Inakuwaje Mzazi Anaweza Lea Watoto Kadhaa Lakini Watoto hawawezi Kulea Mzazi Wao

Haya ni matokeo hasi ya dini na umagharibi.
Dini zimepandikiza kwa waafrika dhana ya mtoto kuachana na wazazi wake na kufanya mambo kivyake, yeye na familia yake mpya.
Mambo hayakua hivi katika jamii nyingi za kiafrika. Ukiona, mke anakuja nyumbani, hakutenganishi na familia yako.
Tunaona wazungu hawajihusishi sana na wazazi wao, wao wana mifumo inayolea wazee. Sie hatuna na tunajifanya kufanya mambo kama wao.
Kiafrika tumekuwa na taratibu zetu za kulea wazee lakini siku hizi vijana wanataka kuendesha magari na kulipa subscriptions za Netflix na Hulu tu. Si kulea wazee.
Ukiongeza fact kwamba wengi tunaoa watu wa kutoka jamii tofauti, wake zetu hawajui tamaduni zetu, ugomvi kila mara unapotaka kusaidia wazazi wako, anataka naye a-level mizani usaidie kwao pia.
Nimeipenda hii
 
Una hoja katika hilo,,,lakini je kwa watoto mlio zaliwa wengi pamoja na kuwa na majukumu yenu ya kulea familia zenu,watashindwa kuchangia kidogo kidogo na kulea wazazi wao?

Lakini pili mazingira ya kiafrika tunayajua wazazi wengi wametulea kwa kutegemea kilimo cha mkono,je wangejiwekeza saa ngapi wakati hicho kidogo walichopata ndio walikitumia kutulea sisi

Ila ukizungumzia huko dunia ya kwanza mlipo nyinyi hoja yako itakuwa na mashiko
Hujaelewa hoja.

Kulea watoto ni suala la kifamilia. Ni suala la "tenda wema uende zako, usingoje shukurani".

Si biashara ya kuwekeza useme nawekeza kwa watoto wangu nawalea, wakikua na wao watarudisha fadhila watanilea. Hii ndiyo mentality ya Kiafrika sehemu nyingi. Ni mentality mbaya sana.

Watoto wana hiyari ya kuwachangia wazazi wao wakiweza, wasipoweza au kutaka napo ni sawa tu.

Sehemu ambayo watoto wanalazimika kulea watake wasitake ni kwa watoto wao, tena wadogo.

Mzazi bora anatakiwa kumuweka mbele mtoto wake. Sisemi kwamba mzazi asisaidiwe na watoto wake, mzazi mwenye mahusiano mazuri na watoto wake, aliyewalea vizuri, aliuewaandaa kuweza kumsaidia, ni nadra sana kuhitaji msaada asisaidiwe. Ila tuondokane na utamaduni wa kuweka obligation ya watoto kusaidia wazazi. Watoto wana obligation ya kulea watoto wao tayari.

Dunia imebadilika. Life expectancy imepanda, watu wanaishi muda nrefu sana siku hizi. Sasa kama mzazi hajajipanga yeye mwenyewe, mtoto naye ana mzigo wa kukea watoto wake, hapi hapo unamuongezea nzigo wa kulea wazazi, hapo ndipo mnapoalika wizi kazini, mtu mmoja anakuwa na mizigo mingi sana.

Watu wajipange kwa elimu, careers nzuri, biashara, kujiwekea mafao ya uzeeni, uwekezaji, etc.

Wasitegemee watoto.

Inawezekana kuna wazee wetu waliotegemea kilimo cha mkono wakawa na changamoto, hawa tunaweza kuwaangalia kama soecial case iliyotokea katika transition oeriod tulip9kuwa tunabadili mifumo, lakini kwendq mbele tuondokane na dhana hii ya kuzaa iki watoto waje kujusaidia uzeeni.

Kwa maisha ya sasa inawezekana kabisa kukatokea pattern ya watoto wengi kuanza kufa kwa madawa ya kulevya, pombe, kujiua, etc, halafu wazee wakaendelea kuishi mpaka miaka 90 na zaidi huko.

Sasa hapo watoto wakifa kabla ya wazazi, ma wqzazi wanategemea watito wawalee, nani atawalea?
 
Siwezi kuogopa jitu jehu kama wewe , Nina mambo mengi ya msingi ndio maana Nakuwa nakupuuza . Uwezo ninao wa kula sahani Moja na wewe jino kwa jino.

Usitarajie kamwe Mimi nilie kwa mods au nilie kwako nitake huruma hiko kitu never and I see you like a Scumbag , nimewatag mods sababu huwa nikilipa mashambulizi unakimbia polisi.
Sitakusamehe sasa kaa tayari. It's not revenge but punishment. Nataka kukuadhibu. Halafu ishu ya masomo nahuzunika sana vijana wa hovyo kama wewe siku hizi mlivyokuwa wapumbavu nakuchukulia ishu ya kusoma ni ya kuchezea. Ndo maana taaluma nyingi nchini zimekuwa utopolo kwasababu ya vijana kama nyie on your 20s hamna dira mustakabal na msaada wowote nchini. Kama wewe unajituma kusoma ili baadaye uibe hilo ndo lengo lako kuu. Kwa muktadha mtazamo huo lazima upigwe stop upelekwe kulima huko.
 
Boss wangu,kichwa cha uzi kinajieleza wazi kwamba inakuwaje mzazi anaweza lea watoto wengi lkn watoto wanashindwa kulea mzazi wao,hatujatofautiana hapo
Soma nilicho andika nimesema na huyo mtoto naye ataweza kulea watoto wake wengi
 
Kiukweli kabisa mzazi ana wajibu wa kumlea mtoto.

Na mtoto akikua akioa na yeye ana wajibu wa kumlea mtoto wake.

Ukitaka mtoto amlee mzazi unaharibu order.

Mzazi anatakiwa kulea watoto huku akijiwekea akiba ya uzeeni.

Mtoto alee mtoto wake na mzazi wake na hapo hapo ajiwekee akiba ya uzeeni hapo ndiyo unaanza kualika ufisadi watu waibe pesa ili kulea wazazi, watoto, kujiwekea akiba.

Mzazi anayemtegemea mtoto wake amlee uzeeni, huyo mtoto akifa kabla ya mzazi itakuwaje hapo?

This happens quite a lot nowadays.
Hapo mwishoni mkuu ndio tunaona watu wanazaa watoto wengi bila mpangilio, anakuambia wakifa wengine, wengine wabaki wa kumlea.
 
Hao watoto nao wanakuwa wanalea watoto wao.
Mkuu kuna wazazi wengine makatili kwa watoto wao utakuta huyo Mzazi alikua ana watesa hao vijana wakati wapo wadogo sana, Wazazi wa zamani wengi wao walikua hawana upendo kwa Watoto wao, Utakuta Mzazi ana uwezo lakini hawapi watoto chakula na utakuta huyo Mzazi anafanya kazi Serikali lakini ukienda kwake familia haipati milo mitatu, na Usiku Baba anarudi kalewa na kuwaletea vurugu familia mke na watoto, Wazazi wenye umri wa kuanzia Miaka 65 nakuendelea % 85 walitesa watoto wao kwa kuto wajali na waki huo wanaishi nao pamoja, yani bora Usimjali mtoto mkiwa mbali kuliko unaishi na familia halafu unawafanyia vitendo ya kinyama, Watoto wana tuna mabaya yote unayomfanyia Mama yao na wao.
Baadae wanakuja kulipa kwa kutokukuali ukiomba pesa kila mtu anasema hana.
 
View attachment 3188476

Nikiwa ndani ya mwendo kasi miezi kadhaa iliyopita,abiria mwenzangu anaongea na mtu kwenye simu kuhusiana na watoto ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao apate matibabu

Baada ya kukata simu yule bwana nikaendeleza mazungumzo yake kwakuwa yalinigusa sana,ndo akanipa kisa cha watoto takribani watano ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao kwa kutoa fedha zao

Bila aibu wanataka mzazi wao akishavuna mazao yake ayauze kisha ndio wakamtibie,tena cha kushangaza sio kwamba watoto wote wapo vibaya,baadhi yao wapo vizur kiuchumi,huyo first born yupo vizur lakini kichwani hakuna kitu

Kweli walisema waswahili kuzaa si kupata,hata kama kuna mambo ambayo huenda wazazi walikosea huko nyuma,lakini kuna mengi sana waliyafanya na kujitoa kwa ajili ya vijana mpaka wakafikia hapo walipofikia

Huu ni mfano mdogo wa watoto ambao hawawajali wazazi wao,na wengine hufikia mbali zaidi kutokana na hadhi zao hapa mjini kuwakana kabisa kwakuwa hawafanani na status zao

Una faida gani wewe hapa duniani na mbinguni kama huwajali wazazi wako,wale tunaosoma vitabu vitakatifu tunafahamu Mola wetu mlezi anasisitiza sana juu ya kuwaangali na kuwatunza wazazi wawili,ikiwa muumba wetu anasisitiza hilo je wewe ni nani uyapuuze hayo

Uko radhi hapa mjini ujionyeshe kwa watu kwamba una fedha nyingi na kutoa ofa nyingi huku wazazi wako wanakosa chakula na mahitaji mengine,unakaa kwenye nyumba nzuri lakini wazazi wako wanakaa kwenye nyumba ya nyasi

Tambua kwamba wazazi wako ndio tiketi yako ya kupata kibali cha mola wako,watu wema wa zamani wakiondokewa na wazazi wao,husikitika sana kwakuwa milango ya kheri imepungua,kuna thawabu ambazo huwa unazipata kwa kuwatunza wazazi wako lakini wengi wetu hatuyazingatii hayo

Tubadilikeni ndugu zangu,bila wazazi wako kukulea na kukutunza usingefikia hapo ulipi leo,unaitwa mheshimiwa fulani au mtaalamu fulani au mzazi fulani kutokana na mchango wa malezi kutoka kwa wazazi wako

Ni hayo tu!
Kwa sababu, hao watoto wake, kipindi anataka wamlee,watakuwa wanalea watoto wao, wajukuu zake, maaana hata wakati hawa wazazi wetu wanatulea, wazazi wao, bqbu nq Bibi setup, wali kuwa vijijini wakijitegemea, wakisubili kutumiwa sukari, Michele mwisho wa mwaka! Babu na Bibi zetu walikuja mjini, baada ya kuzeeka Sana, kufata matibabu, lakini wakafa baada yq muda mfupi!
Vitu vingine vipo wazi kabisa, umalize masomo, upate kazi, ujenge, au upange nyumba, uwalete wazazi wako uishi nao mjini, pamoja na mke na watoto wako, wanaoweza kufanya hv ni wachache tena hapo, unq miakq 45+mjini kugumu, kwa wengi mpaka una miaka 45+bado hujajipata kuweza kuwa na nyumba ukae na wazazi wako, mke na watoto, ukitaka uje ulelewe na watoto wako, wape zaidi yq elimu, wape kianzio cha maisha, kipato, au Jenga maisha na miundombinu itakayokuwezesha kuishi bila kutegemea msaada wa kifedha kutoka kwa watoto
 
Hapo mwishoni mkuu ndio tunaona watu wanazaa watoto wengi bila mpangilio, anakuambia wakifa wengine, wengine wabaki wa kumlea.
Habari za kuzaa watoto wengi ni matokeo ya agrarian societies zilizokuwa zinafanyisha kazi za kulimisha watoto. Kimsingi watoto wanatumika kwa child labor.

Siku hizi dunia ya elimu na teknolojia watu wanazaa watoto wachache zaidi ili kuweza kuwaelimisha na kuwapa nafasi nzuri ya maisha bora.
 
Ni mtazamo tu wa waafrica walio wengi hasa masikini,lakini kimsingi kwa familia zinazojimudu mzazi hawezi kumtegemea mtoto..wengi walishajipanga huwezikuta wanasumbua uzeeni..
Ni umasikini tu ndio unapelekea mzazi sijui kutoa laana kisa eti hasaidiwi..
 
View attachment 3188476

Nikiwa ndani ya mwendo kasi miezi kadhaa iliyopita,abiria mwenzangu anaongea na mtu kwenye simu kuhusiana na watoto ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao apate matibabu

Baada ya kukata simu yule bwana nikaendeleza mazungumzo yake kwakuwa yalinigusa sana,ndo akanipa kisa cha watoto takribani watano ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao kwa kutoa fedha zao

Bila aibu wanataka mzazi wao akishavuna mazao yake ayauze kisha ndio wakamtibie,tena cha kushangaza sio kwamba watoto wote wapo vibaya,baadhi yao wapo vizur kiuchumi,huyo first born yupo vizur lakini kichwani hakuna kitu

Kweli walisema waswahili kuzaa si kupata,hata kama kuna mambo ambayo huenda wazazi walikosea huko nyuma,lakini kuna mengi sana waliyafanya na kujitoa kwa ajili ya vijana mpaka wakafikia hapo walipofikia

Huu ni mfano mdogo wa watoto ambao hawawajali wazazi wao,na wengine hufikia mbali zaidi kutokana na hadhi zao hapa mjini kuwakana kabisa kwakuwa hawafanani na status zao

Una faida gani wewe hapa duniani na mbinguni kama huwajali wazazi wako,wale tunaosoma vitabu vitakatifu tunafahamu Mola wetu mlezi anasisitiza sana juu ya kuwaangali na kuwatunza wazazi wawili,ikiwa muumba wetu anasisitiza hilo je wewe ni nani uyapuuze hayo

Uko radhi hapa mjini ujionyeshe kwa watu kwamba una fedha nyingi na kutoa ofa nyingi huku wazazi wako wanakosa chakula na mahitaji mengine,unakaa kwenye nyumba nzuri lakini wazazi wako wanakaa kwenye nyumba ya nyasi

Tambua kwamba wazazi wako ndio tiketi yako ya kupata kibali cha mola wako,watu wema wa zamani wakiondokewa na wazazi wao,husikitika sana kwakuwa milango ya kheri imepungua,kuna thawabu ambazo huwa unazipata kwa kuwatunza wazazi wako lakini wengi wetu hatuyazingatii hayo

Tubadilikeni ndugu zangu,bila wazazi wako kukulea na kukutunza usingefikia hapo ulipi leo,unaitwa mheshimiwa fulani au mtaalamu fulani au mzazi fulani kutokana na mchango wa malezi kutoka kwa wazazi wako

Ni hayo tu!
Sio kazi yao na hawalazimiki kufanya hivyo, ila mzazi ana wajibu kisheria juu ya malezi na ustawi wa watoto wake na kutofanya hivyo huweza kupelekea kushurutishwa kwa mujibu wa sheria kutekeleza wajibu huo.
 
So tunaconclude kwamba hakuna mwenye makosa, ni wazazi wanalipia karma zao kwa matendo kadha wa kadha waliyowafanyia watoto wao?

Em tujaribu kugeuza kioo, means kuanzia ukiwa mdogo hujawahi kuwakwaza wazazi wako kwa namna yoyote ile?,. Na kwanini uwe mzito kumsamehe mzazi aliyakua nawe yapo mengi ulimkwaza kwa kujua ama kutokujua na alipiga moyo konde kukukuza mpaka umefika ulipo?
Hiyo kitu ni rahisi sana kusema ila yakikukuta ndo utajua,,,,
Sasa mfano umepata ajira halafu ndo kipindi mzee maisha yamembonda kisawasawa, unaamua kubeba majukumu ya familia, mbaya zaidi ukute mzee aliuza na nyumba mmeenda kupanga nyumba nzima.
Baada ya muda naye anapata kibarua chake kwahiyo mnaisukuma familia lakini mchango mkubwa ni wewe.
Baada ya muda unaamua kuuza viwanja vyako na kuchukua mikopo kupitia mshahara na pesa unawakabidhi wajenge nyumba na waanze biashara...
Mikopo uliyokuwa ukichukua kipindi chote hicho inakuzidi maana mshahara hautoshi kuendesha maisha unakimbia kazi ya Serikalini unaingia kutafuta hela mtaani..
Then ghafla unagundua wamechukua mikopo zaidi ya mitatu kupitia hii nyumba na kilichofanyika cha maana huambiwi na duka limekufa...
Na tokea ulivyoachia ujenzi wa nyumba ndo ilivyo mpaka leo, lakini wamekuwa wakipata hela lakini hamna chochote walichofanya kwenye nyumba,, kwamba ukute mzee yuko busy kujaza duka na kulipa madeni ya mama wa kambo ambaye yuko busy na vikundi visivyozalisha vya akina mama..
Na hivyo vyote vitokee kwenye interval ya miaka kama 15,, sasa nawe umeshakuwa mtu mzima una kama 40 kwa miaka na una familia yako inakuhitaji...
Kwahiyo utaendelea kuwabeba au uendelee na maisha yako?
 
Bila aibu wanataka mzazi wao akishavuna mazao yake ayauze kisha ndio wakamtibie,tena cha kushangaza sio kwamba watoto wote wapo vibaya,baadhi yao wapo vizur kiuchumi,huyo first born yupo vizur lakini kichwani hakuna kitu
Kiukweli kabisa bila kupindisha maneno kuna Wazazi wengine walifanya kazi ya kuzaa tu watotp wamejilea.

Hasa first born inakuta yeye ndiye kalea wadogo zake.
 
View attachment 3188476

Nikiwa ndani ya mwendo kasi miezi kadhaa iliyopita,abiria mwenzangu anaongea na mtu kwenye simu kuhusiana na watoto ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao apate matibabu

Baada ya kukata simu yule bwana nikaendeleza mazungumzo yake kwakuwa yalinigusa sana,ndo akanipa kisa cha watoto takribani watano ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao kwa kutoa fedha zao

Bila aibu wanataka mzazi wao akishavuna mazao yake ayauze kisha ndio wakamtibie,tena cha kushangaza sio kwamba watoto wote wapo vibaya,baadhi yao wapo vizur kiuchumi,huyo first born yupo vizur lakini kichwani hakuna kitu

Kweli walisema waswahili kuzaa si kupata,hata kama kuna mambo ambayo huenda wazazi walikosea huko nyuma,lakini kuna mengi sana waliyafanya na kujitoa kwa ajili ya vijana mpaka wakafikia hapo walipofikia

Huu ni mfano mdogo wa watoto ambao hawawajali wazazi wao,na wengine hufikia mbali zaidi kutokana na hadhi zao hapa mjini kuwakana kabisa kwakuwa hawafanani na status zao

Una faida gani wewe hapa duniani na mbinguni kama huwajali wazazi wako,wale tunaosoma vitabu vitakatifu tunafahamu Mola wetu mlezi anasisitiza sana juu ya kuwaangali na kuwatunza wazazi wawili,ikiwa muumba wetu anasisitiza hilo je wewe ni nani uyapuuze hayo

Uko radhi hapa mjini ujionyeshe kwa watu kwamba una fedha nyingi na kutoa ofa nyingi huku wazazi wako wanakosa chakula na mahitaji mengine,unakaa kwenye nyumba nzuri lakini wazazi wako wanakaa kwenye nyumba ya nyasi

Tambua kwamba wazazi wako ndio tiketi yako ya kupata kibali cha mola wako,watu wema wa zamani wakiondokewa na wazazi wao,husikitika sana kwakuwa milango ya kheri imepungua,kuna thawabu ambazo huwa unazipata kwa kuwatunza wazazi wako lakini wengi wetu hatuyazingatii hayo

Tubadilikeni ndugu zangu,bila wazazi wako kukulea na kukutunza usingefikia hapo ulipi leo,unaitwa mheshimiwa fulani au mtaalamu fulani au mzazi fulani kutokana na mchango wa malezi kutoka kwa wazazi wako

Ni hayo tu!
mtoto umleavyo ndivyo akuavyo 🐒
 
Hiyo kitu ni rahisi sana kusema ila yakikukuta ndo utajua,,,,
Sasa mfano umepata ajira halafu ndo kipindi mzee maisha yamembonda kisawasawa, unaamua kubeba majukumu ya familia, mbaya zaidi ukute mzee aliuza na nyumba mmeenda kupanga nyumba nzima.
Baada ya muda naye anapata kibarua chake kwahiyo mnaisukuma familia lakini mchango mkubwa ni wewe.
Baada ya muda unaamua kuuza viwanja vyako na kuchukua mikopo kupitia mshahara na pesa unawakabidhi wajenge nyumba na waanze biashara...
Mikopo uliyokuwa ukichukua kipindi chote hicho inakuzidi maana mshahara hautoshi kuendesha maisha unakimbia kazi ya Serikalini unaingia kutafuta hela mtaani..
Then ghafla unagundua wamechukua mikopo zaidi ya mitatu kupitia hii nyumba na kilichofanyika cha maana huambiwi na duka limekufa...
Na tokea ulivyoachia ujenzi wa nyumba ndo ilivyo mpaka leo, lakini wamekuwa wakipata hela lakini hamna chochote walichofanya kwenye nyumba,, kwamba ukute mzee yuko busy kujaza duka na kulipa madeni ya mama wa kambo ambaye yuko busy na vikundi visivyozalisha vya akina mama..
Na hivyo vyote vitokee kwenye interval ya miaka kama 15,, sasa nawe umeshakuwa mtu mzima una kama 40 kwa miaka na una familia yako inakuhitaji...
Kwahiyo utaendelea kuwabeba au uendelee na maisha yako?
Duuuh, i feel sorry for you my friend.
In your case, hao ndio wazazi wanaopaswa kupuuzwa🤝
Hope you find peace 🙏
 
Ndiomana inashauriwa msigusanishe vikojoleo km hamna uwezo wa kulea hao watoto mnaowaleta.!!

Kuna watu maisha magumu wanazaliana km panya halafu mibishi ukishauri wazee kwa mpango, wanajipa matumaini watazaa Nyerere mwisho wa siku wanatuletea watu wa ajabu wanakuja kubaka na kulawiti watoto.!!
 
Hiyo kitu ni rahisi sana kusema ila yakikukuta ndo utajua,,,,
Sasa mfano umepata ajira halafu ndo kipindi mzee maisha yamembonda kisawasawa, unaamua kubeba majukumu ya familia, mbaya zaidi ukute mzee aliuza na nyumba mmeenda kupanga nyumba nzima.
Baada ya muda naye anapata kibarua chake kwahiyo mnaisukuma familia lakini mchango mkubwa ni wewe.
Baada ya muda unaamua kuuza viwanja vyako na kuchukua mikopo kupitia mshahara na pesa unawakabidhi wajenge nyumba na waanze biashara...
Mikopo uliyokuwa ukichukua kipindi chote hicho inakuzidi maana mshahara hautoshi kuendesha maisha unakimbia kazi ya Serikalini unaingia kutafuta hela mtaani..
Then ghafla unagundua wamechukua mikopo zaidi ya mitatu kupitia hii nyumba na kilichofanyika cha maana huambiwi na duka limekufa...
Na tokea ulivyoachia ujenzi wa nyumba ndo ilivyo mpaka leo, lakini wamekuwa wakipata hela lakini hamna chochote walichofanya kwenye nyumba,, kwamba ukute mzee yuko busy kujaza duka na kulipa madeni ya mama wa kambo ambaye yuko busy na vikundi visivyozalisha vya akina mama..
Na hivyo vyote vitokee kwenye interval ya miaka kama 15,, sasa nawe umeshakuwa mtu mzima una kama 40 kwa miaka na una familia yako inakuhitaji...
Kwahiyo utaendelea kuwabeba au uendelee na maisha yako?
Uko sahihi.....hawa watoto waliozalowa wanakuta kwao kuna nafuu hawatakuelewa
 
Back
Top Bottom