Inakuwaje Mzazi Anaweza Lea Watoto Kadhaa Lakini Watoto hawawezi Kulea Mzazi Wao

Inakuwaje Mzazi Anaweza Lea Watoto Kadhaa Lakini Watoto hawawezi Kulea Mzazi Wao

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Screenshot_20241230_113433_Google.jpg


Nikiwa ndani ya mwendo kasi miezi kadhaa iliyopita,abiria mwenzangu anaongea na mtu kwenye simu kuhusiana na watoto ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao apate matibabu

Baada ya kukata simu yule bwana nikaendeleza mazungumzo yake kwakuwa yalinigusa sana,ndo akanipa kisa cha watoto takribani watano ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao kwa kutoa fedha zao

Bila aibu wanataka mzazi wao akishavuna mazao yake ayauze kisha ndio wakamtibie,tena cha kushangaza sio kwamba watoto wote wapo vibaya,baadhi yao wapo vizur kiuchumi,huyo first born yupo vizur lakini kichwani hakuna kitu

Kweli walisema waswahili kuzaa si kupata,hata kama kuna mambo ambayo huenda wazazi walikosea huko nyuma,lakini kuna mengi sana waliyafanya na kujitoa kwa ajili ya vijana mpaka wakafikia hapo walipofikia

Huu ni mfano mdogo wa watoto ambao hawawajali wazazi wao,na wengine hufikia mbali zaidi kutokana na hadhi zao hapa mjini kuwakana kabisa kwakuwa hawafanani na status zao

Una faida gani wewe hapa duniani na mbinguni kama huwajali wazazi wako,wale tunaosoma vitabu vitakatifu tunafahamu Mola wetu mlezi anasisitiza sana juu ya kuwaangali na kuwatunza wazazi wawili,ikiwa muumba wetu anasisitiza hilo je wewe ni nani uyapuuze hayo

Uko radhi hapa mjini ujionyeshe kwa watu kwamba una fedha nyingi na kutoa ofa nyingi huku wazazi wako wanakosa chakula na mahitaji mengine,unakaa kwenye nyumba nzuri lakini wazazi wako wanakaa kwenye nyumba ya nyasi

Tambua kwamba wazazi wako ndio tiketi yako ya kupata kibali cha mola wako,watu wema wa zamani wakiondokewa na wazazi wao,husikitika sana kwakuwa milango ya kheri imepungua,kuna thawabu ambazo huwa unazipata kwa kuwatunza wazazi wako lakini wengi wetu hatuyazingatii hayo

Tubadilikeni ndugu zangu,bila wazazi wako kukulea na kukutunza usingefikia hapo ulipi leo,unaitwa mheshimiwa fulani au mtaalamu fulani au mzazi fulani kutokana na mchango wa malezi kutoka kwa wazazi wako

Ni hayo tu!
 
Inashangaza Sana mkuu.

Mzazi anabidi kupewa kila kitu , Kuhudumiwa , kutunzwa na kupewa pesa za kutosha.

Ni vile tu mtu mweusi ana ufahamu mdogo Sana.
Mimi nadhani kutaka mtoto amlee mzazi ndiyo ufahamu mdogo sana wa watu weusi.

Jukumu la mzazi ni kumlea mtoto na kumtafutia mali ya kuja kurithi.

Siyo kukaa tu kusubiri kulelewa na mtoto.
 
Mimi nadhani kutaka mtoto amlee mzazi ndiyo ufahamu mdogo sana wa watu weusi.

Jukumu la mzazi ni kumlea mtoto na kumtafutia mali ya kuja kurithi.

Siyo kukaa tu kusubiri kulelewa na mtoto.


Ufahamu mdogo ni pale upo na uwezo mzuri wa kiuchumi Ila mama yako au baba yako anapata shida that's bullshit Nigga.
 
Hapana, Ninamaanisha nikiwa serious sana, fikiria tu vizuri.

Ni nani anayetakiwa kumlea mwenzie kati ya mzazi na mtoto?
Unatambua hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha,je pale wazazi wako wanapokosa nguvu ya kujitafutia unataka nani awatunze?

Tuache kuwa na fikra na tamaduni za kimagharibi kutaka wazazi wetu wakatunzwe katika nyumba za wazee
 
Inashangaza Sana mkuu.

Mzazi anabidi kupewa kila kitu , Kuhudumiwa , kutunzwa na kupewa pesa za kutosha.

Ni vile tu mtu mweusi ana ufahamu mdogo Sana.
Mzazi ndiye anatakiwa kuachia watoto urithi. Waafrika na watu wengi duniani wameishi hivyo kwa miaka mingi sana. Hii ya kusaidia wazazi kimali imekuja juzi juzi tu.
 
Back
Top Bottom