Inakuwaje Mzazi Anaweza Lea Watoto Kadhaa Lakini Watoto hawawezi Kulea Mzazi Wao

Muda mwingine wako sahihi.

Kuna mzazi hajahusika kivyovyote katika malezi yako, umejitesekea na kujipambania mwenyewe tu, huyo hata akikataliwa ni sawa.

Tunaopaswa kuwashangaa ni wanaokataa watoto wao.
Hili nalo linashangaza sana,,.
Means wanaokataa watoto ndio hao wazazi wanaopaswa kupuuzwa
 
Hapana, Ninamaanisha nikiwa serious sana, fikiria tu vizuri.

Ni nani anayetakiwa kumlea mwenzie kati ya mzazi na mtoto?
Ngoja waje kukutisha eti "utapata laana"

Watu wanazaa tu "out of ego and peer pressure" watoto 5 kisha wanawatelekeza, na watoto wakija kuwatelekeza wao, wanakimbilia kuwaita viongozi wa dini kukutisha eti utapata laana..
 
Muda mwingine wako sahihi.

Kuna mzazi hajahusika kivyovyote katika malezi yako, umejitesekea na kujipambania mwenyewe tu, huyo hata akikataliwa ni sawa.

Tunaopaswa kuwashangaa ni wanaokataa watoto wao.
Umejipambania baada ya kuwa mkubwa na nguvu zako si ndio

Vp ulipokuwa mchanga na mdogo?
 
Ufahamu mdogo ni pale upo na uwezo mzuri wa kiuchumi Ila mama yako au baba yako anapata shida that's bullshit Nigga.
Huwezi kumlazimisha mama yako au baba yako asipate shida, hayo ni maisha yao.

Ni sawa na kudhani kuwa unaweza kumfanya mtu mwingine awe tajiri. Kuwa tajiri au masikini ni maamuzi ya mtu binafsi.

Kudhani kuwa mtoto akiwa na uwezo wa kifedha basi ni lazima wazazi wake nao waishi kifahari ni bullshit.
 
View attachment 3188476

Nikiwa ndani ya mwendo kasi miezi kadhaa iliyopita,abiria mwenzangu anaongea na mtu kwenye simu kuhusiana na watoto ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao apate matibabu

Baada ya kukata simu yule bwana nikaendeleza mazungumzo yake kwakuwa yalinigusa sana,ndo akanipa kisa cha watoto takribani watano ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao kwa kutoa fedha zao

Bila aibu wanataka mzazi wao akishavuna mazao yake ayauze kisha ndio wakamtibie,tena cha kushangaza sio kwamba watoto wote wapo vibaya,baadhi yao wapo vizur kiuchumi,huyo first born yupo vizur lakini kichwani hakuna kitu

Kweli walisema waswahili kuzaa si kupata,hata kama kuna mambo ambayo huenda wazazi walikosea huko nyuma,lakini kuna mengi sana waliyafanya na kujitoa kwa ajili ya vijana mpaka wakafikia hapo walipofikia

Huu ni mfano mdogo wa watoto ambao hawawajali wazazi wao,na wengine hufikia mbali zaidi kutokana na hadhi zao hapa mjini kuwakana kabisa kwakuwa hawafanani na status zao

Una faida gani wewe hapa duniani na mbinguni kama huwajali wazazi wako,wale tunaosoma vitabu vitakatifu tunafahamu Mola wetu mlezi anasisitiza sana juu ya kuwaangali na kuwatunza wazazi wawili,ikiwa muumba wetu anasisitiza hilo je wewe ni nani uyapuuze hayo

Uko radhi hapa mjini ujionyeshe kwa watu kwamba una fedha nyingi na kutoa ofa nyingi huku wazazi wako wanakosa chakula na mahitaji mengine,unakaa kwenye nyumba nzuri lakini wazazi wako wanakaa kwenye nyumba ya nyasi

Tambua kwamba wazazi wako ndio tiketi yako ya kupata kibali cha mola wako,watu wema wa zamani wakiondokewa na wazazi wao,husikitika sana kwakuwa milango ya kheri imepungua,kuna thawabu ambazo huwa unazipata kwa kuwatunza wazazi wako lakini wengi wetu hatuyazingatii hayo

Tubadilikeni ndugu zangu,bila wazazi wako kukulea na kukutunza usingefikia hapo ulipi leo,unaitwa mheshimiwa fulani au mtaalamu fulani au mzazi fulani kutokana na mchango wa malezi kutoka kwa wazazi wako

Ni hayo tu!
Simply because it's not illegal for one to abandon his/her parents..
 
Hapo mara nyingi inakuwa mzazi hajawalea watoto vizuri.
 
Hawa ndio ambao inabidi wapuuzwe wakifika utu uzimani,
Mie nawashangaa wale ambao wamelelewa na wazazi wao vizuri tu lakini wakifika mahali huwa wanawakataa sijui shida huwaga nini
Labda kungekuwa na wazoefu watupe miongozo
Cc. Mjuni Lwambo
Sasa tupo pamoja.

Mtoto aliyelelewa na kutunzwa kwa moyo mmoja na wazazi wake kisha akaja kuwatelekeza ukubwani mara nyingi (sio zote) huwa anakuwa anatawaliwa na mke wake.

Yaani anatunza sana ndugu wa mke kuliko ndugu zake na ikitokea amefilisika mke anamkimbia na ndugu wa mke pia wanamzimia simu.

KATAA NDOA.
 
Hili ulilosema nalo huchangia sana vwatoto kuwasahau wazazi wao,akisha zama katika penzi la mke basi anamsahau hata mzazi wake
 
Back
Top Bottom