KERO Inakuwaje mtu mwenye tiketi analazimishwa kulipia ushuru wa kuingia katika Stendi ya mabasi 88 Dodoma?

KERO Inakuwaje mtu mwenye tiketi analazimishwa kulipia ushuru wa kuingia katika Stendi ya mabasi 88 Dodoma?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Halmashauri ya Jiji la Dodoma inawaibia abiria waliokata tiketi kupitia mfumo kwa kuwalazimisha kulipia ushuru wa kuingia stendi na kupanda mabasi. Hili ni jambo lisilo sahihi ambalo sijawahi kuliona katika stendi nyingine za mikoani.

Ndiyo maana baadhi ya abiria wameanza kuepuka kupandia mabasi stendi na badala yake wanapandia kwenye ofisi za kampuni za mabasi.

Ofisi ya Waziri Mkuu–TAMISEMI na Wizara ya Uchukuzi, jambo hili si sahihi na linahitaji kushughulikiwa.

IMG-20260818-WA0009.jpg
 
Stand yoyote ile duniani, kama una ticket mkononi haupaswi kulipia.

Wewe unaenda kupanda gari, ambalo tayari limeshalipa tax. Abiriw unapaswa kuonesha ticket tu.
 
Pale msamvu moro huu usenge upo kwa mda sasa niliamsha ugomvi pale wakanisihi tu wao ni waajiliwa wanafata maelekezo ...hata kelele za mabasi yaishie magufuli inaweza kua wanataka kuanza huo wizi pale..serikali gani inakaa kuumiza wananchi huu ni wizi wa wazi
 
Nipo Stendi kuu ya mabasi Dodoma wanalazimisha abiria kulipa ushuru shiringi 300 hata kama tayari una ticket ya Bus.
 
Back
Top Bottom