gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,312
- 3,345
Salaam wanajamvi,
Juzi kulikuwa na mkutano ulioitishwa na wahariri wa vyombo vya habari mkoani Iringa ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mh Makamu wa Rais.
Mkutano huu dhima yake mahususi wahariri walilenga kumpatia Mh Makamu wa Rais taarifa juu ya kile walichobaini nini chanzo cha kukauka kwa mto Ruaha mkuu ambapo yapata siku 120 sasa hautiririshi maji kabisa.
Kwa wasiofahamu mto Ruaha mkuu unachangia 25% ya maji yanayotarajiwa kutumika kwenye bwawa la Mwl Nyerere. Pia mto huu pia ndio chanzo kikuu cha Maji kwenye bwawa la Mtera ukisaidiana na mto Kizigo ambayo yote imekauka.
Kwenye mkutano huo wahariri walimueleza mh Makamu wa Rais kwamba kadhia yote hii inatokana na shughuli zakibinadamu zinazofanyika kwenye bonde la Ihefu ambazo ni ufugaji na kilimo ambapo wengi wa watuhumiwa ni familia 12 za vigogo.
Wahariri wameweka wazi kwamba yupo naibu waziri aliwaamuru askari wa uhifadhi aachie kundi la ng'ombe lilokamatwa ifadhini kwenye bonde la Ihefu jambo ambalo linapelekea ugumu kwa wahifadhi kutekeleza majukumu yao.
Mh Rais kuendelea kukumbatia viongozi wa aina hii inatia hasira sana kwa sisi wananchi wako ambao leo tumeingia kwenye kadhia ya mgao wa umeme huku chanzo kikiwa watu wachache ambao wanajali maslahi yao kuliko maslahi ya nchi.
Mh Rais naikumbuka speech moja ya baba wataifa alieleza kuliwahi kuwa na waziri mmoja nchini uingereza alipotuhumiwa tu na kashfa ya umalaya mamlaka yake ya uteuzi ilichagua na kumuapisha mtu mwingine pasipo hata kumjulisha mtuhumiwa.
Nyerere alitaka kuwaeleza mawaziri kwamba wanatakiwa wawe watu safi kwani wao ni kioo, kitendo cha kuwa na kashfa za hovyohovyo ni kosa.
Mh Rais tafadhali huyu naibu waziri hakustahili kuwepo ofisini leo kwani ni siku ya tatu sasa tangu jambo hili liibuliwe na wahiriri.
Tadhali chukueni hatua.
Asante.