Inashangaza: Watu wanamuomba ruhusa Rais Magufuli, badala ya kupewa wanatumbuliwa

Si ndo apo...yaani mtu mmoja ni Mwenyekiti wa Chama,Rais,Mwenyekiti wa Kamati,MNEC,Amiri Jeshi Mkuu,Mkuu Dola...hizi kofia zote jamani.
Kama alikuwa anajua mpaka idadi ya samaki wa baharini na mito...sembuse watu et.... Tunaongozwa na genius
 
Kila mtu kwenye maisha anataka zaidi. Hata Magufuli angeridhika basi mpaka leo angekuwa mwalimu sengerema secondary anasubiri kustaafu na abebe million 80 zake. Acheni hizo.

Kutoridhika kwake ndo maana leo ni Rais.Mtu kaomba ruhusa akashiriki kura za maoni,mpe ruhusa akishindwa atarudi kazini.Akishinda ndo ataresign maana kwa ticket ya CCM huyo mtu kushinda ni asilimia 99.

Kazi ngumu ni kupita kwenye kura za maoni.
 
Wife kwani una ndugu yako ana gombea? Mwambie achague moja! Akishindwa apambane na hali yake na asome halama za nyakati!
Hapana,wanaomba ruhusa kwa sababu wanajua kura za maoni hazina mwenyewe. Wanafanya hivyo kwa sababu wanajua wakipigwa chini kwenye kura za maoni wanarudi kazini.

Tofautisha kumba ruhusa na kujiuzulu.
 
Wanaomba ruhusa ya siku kadhaa,badala ya kupewa ruhusa wanakuwa replaced. Ina maana wakishindwa kura za maoni ndo basi tena.
Ohoooo ingekuwa ni hivyo Magufuli asingekuwa Rais leo. Hiyo methali ni ya kupotosha watu. Aliyeanzisha hakutaka watu wafanikiwe. Ukitaka kufanikiwa lazima ushike hapa, pale,kule.
Mkuu zama zinabadilika ujue, haiwezekani wewe uliteuliwa kuwa IGP, halafu kwa tamaa zako ukaamua kugombea ubunge, Je wakati huo wa mchakato wa uchaguzi nani atakuwa anaserve as IGP!?, In fact lazima mwingine ateuliwe ili aserve as IGP.
 
Cha muhimu ni kumpiga chini Oktoba , msifanye makosa alafu mje kulia lia tena humu.

Madikteta ni watu hatari sana, mwisho wa siku wakipita hawakawii kuomba kuongezewa muda mara katiba ibadirishwe, si umeona Urusi.
Hata Libya mlisema madikteta ni watu hatari, iangilie leo Libya bila Gadafi
 
Mkuu zama zinabadilika ujue, haiwezekani wewe uliteuliwa kuwa IGP, halafu kwa tamaa zako ukaamua kugombea ubunge, Je wakati huo wa mchakato wa uchaguzi nani atakuwa anaserve as IGP!?, In fact lazima mwingine ateuliwe ili aserve as IGP.
Mchakato wa kura za maoni hauna uhakika. Akishindwa kura za maoni anarudi kazini. Akishinda kura za maoni hapo ndo anaresign/anaachia ngazi. Kuliko kuwaachisha kazi mapema namna hii. Wao waliomba ruhusa ila Rais anawaachisha kazi. Sio fair.
 
Hata Libya mlisema madikteta ni watu hatari, iangilie leo Libya bila Gadafi
Kwani Tanzania before Magufuli si ilikuwa na amani tu.Usilinganishe vitu visivyolinganishika. Libya na Tanzania ni context tofauti.
 
Ushapewa nafasi ya kuwatumikia watu utatue matatizo yao ukaona haitoshi, basi anakuvua anakuacha ukasake ile unayotaka. Wale wana tamaa wanawazamils 250 baada ya miakamitano we wadhani mchezo.
 
Hapana,wanaomba ruhusa kwa sababu wanajua kura za maoni hazina mwenyewe. Wanafanya hivyo kwa sababu wanajua wakipigwa chini kwenye kura za maoni wanarudi kazini.
Tofautisha kumba ruhusa na kujiuzulu.
Muda huo wa mchakato wa kura za maoni kazi aliyoiacha itakuwa inafanywa na nani!, Halafu mbona simple tu akiamua kuondoka na nafasi yake inaondoka kuna vijana wengi wanaoweza kufanya kazi, haiwezekani mtu huyo huyo asubiriwe Hadi amalize personal affairs zake halafu arudi kwa kazi....lol
 
Hivi mwanamke akienda martenity leave, kazi zake hufanywa na nani? Siku hizi na technolojia hii unaweza fanya kazi kwa online,pia kuna wasaidizi kibao. Kura za maoni huwa hazichukui muda mrefu. Hata mwezi huwa haufiki.
 
Mchakato wa kura za maoni hauna uhakika. Akishindwa kura za maoni anarudi kazini. Akishinda kura za maoni hapo ndo anaresign/anaachia ngazi. Kuliko kuwaachisha kazi mapema namna hii. Wao waliomba ruhusa ila Rais anawaachisha kazi. Sio fair.
Mkuu unajua ukikaa chini na kujiuliza unagundua kuwa haiwezekani...wewe ukiamua kuondoka Basi na nafasi yako inaenda na wengine. MKUU HEBU KAA CHINI UFIKIRIE utaona kabisa that's unfair.
 
si ninyi wenyewe mmeamua kuiita nchi yetu "Tanzania ya Magufuli" badala ya "Tanzania Yetu"??

kuleni jeuri yenu sasa!
 
Magufuli mwenyewe alienda Chato miezi kama mitatu kipindi cha Coronavirus. Akawa anafanya kazi kwa online ,kutwa kumuelekeza Ummy Mwalimu.
Makonda aka Bashiiiiite mtoto wa Mwalim mkuu!
 
Mkuu unajua ukikaa chini na kuniuliza unagundua kuwa haiwezekani...wewe ukiamua kuondoka Basi na nafasi yako inaenda na wengine. MKUU HEBU KAA CHINI UFIKIRIE utaona kabisa that's unfair.
Inawezekana kaka.Ndo maana wakaomba Ruhusa na sio kajiuzulu. Kwa Magufuli why iliwezekana. Aliomba ruhusa Sengerema secondary kwenda kugombea kura za maoni Biharamulo.

Aliposhindwa kura za maoni akarudi kazini. Kafanya hivyo kwa vipindi viwili mfululizo. Magufuli kashindwa kura za maoni vipindi viwili mfululizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…