Inamaanisha nini kufuatilia bunge la Kenya zaidi kuliko bunge letu tukufu?

Bongo hatuna Bunge ni Bonge la CCM
 
Futa neno tukufu aisee
 
Watu wanafatilia vitu vyenya maana
 
Ni kwa sa Ni kwa sababu tangu November 2020 hatuna Bunge bali ni mkusanyiko wa wahuni wa CCM.
 
Bunge letu la nchi ya kusadikika kinacholiondolea mvuto ni habari ya kumsifia tuuuuuuuu Raisi wa nchi ya kusadikika , mbunge anasimama na kutumia dk12 akimsifia Raisi kuwa ameleta maziwa, mvua, upepo ,tufani ya maendeleo kuliko awamu zote Za Marais wa nchi ya kusadikika walitangulia kutawala ,pia bunge lote linawaka moto kwa kukung'uta makofi ya pongezi ,kwa kila sifa anayomwagiwa halafu hoja ya msingi mbunge anaunga mkono kwa dk2 bila kuchangia chochote hoja yoyote,Mambo haya yanachosha sana
 
Uzito wa mjadala unachangia pia, japokuwa maagizo yanatoka juu na spika pamoja na makamu wake walishaamua kuchagua upande hakuna tofauti sana na wanasesere waliopo hapo mjengoni Dodoma ambao huelekezwa na wakuu wa vyama vyao namna ya kupiga kura kwenye miswada yenye utata.
 
Kwa kweli huwezi kufuatilia Bunge la Chama kimoja ambao wao waliingia bila kuchaguliwa na wananchi kwenye sanduku la kura!
Bunge la Tanzania ni lile la (9 na 10) liliongozwa na marehemu Samwel Sita na Anna Makinda! Bunge lililokuwepo chini ya Utawala wa awamu ya nne (Mheshimiwa J.M.Kikwete)
 
Kwa kweli huwezi kufuatilia Bunge la Chama kimoja ambao Wabunge waliingia bila kuchaguliwa na wananchi kwenye sanduku la kura!
Bunge la Tanzania ni lile la (9 na 10) liliongozwa na marehemu Samwel Sita na Anna Makinda! Wakati wa Utawala wa awamu ya nne (Mheshimiwa J.M.Kikwete)
 
Watu wanapenda drama.

Bunge letu halina drama.

Bunge la Kenya mara wabunge wanataka kupigwa na wananchi, nara Deputy President anataka kutolewa.

Lazima wabongo wafuatilie huku wakisema "Lini na sisi tutapata chachandu kama hizi, bunge ketu limepooza sana".
 
Duuu Mimi sijaona mtanzania anayefuatiliwa bunge la Kenya dadayangu wewe umekutana nao wapi na sample space ya tafiti yako ni kiasi gani?
 
Usijitoe Akili Unapoona Ukweli Wa Kenya
 
Hivi kabla ya 2018 wakati wabunge wa CHADEMA walipokuwa wengi bungeni bunge lilikuwa na drama?
 
Hivi mnajua kama Tz bunge linaendelea, tena kuna vikao vya Kamati za Bunge. Lakini watu hawana time
 
Kwani sisi tuna bunge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…