Inasemekana watu wengi wenye hii alama kwenye sikio wana hatma ya kuwa matajiri

Inasemekana watu wengi wenye hii alama kwenye sikio wana hatma ya kuwa matajiri

Stability

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2020
Posts
822
Reaction score
2,966
Screenshot_20250907-155807.png
 
Nikama naelekea kushawishika hivii , niko nayo na nikiwa mtoto nilikuwa nachekwa sana kuwa nimetoboa sikio kitu ambacho kilipelekea hadi nikalalamike kwa Mama kuwa nikwanini wanitoboe sikio wakati mimi ni mwanaume , Mama aliniambia usikubali kuwasikiliza watu kwenye maisha yako utateseka sana ,hakuna sikio lililotobolewa na zaidi niichukulie hiyo kama alama muhimu ninayofaa kujivunia nayo.

Of course sikumuelewa na pengine hata yeye hakuwa amemaanisha kwa tafasiri ya mleta mada lakini niliipokea kauli ya Mama kwa uzito na hata leo naweza kusema ninacho cha kujivunia ,japo siwezi sema moja kwa moja pengine sababu ya mafanikio yangu yametokana na hiyo alama (maana kati ya watu waliyobahatika kupitia msoto namimi nimo🤣)
 
Wenye hicho kitobo huwa watu wakorofi,Sugu,wapole lakini ukianzisha ugomvi wao wanamaliza kwa kukupa kichapo.

Huwa wenye bahati ya kupendwa sana lakini wana attitude flani unaweza kuona wanajiona ila sio hivyo. Familia na majirani hata watu wasio wajua huwapenda na kuwapa heshima sana.

Pia ukibahatika kuwa rafiki yake utakuwa rafiki wake wa kweli hana unafiki lakini elewe kwenye neno unafiki(yaani hata uwe rafiki yake ukiongopa anakupa ukweli papohapo)

Wazee wao huwapenda sana huanza kuwawekezea kutokea utotoni mwao hii ndio sababu mojawapo kuwepo na mafanikio kwenye maisha yao.
 
Back
Top Bottom