NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Hii nchi kwangu inanishangaza sana, Ni ka nchi kadogo lakini manchi mengi makubwa yaliyodhamiria kuifuta kwenye rmani ya dunia hayajaweza mpaka leo. Ni mwendo wa kupigana, Ni sawa na Sungura na Tembo wanapigana kitu ambacho ni kama mazingaombwe.
Pia nimesoma historia kadhaa kuona kwamba nchi ndogo kama Israel ilizikalisha nchi kama sita hivi kubwa za kiarabu kwenye vita iliyochukua siku chache sana, Hii inawezekanaje?