Inakuwaje mtu anamaliza degree hajui kuongea English?

Naomba niwe mkalimani , anasema hivi "

Unamaanisha nini kupatikana? Kupatikana kupitia elimu rasmi / isiyo rasmi?

Ninaona kuwa ngumu kupata hoja yako, kwa hivyo watu wote walioelimika ni watumwa wa mafanikio yao ya kitaaluma? Wivu kwa wale ambao wamefanikiwa kitaaluma hautakufanya ujifunze lugha. ".

Tumeelewana ?β€Š
 
Kila mtu anaweza kuwa mkalimani siku hizi. Google amewarahisishia vilaza wasiachwe nyuma.
 
Je ulijua kwanini yeye alikuwa anapata mademu wa Kishua na wewe hupati, ulimuuliza ?

Umejiuliza umekosa nini kwa yeye kupata huo uteuzi wakati wewe unahangaika? na Lugha?

Jitathmini utajua kwanini?
Alikuwa anawapata sababu yeye alikuwa anafake life sana sababu ni wa huko nje ya mji ( kibamba) ,Mimi sikuwa wa huko na sikuwa na uhitaji wa madem wa hivyo sababu walikuwa around me

Alikula teuzi simply sababu ya kuwa UVCCM kitambo sana na pia alikuwa ni good in speaking bla bla za siasa.

Mimi sijapata teuzi sababu nilikuwa nje ya mfumo wa kuweza kuteuliwa though nipo kwenye system .

So cool down mwamba.
 
super f..l
 
Kwani English si ni somo kati ya masomo kadhaa anayofundishwa?

Ufaulu na uelewa wake kwenye masomo mengine ukoje?

Kuna wanaoongea English, hawajui inaandikwaje, hivyo sio maarifa ya msingi mtu kujua katika maisha yake!
whats the point kama ulifaulu masomo kwa kutumia kiingereza afu hukijui maana yake ulikariri hiyo gpa uliipata vipi ?hizo hoja za kujibia maswali yao uliwezaje??
 
Haya mambo watu wanayadharau ila nikupe mfano kuna jamaa mmoja alinifanyia mchongo nikipata kazi kwenye ngo fulani ya kijerumani basi bwana mimi nilikua niko chini yake yeye alikua boss wangu sasa kulikua na jamaa mmoja mkenya yeye ndo alikua supervisor akawa anausisitiza tujitahidi tujue lugha ya kiingereza maana report kabla ya kusbmit jamaa ana zipitia anarekebisha anazituma. zikitokea presentation huyo mkenya anafanya maisha yanaenda basi siku huyu jamaa akawa ameenda kwao kenya jamaa yangu akashika nafasi yake aisee ikatokea presentation ofisini kuna wachina, wa ghana, na mataifa kama matano tofauti pale huu mkutano ulikua zanzibar, tukaandaa power point kama kawaida sasa wakati wa kupresent duuh yule jamaa yangu alitia aibu aisee pale mbele yaani ilibidi mzungu mmoja ambaye alikua boss mkubwa akaokoe jahazi pale akasingizia kwamba jamaa hayuko vizuri {anaumwa} . Baada ya kikao ilibidi jamaa afanyiwe recheck tena walidhani amedanganya kwamba ana masters ya hiko kitu H.R wa pale ofisini aliwapigia hadi ma referee
 
Siyo lazima kuongea english kwa ufasaha ndiyo uwe msomi. Kuandika na kuzungumza ni vitu viwili tofauti. Kuongea ni kwa kuwa na practice na lugha na ndiyo maana kuna watu hata hawakusoma lakini wanapiga lugha vizuri sana.

Nimewahi kukutana na wanasayansi wabobevu sana kwenye taaluma zao lakini wakifanya presentations kwenye mikutano ya kimataifa english yao ni ya kubabaisha (unaweza kuta mother tongue ni french au spanish). Na wala hakuna anayewacheka wala kuwakebehi kuwa hawajui lugha.
 
Aongee kiingereza kwani alisomea degree ya kuongea kiingereza?
 
whats the point kama ulifaulu masomo kwa kutumia kiingereza afu hukijui maana yake ulikariri hiyo gpa uliipata vipi ?hizo hoja za kujibia maswali yao uliwezaje??
Ni rahisi tu, Pythagoras sijui hata ina maana gani ila hesabu ndo inakwenda!

Kuna somo kamilifu la kiingereza, inanibidi nitumie muda gani kuweza kukielewa kwa level ya kukitumia kuelewa masomo mengini?

Wewe uliyekikuta kiingereza shule, umewahi au hata kujaribu KUWAZA kwa kutumia lugha ya kigeni?

Hivyo ndivyo wanavyopata hayo ma-gpa yao.
 
Yani balaa juu ya hatari
 
Hoja nzuri ila wachangiaji watakwambia English ni lugha tu kama kilivyo kihehe, kinyatulu nk, lakini hoja inakuwaje mtu utumie lugha ya hii taaluma toka darasa la 9 hadi chuo kikuu - miaka zaidi ya 9 ushindwe kuingoea ki ufasaha? unafauluje mitihani na presentations zako?
 
akilo zako ni finyo πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ex wangu ni mwalimu wa kingereza shule fulani nilivokua naye ndo nikajua watoto huko shuleni wanafundshwa unywanywa
 
Ili kuokoa watu wasiumbuke kwa kushindwa kuandika ruling zao kwa ufasaha, mweshimiwa mmoja alianzisha mkakati wa kuwaokoa kwa kuwaambia waandike kwa kiswahili.

Hii lugha sijui ikoje, unaweza kujifuza kichaga, kimakua ama kisukuma kwa mwaka 1 tu na ukawa fundi balaa, ila lugha hii vagosha yaani miaka 9 shuleni lakini hiiiii.. !! the the the ndo inajaa mate πŸ˜›πŸ˜› hadi unaomba panadol.
 
Hivi ukiambiwa uwe na msomi asiyeongea kiingereza kama "Marehemu" Mzee wetu au waongea kiingereza wasiokuwa wasomi kama Miss Tanzania wetu maarufu kuliko wote, ungemchagua nani?
 
Kuna vichaa huko uingereza wanapiga ngeli ya maana..!!!
Kiingereza chetu cha engineering kipo hivi....
Prove that X = Y
Kinachofuata ni kukata nyanga then pale mwishoni unamalizia tu.. HENCE PROVED
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…