wanastahili kuwepo upinzani siyo Chama tawala.

Maendeleo hayana vyama!
Wewe una akili sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom