Inakuwaje mwanaume mpaka una miaka 30 au 40 haujaoa na una hela?

Ukioa mapema kuna uwezekano mkubwa wa kuupata umasikini

ambayo haijaoa mingi haipendi maendeleo ipo ipo tu inasubiri mtu wa kuja kumuinua labda malaika, walio ndani ya ndoa wengi wameendelea wanapata ile stability na uchu wa kutafuta maendeleo inapatikana nguvu kutoka pande zote mbili
 
Ni kweli kila mtu na comfortability na maamuzi yake mwengine hapendi maisha ya ndoa
 
ambayo haijaoa mingi haipendi maendeleo ipo ipo tu inasubiri mtu wa kuja kumuinua labda malaika, walio ndani ya ndoa wengi wameendelea wanapata ile stability na uchu wa kutafuta maendeleo inapatikana nguvu kutoka pande zote mbili

Mkuu ukikimbilia kuoa mapema kwa maisha yetu haya ya kubangaiza na upate na mwanamke kichwa maji then upate tu watoto wawili tu...usitegemee kutimiza ndoto ulizokuwa nazo kabla ya kuoa.
 

Ebana kuoa ni target na sio fassion elimrad tu umeoa! utakuja umie pamoja na kuwah kwako kuoa!
 
Kaa makini xana wew unaejdanganya kuoa mapema, kwanza kaa mbal xan ucje kutuambukza tabia yako ilvo mbaya.
 

Ni yupi mwenye nafuu: asiyeoa lakini anagonga binti za watu au aliyeoa lakini bado anachapa mabinti kibao pembeni???
 
kwani kuoa lazima!! kila mtu na mipango yake bwana.
we hiyo miaka 25 wengine bado wapo vyuoni na ndio kwanza masomo yamekolea.. kuoa sio fashion, mtu unaoa ndani una godoro tu, wengine pesa zipo lakini anajua nini hasa anachosubiri si kwamba amekaa tu we hujui anawaza nini au amepanga nini..
 
Leo ww ndo wa kukomenti hivi? mbona sitaki kuamini?
 
Ndo hapo nami nashangaa leo yamewakuta yapi?
 
Acha kupotosha umma ww!
Hizo western culture haziingiliani na maisha halisi ya kibongo!

Ndio maana katiba ya Tz inasema mojawapo ya sifa za rais awe ameoa au kuolewa!

Alafu kuoa au kuolewa ni sifa nzuri kwa jamii na humpendeza Mungu.

Mkuu hivi kweli na akili zako unadhani kuwa na mke au mume ndio uwezo wa kuongoza? Au kwako kwa sababu imeandikiwa kwenye katiba ndio kama mstahafu kwako?

Hivi suala la kuoa au kuolewa lina uhusiano gani na utamaduni? naweza kukubali kuwa aina ya kuona inahusiana na utamaduni lakini kuoa kwenyewe ni auamuzi na uwezo wa mtu.

Ulaya kuna watu wanaoa wakiwa na miaka 20, sasa tunaweza kusema tusioe na miaka 20 kwa kuwa ni western culture? au wanaaolewa na miaka 20 tunaweza kusema tusifanye hivyo kwa kuwa western culture wanafanya hivyo? Unaamini kuwa ukioa unaoa kwa ajili ya sifa au kumfurahisha mungu?

Vizuri tukielimisha mkuu, wengine tuko nyuma kiasi.
 
du ukisoma baadhi ya post za hapa unaona kabisa kuna watu bado wato stone age, wengine iron age wengine IT age.
 

Sijakuelewa hasa point yako iko wapi hapa?
 
Unaweza ukawa na pesa ila ukakosa busara za kuishi na mke kwa hiyo bora ujipange kwanza kupunguza watoto wa mitaani wanaotokana na ndoa za mwezi mmoja mara kila mtu njia yake
 
Pia wengine ni matokeo ya waliyopitia huko nyuma
 
Leo ww ndo wa kukomenti hivi? mbona sitaki kuamini?
uniqe DADA swala la mtu kuoa linahitaji kujipanga, na kujipanga si kuwa na pesa tu hata utayari wa akili.
siku hizi umri si tatizo, pengine mtu yawezekana hajaona wife material anayemhitaji au ishu nyingine. Hatuangalii mke tu,lazima upate picha ya familia nzima itakavyokuwa hapo baadaye.
 
Last edited by a moderator:
Sijakuelewa hasa point yako iko wapi hapa?

Unaposema hautuwezi kuiga utamaduni wa magharibi maana yake nini? Umesema kwa mazingira ya kibongo haiwezekani lakini ya kimagharibi inawezekana. Nimetoa mfano kuwa kuna watu magharibi wanaoa wakiwa na miaka 20 na wengine miaka 50. If we do the same can we be called imitating westerners? Point is ndoa si suala la kuiga, kila mtu ana conditions zake.

Unaposema hata kwenye katiba imeandikwa....ina maana wewe mawazo yako kuhusiana na ndoa yanatokana na katiba au mazingira yako binafsi? Au kuoa kunaongeza uwezo wa utendaji wa mtu kuwa rais? My point here is, marriage is a personal issue regardless of what constitution says. Na kama huna uwezo wa kuongoza hata ukioa au ukiolewa, hali hiyo haibadiliki licha ya kuandikwa kwenye katiba.

My main point is ndoa ni suala binafsi. kuona na miaka 20,40 au 60 ni uamuzi binafsi wa mtu. Kumuuliza mwanaume kwanini hajaoa is very gay.
 
Nimekuelewa kiongozi lakini kwa nini mwanamke anayefikisha miaka 30 hajaolewa huwa mnampiga majungu na kumuita majina mabaya?coz kama kuoa ni maamuzi ya mtu likewise kuolewa napo ni maamuzi ya mtu mwenyewe huwezi kulazimisha kuingia kwenye ndoa kisa marafiki zako,schoolmate,majirani zako wote wameoewa ndio ni zaidi ya tendo la ndoa so leo yamewakuta wanaume mnakuwa wakali hebu acheni kuogopa majukumu bana OENI
 
Last edited by a moderator:

haha hakuna anayeogopa majukumu... mwanamke hata akifikisha miaka 30 hajaolewa siwezi kushangaa...ila zaidi ya hapo lazima kuna tatizo ila sio kwa mwanaume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…