Inakuwaje Mzazi Anaweza Lea Watoto Kadhaa Lakini Watoto hawawezi Kulea Mzazi Wao

Inakuwaje Mzazi Anaweza Lea Watoto Kadhaa Lakini Watoto hawawezi Kulea Mzazi Wao

Mtoto kumlea mzazi wake ni yeye aamue tu lakini hawajibiki moja kwa moja kumlea.
Halafu wazazi wenye mtazamo wa kuja kulelewa na watoto, mara nyingi huwa hawawajibiki ipasavyo kulea watoto wao.

Mzazi unaejua wajibu wako vizuri, huwezi kuwa na mtazamo wa kuja kulelewa na watoto.

Kwa sababu utajua fika ugumu wa kulea mtoto, na utajua kuwa hao watoto wako nao watakuwa na familia na watoto w kulea.

Badala ya kusubiri waje wakulee, utajitahidi kutafuta mali angalau watoto wako waje warithi, wapate support ya kuwarahisishia maisha yao na familia zao.
 
Nakubaliana na wewe juu ya hoja yako

Lakini

Kuna wengine wamepata malezi mazuri ila baada ya kuwa na ndoa zao basi kila kitu kinabadilika
Kiukweli kabisa mzazi ana wajibu wa kumlea mtoto.

Na mtoto akikua akioa na yeye ana wajibu wa kumlea mtoto wake.

Ukitaka mtoto amlee mzazi unaharibu order.

Mzazi anatakiwa kulea watoto huku akijiwekea akiba ya uzeeni.

Mtoto alee mtoto wake na mzazi wake na hapo hapo ajiwekee akiba ya uzeeni hapo ndiyo unaanza kualika ufisadi watu waibe pesa ili kulea wazazi, watoto, kujiwekea akiba.

Mzazi anayemtegemea mtoto wake amlee uzeeni, huyo mtoto akifa kabla ya mzazi itakuwaje hapo?

This happens quite a lot nowadays.
 
Tumia akili hata huyo mtoto atalea watoto wake kibao ...tumia akili jibu lipo umelitamka mwenyewe labda ungesema inakuwaje mzazi kalea watoto kibao ila hao watoto wanashindwa kulea watoto wao kibao.
View attachment 3188476

Nikiwa ndani ya mwendo kasi miezi kadhaa iliyopita,abiria mwenzangu anaongea na mtu kwenye simu kuhusiana na watoto ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao apate matibabu

Baada ya kukata simu yule bwana nikaendeleza mazungumzo yake kwakuwa yalinigusa sana,ndo akanipa kisa cha watoto takribani watano ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao kwa kutoa fedha zao

Bila aibu wanataka mzazi wao akishavuna mazao yake ayauze kisha ndio wakamtibie,tena cha kushangaza sio kwamba watoto wote wapo vibaya,baadhi yao wapo vizur kiuchumi,huyo first born yupo vizur lakini kichwani hakuna kitu

Kweli walisema waswahili kuzaa si kupata,hata kama kuna mambo ambayo huenda wazazi walikosea huko nyuma,lakini kuna mengi sana waliyafanya na kujitoa kwa ajili ya vijana mpaka wakafikia hapo walipofikia

Huu ni mfano mdogo wa watoto ambao hawawajali wazazi wao,na wengine hufikia mbali zaidi kutokana na hadhi zao hapa mjini kuwakana kabisa kwakuwa hawafanani na status zao

Una faida gani wewe hapa duniani na mbinguni kama huwajali wazazi wako,wale tunaosoma vitabu vitakatifu tunafahamu Mola wetu mlezi anasisitiza sana juu ya kuwaangali na kuwatunza wazazi wawili,ikiwa muumba wetu anasisitiza hilo je wewe ni nani uyapuuze hayo

Uko radhi hapa mjini ujionyeshe kwa watu kwamba una fedha nyingi na kutoa ofa nyingi huku wazazi wako wanakosa chakula na mahitaji mengine,unakaa kwenye nyumba nzuri lakini wazazi wako wanakaa kwenye nyumba ya nyasi

Tambua kwamba wazazi wako ndio tiketi yako ya kupata kibali cha mola wako,watu wema wa zamani wakiondokewa na wazazi wao,husikitika sana kwakuwa milango ya kheri imepungua,kuna thawabu ambazo huwa unazipata kwa kuwatunza wazazi wako lakini wengi wetu hatuyazingatii hayo

Tubadilikeni ndugu zangu,bila wazazi wako kukulea na kukutunza usingefikia hapo ulipi leo,unaitwa mheshimiwa fulani au mtaalamu fulani au mzazi fulani kutokana na mchango wa malezi kutoka kwa wazazi wako

Ni hayo tu!
 
Sasa tupo pamoja.

Mtoto aliyelelewa na kutunzwa kwa moyo mmoja na wazazi wake kisha akaja kuwatelekeza ukubwani mara nyingi (sio zote) huwa anakuwa anatawaliwa na mke wake.

Yaani anatunza sana ndugu wa mke kuliko ndugu zake na ikitokea amefilisika mke anamkimbia na ndugu wa mke pia wanamzimia simu.

KATAA NDOA.
VIpi kwa ambao hawajaoa wala kuolewa lakini wana wakataa wazazi,

Na kuna ile ( Hii ni kwa hawa vijana wa mjini mjini ambao bado huwezi kusema umri umeenda ) huwa hawapendi hata kushow off na wazazi wao kwavile wengine wamezeeka sana , au Laah wazazi wao ni masikini sana na mionekano yao anahisi labda hakustahili kuwa na wazazi kama hao,. Japo nadhani huu ni utoto wakikua wataacha.

Tuje kwa hawa wengine watu wazima lakini wamewatenga wazazi wao kiasi kwamba hadi majirani na watu wa karibu wanaingilia kati lakini wapi, hawa nao wanashida gani?
 
Mzazi ndiye anatakiwa kuachia watoto urithi. Waafrika na watu wengi duniani wameishi hivyo kwa miaka mingi sana. Hii ya kusaidia wazazi kimali imekuja juzi juzi tu.
Ni kweli hii ya mtoto kumtajirisha mzazi au kutwishwa wajibu wa mzazi wake imekuja na ile ya WAUMINI WA DINI KUWATAJIRISHA VIONGOZI WAO WA DINI IWE NI WANAO JIDAI UTUME AU UNABII AU UINJILISTI NK ,,,ni pakeji za kiseng3 kabisa ...ccm ni mafiiii
 
Wakuu waliotoa hoja hapo juu wako sahihi sana ya kwamba, Sio Majukumu ya mtoto kumlea mzazi, Ukizaa manake una means ya kulea hao watoto, pia mzazi jiandalie maisha yako ya uzeeni, Usitegemee watoto!
Mkuu uko sahihi,
But incase hukufanikiwa kujiandalia maisha yako mazuri na ulijitahidi kwa kila namna kuwaweka wanao mahali pazuri na wamekuwa,
kWahiyo huzistahili japo kidogo fadhila za wanao?🤔
 
Kiukweli kabisa mzazi ana wajibu wa kumlea mtoto.

Na mtoto akikua akioa na yeye ana wajibu wa kumlea mtoto wake.

Ukitaka mtoto amlee mzazi unaharibu order.

Mzazi anatakiwa kulea watoto huku akijiwekea akiba ya uzeeni.

Mtoto alee mtoto wake na mzazi wake na hapo hapo ajiwekee akiba ya uzeeni hapo ndiyo unaanza kualika ufisadi watu waibe pesa ili kulea wazazi, watoto, kujiwekea akiba.

Mzazi anayemtegemea mtoto wake amlee uzeeni, huyo mtoto akifa kabla ya mzazi itakuwaje hapo?

This happens quite a lot nowadays.
Una hoja katika hilo,,,lakini je kwa watoto mlio zaliwa wengi pamoja na kuwa na majukumu yenu ya kulea familia zenu,watashindwa kuchangia kidogo kidogo na kulea wazazi wao?

Lakini pili mazingira ya kiafrika tunayajua wazazi wengi wametulea kwa kutegemea kilimo cha mkono,je wangejiwekeza saa ngapi wakati hicho kidogo walichopata ndio walikitumia kutulea sisi

Ila ukizungumzia huko dunia ya kwanza mlipo nyinyi hoja yako itakuwa na mashiko
 
Kuna tukio kubwa walifanyiwa na hao wazazi na sasa it's a pay back time. Wanalipa kisasi..
So tunaconclude kwamba hakuna mwenye makosa, ni wazazi wanalipia karma zao kwa matendo kadha wa kadha waliyowafanyia watoto wao?

Em tujaribu kugeuza kioo, means kuanzia ukiwa mdogo hujawahi kuwakwaza wazazi wako kwa namna yoyote ile?,. Na kwanini uwe mzito kumsamehe mzazi aliyakua nawe yapo mengi ulimkwaza kwa kujua ama kutokujua na alipiga moyo konde kukukuza mpaka umefika ulipo?
 
Wao hawa wazazi wasiolelewa je walilea wazazi wao?
Baadhi ya watu wanataka kuleta huruma za kijinga humu. Mkuu, watu wanasema kwa sasa mimi ni cold heart sana. Yaani mimi wa mwaka 2019 na mimi huyu wa mwaka 2024 ni watu wawili tofauti kabisa.

Experience can turn a sheep into a wolf..
 
Tumia akili hata huyo mtoto atalea watoto wake kibao ...tumia akili jibu lipo umelitamka mwenyewe labda ungesema inakuwaje mzazi kalea watoto kibao ila hao watoto wanashindwa kulea watoto wao kibao.
Boss wangu,kichwa cha uzi kinajieleza wazi kwamba inakuwaje mzazi anaweza lea watoto wengi lkn watoto wanashindwa kulea mzazi wao,hatujatofautiana hapo
 
So tunaconclude kwamba hakuna mwenye makosa, ni wazazi wanalipia karma zao kwa matendo kadha wa kadha waliyowafanyia watoto wao?

Em tujaribu kugeuza kioo, means kuanzia ukiwa mdogo hujawahi kuwakwaza wazazi wako kwa namna yoyote ile?,. Na kwanini uwe mzito kumsamehe mzazi aliyakua nawe yapo mengi mlimkwaza kwa kujua ama kutokujua na alipiga moyo konde kukukuza mpaka umefika ulipo?
Katika suala la PESA YANGU mimi sinaga msalie mtume. Kwanza tambua hilo. Mtu anayecheza na pesa yangu, hata kama ni mzazi wangu, atageuka kuwa adui on the spot. Kwangu mimi wa kwanza Mungu, wa pili mimi mwenyewe, wa tatu, PESA/HELA YANGU alafu wengine ndio wanaofuata...
 
Katika suala la PESA YANGU mimi sinaga msalie mtume. Kwanza tambua hilo. Mtu anayecheza na pesa yangu, hata kama ni mzazi wangu, atageuka kuwa adui on the spot. Kwangu mimi wa kwanza Mungu, wa pili mimi mwenyewe, wa tatu, PESA/HELA YANGU alafu wengine ndio wanaofuata...
Una msimamo mkali sana,. Ila ni vizuri as long as unaishi kwa amani
 
ushakwisha dawa yako kama unataka kupona omba msamaha humu hadharani. La sivyo hata hayo masomo yako nitayakatisha.

Sipendi upuzi
Siwezi kuogopa jitu jehu kama wewe , Nina mambo mengi ya msingi ndio maana Nakuwa nakupuuza . Uwezo ninao wa kula sahani Moja na wewe jino kwa jino.

Usitarajie kamwe Mimi nilie kwa mods au nilie kwako nitake huruma hiko kitu never and I see you like a Scumbag , nimewatag mods sababu huwa nikilipa mashambulizi unakimbia polisi.
 
Back
Top Bottom