Inashangaza kuona Naibu Waziri anaeshutumiwa kuwaamuru askari wa uhifadhi wawaachie ng'ombe waliokamatwa bonde la Ihefu bado yupo ofisini

Inashangaza kuona Naibu Waziri anaeshutumiwa kuwaamuru askari wa uhifadhi wawaachie ng'ombe waliokamatwa bonde la Ihefu bado yupo ofisini

Mashimba anakipi ambacho amekifanya kinachoweza kuonesha ubunifu unaoweza saidia wafugaji kwenye wizara ya mifugo?
Kama mashimba anaona kwamba mifumo iliomuweka ofisini inamkwamisha kwanini hajiuzuru anaendelea kung'ang'ania ofisi?
Nitajie ubunifu wa kila waziri kwenye wizara yake ndipo tupime na kuamua kuwa Mashimba ni mzigo. Vinginevyo yatabakia kuwa majungu na chuki binafsi tu.
 
Moja ya wiraza ambazo kwa miaka mingi huwa zinakosa watu makini basi ni wizara ya mifugo,kama wewe sio mfugaji haya huwezi yajua.

Nchi hii ina maabara chache mno za mifugo kitu ambacho ni kituko.Tena huwenda maabara hizi zipo mikoani tu tena hazipo vizuri kivifaa.

Madtari wetu wa mifugo wanatibu wanyama wetu kama wapiga ramli.
Maabara hizi hazikupaswa kukosekana kwenye ngazi ya wilaya.Najua utaniuliza mbona mtangulizi wake hajazileta, acha wawe wanapigwa chini labda siku moja atapatikana alie timamu.

Tatizo lako unathaminisha ubora wa kiongozi kwakuangalia uzalendo tu,hii haitoshi tunahitaji matokeo.

Huyu mashimba ni mzigo na nakuhakikishia hana safari huyu.Nilishamsikia mama akilalamika mara kwa mara,huyu hana safari.
 
Lazima abakie Ofisini hana soni, na kipindi cha kuusaka ubunge alishatoa rushwa sana hadi chama kikampitisha na wananchi wakampa kulipa fadhila. Sasa unategemea nini?
 
Salaam wanajamvi,

Juzi kulikuwa na mkutano ulioitishwa na wahariri wa vyombo vya habari mkoani Iringa ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mh Makamu wa Rais.

Mkutano huu dhima yake mahususi wahariri walilenga kumpatia Mh Makamu wa Rais taarifa juu ya kile walichobaini nini chanzo cha kukauka kwa mto Ruaha mkuu ambapo yapata siku 120 sasa hautiririshi maji kabisa.

Kwa wasiofahamu mto Ruaha mkuu unachangia 25% ya maji yanayotarajiwa kutumika kwenye bwawa la Mwl Nyerere. Pia mto huu pia ndio chanzo kikuu cha Maji kwenye bwawa la Mtera ukisaidiana na mto Kizigo ambayo yote imekauka.

Kwenye mkutano huo wahariri walimueleza mh Makamu wa Rais kwamba kadhia yote hii inatokana na shughuli zakibinadamu zinazofanyika kwenye bonde la Ihefu ambazo ni ufugaji na kilimo ambapo wengi wa watuhumiwa ni familia 12 za vigogo.

Wahariri wameweka wazi kwamba yupo naibu waziri aliwaamuru askari wa uhifadhi aachie kundi la ng'ombe lilokamatwa ifadhini kwenye bonde la Ihefu jambo ambalo linapelekea ugumu kwa wahifadhi kutekeleza majukumu yao.

Mh Rais kuendelea kukumbatia viongozi wa aina hii inatia hasira sana kwa sisi wananchi wako ambao leo tumeingia kwenye kadhia ya mgao wa umeme huku chanzo kikiwa watu wachache ambao wanajali maslahi yao kuliko maslahi ya nchi.

Mh Rais naikumbuka speech moja ya baba wataifa alieleza kuliwahi kuwa na waziri mmoja nchini uingereza alipotuhumiwa tu na kashfa ya umalaya mamlaka yake ya uteuzi ilichagua na kumuapisha mtu mwingine pasipo hata kumjulisha mtuhumiwa.

Nyerere alitaka kuwaeleza mawaziri kwamba wanatakiwa wawe watu safi kwani wao ni kioo, kitendo cha kuwa na kashfa za hovyohovyo ni kosa.

Mh Rais tafadhali huyu naibu waziri hakustahili kuwepo ofisini leo kwani ni siku ya tatu sasa tangu jambo hili liibuliwe na wahiriri.

Tadhali chukueni hatua.

Asante.
Si mpaka aambiwe na captain? Akitumbua atatumbuliwa pia.
 
Serikali ya mama ni dhaifu sana, ni kibogoyo haina meno ya kung'ata!.
 
Kuna hawa wawili kaswaswadu na mwakibolibo
 
Kila mmoja anajua kuwa kila aliyepo kwenye nafasi ya uongozi wa kuchaguliwa awamu hii ni matokeo ya uharamia uliofanyika kwenye uchaguzi wa 2020. Kusafishika kwao, kwanza yabidi wakiri kuwa wao zao la uharibifu. Pili wajutie wao kuwa zao la uovu. Tatu, wawe na dhamira ya wao wenyewe kubadilika na kuweka mifumo ambayo utazuia njia ovu waluzopitia. Watakaofanya hivyo wanastahili msamaha.
Kwa huu mfumo mbovu hata wewe mkuu leo ungekuwa Rais madudu yangeendelea kama kawaida
 
Back
Top Bottom