Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,559
- 11,180
Asilimia kubwa ya binadamu mtu mzima anapenda na ana tamani kuoa na ukiona mtu hajaoa si jambo jema kumcheka kwani ukute ana mambo kibao ambayo yamepelekea yeye kutokuoa by the way ndoa ni ridhiko la nafsi mbili zilizoamua kuishi pamoja na si fedha na ndio maana ndoa nyingi zina fail kwa kuwa mtu ameweka malengo ya "NIKIPATA KAZI TU NAOA" na huwa hajiulizi je "JE KAZI IKIKATIKA NDANI YA NDOA ITAKUAJE?". Uwe huna kazi au una kazi au una hela au huna lakini kama mmekubaliana kwa pamoja kwamba mnahitaji kuishi pamoja kama mume na mke hapo ndio ndoa ya dhati