UPUUZI!!!! TAKATAKA!! (Kwa sauti ya MUSIBA). Mtoa post hivi unajua kuwa Mtu kuwa na maarifa sio lazima aelewe lugha ya Kiingereza? na ndyo maana wataalam wanataka Lugha ya kiswahili ifundishwe mpaka vyuoni. Hivi haufahamu kuwa Wachina licha ya kupiga hatua kubwa ktk Uchumi wa Dunia lakini Mtaala wao wa Elimu unatumia Lugha yao ya kichina (Mandalin Chinese)? Hivi mtoa mada unafahamu nini kuhusu Lugha? Je unajua kuwa kila Lugha ni bora(Langauge Superiority)? Mtoa mada hivi unajua misingi ya kuwa na maarifa ktika nyanja ya kujifunzia au ktk nyanja ya taaluma fulani, hakuzingatii Lugha?
Mtoa mada, hivi unajua hata hicho kingereza kimetohoa maneno kutoka lugha nyingine? Kingereza cha karne ya 13 B k ni tofauti na cha sasa? Kasome shahiri linalojulikana kama "I too Sing America"..
Mtoa mada, mm ni Mwl. Katika Elements za lugha tunaangalia Arbitrarity (Unasibu). Ktk unasibu ndyo tunapata hizo lugha zote na ukisoma Unasibu utagundua kila lugha ni bora kwakuwa mwanadamu hazaliwi na lugha, bali anaikuta tu, nakuongezea hapa System, conventional, n.k.
Note: Sijasema watu wasijifunze kiingereza kwa kuwa ni Lugha inayozungumzwa ulimwengu mzima na hii ni kutokana na maendeleo yao tu, na kutawala baadhi ya maeneo Duniani kuanzia kipindi kile cha Utumwa, kipropaganda na kibiashara zaidi. Hata Lugha ya kiswahili ingekuwa kule Uingereza now na kingerza kingekuw hku basi kiswahili kingekuwa lugha maahughuli ulimwenguni, lakin ktk misingi ya kupata maarifa nakupinga.
Watu wajifunze kiingereza, kichina, kifaransa, kilatini, kiyahudi n.k kwakuwa Kila lugha ina umuhimu wake kama chombo kikuu cha mawasiliano; amabapo kupitia mawasiliano haya tunaweza kuhawilisha mitazamo yetu, kutoa maoni, mapendekezo, kubadilishana mawazo, kutuunganisha kibiashara, kiutamaduni, kijamii, kisiasa n.kl. Lakini ktk kupata maarifa kila jamii itumie lugha yake ili kuzalisha wasomi wanaoelewa kile walichojifunza zaidi. Tafiti zinaonesha kuwa mtu anayejifunza kwa Lugha yake huwa anaelewa zaidi(Mbobevu) kuliko yule anayetumia lugha nyingne. Kamsome Abraham Manslow ktk Language in learnig na John Locke, au achana na hawa wote utachanganyikikwa, naomba ukamsome BENJAMIN BLOOM Ktk ile Theory yake ya COGNITIVE DOMAIN ktk kipengele cha Learning, achana na Theory yake iliyozoeleka ya BLOOM TAXONOMY tafadhali!!!! alafu njoo hapa.
Achana kabisa na wakina Ivan Pavlov, B.F Skinner watakuchanganya hao.!!, _π
Nimemaliza