Inakuwaje Mzazi Anaweza Lea Watoto Kadhaa Lakini Watoto hawawezi Kulea Mzazi Wao

Inakuwaje Mzazi Anaweza Lea Watoto Kadhaa Lakini Watoto hawawezi Kulea Mzazi Wao

Bora ningekuwa nimejizaa.

Lakini nimezaliwa, halafu walionizaa wanataka niwahudumie. Nani aliyewaambia kwamba ninataka wanizae halafu niwahudumie?

Inamaana walikuwa wanaleta ka'chuma ulete' ili niwe natafuta mali kuwahudumia?
Tuko pamoja hao wazazi hatujawatumia barua watuzae ni shobo zao na kutulea ni jukumu lao..! Namuhudumia mzazi nikijisikia sio jukumu langu ni la wazazi wake 😹😹
 
Wazazi wa karne hii acheni na mambo ya wadada wa kazi watoto wakifika 11+ years...
Watoto wa umri huo inabidi wajifulie, wasafishe nyumba na wapike angalau hata mara 4 kwa wiki chakula cha usiku. Na kila siku usiku waoshe vyombo na kusafisha jiko kabla ya kulala.Weekend mama unaingia mzigoni mapishi na katikati ya wiki mnaweza order nje chakula kitamu.

Wakizoea kujitunza na kutunza familia toka wadogo wakikua wala hawatohitaji maelekezo itakua ndani yao and watajitunza wao vizuri wakianza kujitegemea, hawawezi sahau nyumbani na hata wakiwa na familia hawatohangaika
 
Tupo kwenye kizazi cha watoto wabinafsi na much know.
Hakuna feeling mbaya kwangu binafsi kama kushindwa kumuhudumia mzazi pale anapohitaji.

It feels so good and proud kumspoil mzazi kwa level yako
Mzazi alieshindwa kutafuta mali kwa uzembe tu na kuoa hovyo mamwanamke nyumba ndogo hadi akazeeka masikini, unajifeelije proud kumsaidia?

Unatakiwa usikitike sana.
 
Ndiomana inashauriwa msigusanishe vikojoleo km hamna uwezo wa kulea hao watoto mnaowaleta.!!

Kuna watu maisha magumu wanazaliana km panya halafu mibishi ukishauri wazee kwa mpango, wanajipa matumaini watazaa Nyerere mwisho wa siku wanatuletea watu wa ajabu wanakuja kubaka na kulawiti watoto.!!
Yaani ni shida watoto wameishia kuwa malaya wa kike, wakiume wvuta bangi na madawa na mbaya zaidia wanahamia kwenye ushoga.

Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kula bila kushiba. Ni mateso sana.
 
Hahahahaaa, eti watazaa Nyerere.

Kuzaa sana ni kuendeleza umasikini tu, unakosa muda wa kutafuta mali unakalia kuzaa zaa tu kama kenge!

Pumbafu kabisa.
 
Mzazi anawajibika kumlea mtoto aliye mzaa na kuhakikisha mtoto wake anawalea watoto wake, watoto sio mtaji ndugu tuache kumwaga mwaga hovyo
 
Hilo ni dogo kuna nyumba moja waliamua kukaa wote vyumba ambavyo Baba yao angejipatia kodi Kwa ajili ya maslah yake
 
View attachment 3188476

Nikiwa ndani ya mwendo kasi miezi kadhaa iliyopita,abiria mwenzangu anaongea na mtu kwenye simu kuhusiana na watoto ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao apate matibabu

Baada ya kukata simu yule bwana nikaendeleza mazungumzo yake kwakuwa yalinigusa sana,ndo akanipa kisa cha watoto takribani watano ambao wameshindwa kumhudumia mzazi wao kwa kutoa fedha zao

Bila aibu wanataka mzazi wao akishavuna mazao yake ayauze kisha ndio wakamtibie,tena cha kushangaza sio kwamba watoto wote wapo vibaya,baadhi yao wapo vizur kiuchumi,huyo first born yupo vizur lakini kichwani hakuna kitu

Kweli walisema waswahili kuzaa si kupata,hata kama kuna mambo ambayo huenda wazazi walikosea huko nyuma,lakini kuna mengi sana waliyafanya na kujitoa kwa ajili ya vijana mpaka wakafikia hapo walipofikia

Huu ni mfano mdogo wa watoto ambao hawawajali wazazi wao,na wengine hufikia mbali zaidi kutokana na hadhi zao hapa mjini kuwakana kabisa kwakuwa hawafanani na status zao

Una faida gani wewe hapa duniani na mbinguni kama huwajali wazazi wako,wale tunaosoma vitabu vitakatifu tunafahamu Mola wetu mlezi anasisitiza sana juu ya kuwaangali na kuwatunza wazazi wawili,ikiwa muumba wetu anasisitiza hilo je wewe ni nani uyapuuze hayo

Uko radhi hapa mjini ujionyeshe kwa watu kwamba una fedha nyingi na kutoa ofa nyingi huku wazazi wako wanakosa chakula na mahitaji mengine,unakaa kwenye nyumba nzuri lakini wazazi wako wanakaa kwenye nyumba ya nyasi

Tambua kwamba wazazi wako ndio tiketi yako ya kupata kibali cha mola wako,watu wema wa zamani wakiondokewa na wazazi wao,husikitika sana kwakuwa milango ya kheri imepungua,kuna thawabu ambazo huwa unazipata kwa kuwatunza wazazi wako lakini wengi wetu hatuyazingatii hayo

Tubadilikeni ndugu zangu,bila wazazi wako kukulea na kukutunza usingefikia hapo ulipi leo,unaitwa mheshimiwa fulani au mtaalamu fulani au mzazi fulani kutokana na mchango wa malezi kutoka kwa wazazi wako

Ni hayo tu!
Nikwasababu watoto na wao wanakuwa na watoto wao.

Mzazi usitegemee sana kulelewa na watoto hasa iwapo haukujipanga. Aliyenacho anaongezewa kwasababu ukiwa na kitu, hautaonekana mzigo kwa watu.

Mfano rahisi angalia mlevi mwenye pesa akifika baa kila mtu anamchangamkia na kutaka amnunulie kinywaji. Lakini nenda wewe hohehahe uone, kila meza ukifika wanataka upewe konyagi ili ulewe haraka uondke
 
Yaani ni shida watoto wameishia kuwa malaya wa kike, wakiume wvuta bangi na madawa na mbaya zaidia wanahamia kwenye ushoga.

Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kula bila kushiba. Ni mateso sana.
Yani ni muendelezo wa mateso na nchi yetu sasa veggies (CCM) hata hawajali kukomboa umaskini kwa wananchi wao zaidi ya kushibisha mitumbo yao na kupokezana vijiti na watoto wao wazidi kutunyonya.!!
 
Ni huzuni sana Mungu awasamehe wote wasio wajali wazazi wao ingali wapo hai

Kuna wanaowish kupata nafasi hiyo ila Muda uliwawahi
Huwa tunajisahau tu.....pale tunapokata UNO tuwe na kumbukumbu kuwa huyu atakayetoka tusimtegemee huko mbeleni...... atakuwa na maisha yake.
 
Hapo ni suala la malezi tu ukilea watoto wako vizuri kwa upendo na hekima wala hutahitaji kuomba msaada wakusaidie wao wenyewe watajitoa. Wakati mwingine tatizo linaanzia kwa wazazi wenyewe hawakua na upendo wala hekima kwa watoto wao na hayo ndio malipo yake, upendo unajengwa ndugu zangu baina ya mtu na mtu na sio kwa sababu wewe ni mzazi basi watoto watakupenda tu No, utakuta mzazi hashindi nyumbani akitoka kazini anapitia bar kurudi nyumbani saa 6 usiku na siku akishinda nyumbani ni kulala tu siku nzima hata muda wa story na watoto wake hana, muda wa kula baba uso wa mbuzi hakuna kuongea kama waswahili wanavyodai wakati kitaalamu muda wa kula ndio muda mzuri wa kuongea na kufurahi kama familia.
 
Babu yangu alikuwa na watoto arobaini na kitu, yaani 40's hii hii. Wote wamelelewa bila shida yoyote, Kila mtoto alikua na kusoma vizuri, walikula na kusaza kabisa. Babu alikuwa mjanja sana, elimu nayo ilimsaidia, kwasababu yeye ndo kiongozi wa ukoo basi Kila mwaka lazima ukoo ukutane. Kwahili tunamshukuru Kwa kusaidia kutulelea baba zetu na ukoo mzima tuko imara sana. Sasa hivi mambo ni mengi.
 
Wazazi wa karne hii acheni na mambo ya wadada wa kazi watoto wakifika 11+ years...
Watoto wa umri huo inabidi wajifulie, wasafishe nyumba na wapike angalau hata mara 4 kwa wiki chakula cha usiku. Na kila siku usiku waoshe vyombo na kusafisha jiko kabla ya kulala.Weekend mama unaingia mzigoni mapishi na katikati ya wiki mnaweza order nje chakula kitamu.

Wakizoea kujitunza na kutunza familia toka wadogo wakikua wala hawatohitaji maelekezo itakua ndani yao and watajitunza wao vizuri wakianza kujitegemea, hawawezi sahau nyumbani na hata wakiwa na familia hawatohangaika
Nimeipenda hii
 
Hapo ni suala la malezi tu ukilea watoto wako vizuri kwa upendo na hekima wala hutahitaji kuomba msaada wakusaidie wao wenyewe watajitoa. Wakati mwingine tatizo linaanzia kwa wazazi wenyewe hawakua na upendo wala hekima kwa watoto wao na hayo ndio malipo yake, upendo unajengwa ndugu zangu baina ya mtu na mtu na sio kwa sababu wewe ni mzazi basi watoto watakupenda tu No, utakuta mzazi hashindi nyumbani akitoka kazini anapitia bar kurudi nyumbani saa 6 usiku na siku akishinda nyumbani ni kulala tu siku nzima hata muda wa story na watoto wake hana, muda wa kula baba uso wa mbuzi hakuna kuongea kama waswahili wanavyodai wakati kitaalamu muda wa kula ndio muda mzuri wa kuongea na kufurahi kama familia.
Nimeipenda hii
 
Babu yangu alikuwa na watoto arobaini na kitu, yaani 40's hii hii. Wote wamelelewa bila shida yoyote, Kila mtoto alikua na kusoma vizuri, walikula na kusaza kabisa. Babu alikuwa mjanja sana, elimu nayo ilimsaidia, kwasababu yeye ndo kiongozi wa ukoo basi Kila mwaka lazima ukoo ukutane. Kwahili tunamshukuru Kwa kusaidia kutulelea baba zetu na ukoo mzima tuko imara sana. Sasa hivi mambo ni mengi.
Huyo mwamba watoto 40!
 
Back
Top Bottom