Inamaanisha nini kufuatilia bunge la Kenya zaidi kuliko bunge letu tukufu?

Wezi wa kura watukufu!
 
Utukufu wa bunge unaendana na matendo ya bunge husika
 
Siye tuna bunge basi? Jengo zuri limejaza vilaza na chawa
 
Mkuu hauoni kama kunakitu kinafanyika kwetu hakiwezi kufanyika? tunakuwa tumechoka na wanagapia wanasema ndio mara wote ndioooooo na wanagapi wanapinga kimya, hizo ni moja ya sababu zinazotufanya tufwatilie Bunge la wenzetu maana kuna utendaji ambao kwetu ni vigumu kabisa kuja kutokea,maana katiba zetu zina tofauti kubwa sana, twende tu mpaka tutakapo fikia.
 
Watanzania kwa umbea hawajambo. Kufuatilia mambo ya watu hawajambo, ila sasa ya kwao ahh, mabadiliko kwao ahh
 
Mara mbinge anaenaenda kavaa suruali ina damu damu sehemu za siri ili kuombe serikali itazamie kwa upya issue ya kodi za pedi. Yaani kila wakati kuna jambo jipya.
 
_
Imekuwa ni mazoea mtu kudharau chako na kuthamini cha mwenzio!.
P
 
unasemea bunge lipi mkuu, hili ambalo kwenye finance bill liliipitisha licha ya kelele za wananchi na baadaye Rais akaipiga chini bill hiyo?

unasema ni zuri kwa kwa sababu ya impeachment ya Gachagua ambayo iko orchestrated na Rais Mwenyewe?

Watanzania tunatabia ya kujidharau sana.
 
Ukweli nikwamba hakuna kitu kamili, Bunge la Kenya ni tamu tusidanganyane.
 
nadhani Africa Mashariki nzima walikua wanafuatilia bunge la Kenya kuona jinsi ambavyo ubovu wa katiba yao wenyewe unavyowasulubisha wao wenyewe 🐒
 
sasa hoja ya kufuatiliwa kwa bunge la Kenya na huyo mdudu vinahusiana nini gentleman?


au,
wewe unatofautiana nini na wale wananchi wa kenya ambao walialikwa kwenye public participation ili kutoa maoni yao kwamba RigGy abanduliwe unaibu rais ama asibanduliwa..

wao wakawa wanachant Ruto must go? 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…